Nini kilikusaidia kupata kazi?

Nini kilikusaidia kupata kazi?

Mku iyo kitu toa akilini ukiendelea kuwaza hayo nakuhakikishia hutapeleka barua hata1. Kwanza private unapeleka mwenyewe tofauti na serikalini hadi mpitie utumishi mnapokuwaga watu zaidi ya elfu kumi
ok mkuu
 
Mku iyo kitu toa akilini ukiendelea kuwaza hayo nakuhakikishia hutapeleka barua hata1. Kwanza private unapeleka mwenyewe tofauti na serikalini hadi mpitie utumishi mnapokuwaga watu zaidi ya elfu kumi
kwahiyo ulipokuwa unapeleka kuomba intern au kazi
 
Vipi kusambaza CVs na application letters kwa email kwa taasisi zilizo mbali na unapoishi kuna ambae imeshamsaidia njia hiyo ?
Yes, Mimi ni mmoja wa watu iliyonisaidia..Now nipo kwenye kazi yangu ya kwanza toka nimalize chuo mwaka jana, bado sijaajiliwa fully ila ni half internship half employed...Asubuhi moja ya december 2019, niliamka kitandani nikiwa nawaza kesho yangu. Nilichofanya nikuchukua simu, kusearch na kutuma application kwa email kwenye kampuni nilizochagua.. Mungu si athumani ndani ya masaa mawili nilitumiwa email ya kuitwa ofisini kwajili ya mazungumzo. Bahati nzuri ofisi ipo moa ninaoishi so it was easy...Ndio leo nipo hapa..offcourse, ndoto yangu kubwa ni kufanya kazi na international organization... I hope Mungu atafungua muda ukifika...
 
Once again, please be informed we have advertised the following positions:
Child Rights Governance Specialist – Dar es SalaamFinance Officer – Kibondo, KigomaProcurement Officer (Buying) – Kibondo, KigomaProcurement Coordinator (Sourcing) – Kibondo, Kigoma

Kindly share the link with your network and encourage qualified candidates to apply. https://tanzania.savethechildren.net/careers

Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
thanks a lot
 
nimcheki naona zinazohitajika ila mimi ni Bsc computer science sipo
 
Yes, Mimi ni mmoja wa watu iliyonisaidia..Now nipo kwenye kazi yangu ya kwanza toka nimalize chuo mwaka jana, bado sijaajiliwa fully ila ni half internship half employed...Asubuhi moja ya december 2019, niliamka kitandani nikiwa nawaza kesho yangu. Nilichofanya nikuchukua simu, kusearch na kutuma application kwa email kwenye kampuni nilizochagua.. Mungu si athumani ndani ya masaa mawili nilitumiwa email ya kuitwa ofisini kwajili ya mazungumzo. Bahati nzuri ofisi ipo moa ninaoishi so it was easy...Ndio leo nipo hapa..offcourse, ndoto yangu kubwa ni kufanya kazi na international organization... I hope Mungu atafungua muda ukifika...
Mkuu kwa maana ya kwamba unatuma CV pamoja tu? na ni mpaka iwe kuna kazi imetangazwa au hata kama hawajatangaza kazi unatuma tuu?? Msaada please apo
 
Kusambaza CV ofisi nilizokua najua kuna kazi za profession yangu kwa private institutions; then UTUMISHI kwa kazi za serikalini; sikuwahi kutumia connection ya mtu wala kutoa rushwa/takrima ili kupata kazi..!
 
Mkuu kwa maana ya kwamba unatuma CV pamoja tu? na ni mpaka iwe kuna kazi imetangazwa au hata kama hawajatangaza kazi unatuma tuu?? Msaada please apo
Mkuu...hakukuwa na kazi iliyokuwa imetangazwa..nilikuwa natuma tu kujaribu bahati kuomba nafasi ya internship au kujitolea.....Kitu kimoja nilichokuja kugundua pale ofisini (miezi 2 baada ya kuanza kazi) ni kuwa walikuwa wana mpango wa kutafuta mtu ndio walikuwa wanajiandaa kutangaza..so kumbe nilipotuma kuomba nafasi wakaamua tu kunichukua direct na wala hawakutangaza tena...All the best mkuu.
 
Ahsante kwa mchango mkuu , so kwenye barua unaandika kuomba internship au sio
 
Nilitaka niandike Uzi kuhusu Maswala ya Ajira etc..

Mie ni kijana bdo.

Wakat nasoma nilitamani kuajiriwa nikiwa BADO nikiwa nasoma Chuo.
Nilikosa kazi.. kwa miaka miwili mwaka wa pili ilikuw ni semester ya mwisho lazima Tufanye FIELD.

Nikaitumia hiyo FURSA.. kujijengea JINA, CONNECTION na UAMINIFU. ktk Taasisi nyeti niliyoenda kufanya Field.

Sikufichi.. wenzangu niliosoma nao Asilimia 70% walienda kufanya Field ilimradi wakamilishe Field report yao basi.. ila hawakuwaza mbele..

Mie nilitarget sehem ambay itaniwezesha kubaki kuendelea kufanya kazi.. na nikajituma kias kwamba siku nakamilisha Field yangu.. OFISI/IDARA nzima inasikitika.. wanatamani nibaki.

Inshort.

Fursa namba moja ukitaka uajiriwe.. ITUMIE FIELD vzr... Piga KAZI kweli kweli.

Pili.. Usiwe MTu wa kuwaza HELA.. yaan unataka ULIPWE ukishagundulika hivy wakat wa Field.. imekula kwako.

Tatu.. SOFT SKILLS.. ukiachia hizo skills kitu kingine cha muhimu UJUZI ulio nje ya kile unavhofanyia field.

Mfano. mimi wakat nafany Field kina baadhi ya wafanyakazi walidhani mimi ni IT wa IDARA.. kumbe siyo Profession yangu... Bali nilitumia vzr skills zangu za IT na kutatua changamoto mbalimbali.. kitu ambacho kilinipa Credit sana..

Kuwa mtulivu.. smart.. na mnyenyekevu.

After kumaliza Field KWA Kuwa MABOSS nishawafanya marafiki na wameona Utendaji kazi wangu.. after one week nikavutiwa WAYA... nikaripot SOMEWHERE.. ndipo nipo kwa SASA natumikia TAIFA.
Wewe unaitwa kimbelembele. [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nimemaliza chuo 2016.

Nimepigika kitaa bila kazi karibia mwaka mzima.

2017 mwezi wa Sita mshikaji wangu akanipigia simu kuna sehemu wanahitaji mtu wa taaluma yako. Nikapeleka CV isiyo na experience [emoji23]

Wakanipa nafasi ya kuanza kazi ila mshahara mdogo kweli. Nimerudi nyumbani bi mkubwa anauliza vipi huko imekuwaje nikamueleza nafasi ipo ila mshahara mdogo[400K] hivyo sitaenda kufanya. Bimkubwa akaniambia usiache hiyo kazi nenda kafanye. Ni rahisi kupata kazi ukiwa kazini kuliko ukiwa nyumbani.

Nikaanza kazi. Kama alivyo niambia bi mkubwa ni rahisi kupata kazi ukiwa na kazi ikawa kweli. Hapo ni kafanya kazi mda si mrefu nikapata sehemu inayolipa vizuri [emoji1488] Ikafikia kipindi hadi kazi nikawa nazikataa [emoji23]

Kuna siku jamaa kanitumia tangazo la kazi kwa vile CV nilikuwa nayo kwenye simu nikatuma ila sikuwa na lengo la kuacha nilipokuwa. Nikaitwa kwenye interview si kwenda.

Saa tano wakati nipo kazini HR wa hiyo kampuni ananipiga simu ananiuliza mbona sijaenda kwenye interview wakati wengine wapo wanaendelea na interview nikamueleza niko kazini. Huwezi akaniuliza wanakulipa shi ngapi wao wakanipa mara mbili nikaanza kazi.

Sasa hivi nipo serikalini shirika moja wapo kubwa la umma nakula maisha tu [emoji23]

Maneno ya mama ya kuwa ukiwa kazini ni rahisi kupata kazi yamekuwa halisi Sana kwenye maisha yangu. [emoji1488]
 
Bahati tu na Mungu

CV yangu hakuna mahali naweza tuma nisiitwe, NASEMA HAKUNA TZ HII UTUMISHI SIJAWAHI OMBA KAZI NISIITWE

Ishu kwangu ni Kujieleza, yaani hapo huwa nakua kama kuku aliemwagiwa maji. Kiingereza kinanisalitigi sana

Ila Mungu mwema siku nafanya usaili wa Oral wakaniuliza kiswahili maswali kama 4
😅😃....daaah unanikumbusha mbali sana adi leo Kwenye oral nikiona panel ya wale jamaa kiingereza kinanitoroka,na sijawahi bahatika kupata ya kiswahili.

Vipi lakini walikuajiri?
 
...pia wakuu mliopata kazi msisahau kutupa infor juu ya kazi mlizopata,

je mnajihisi kuridhika na hizo kazi au ndo mnatamani kuacha Ili mjiajiri kama wengne wanavyosema?

Vipi changamoto mnazozipata ktk kufikia ndoto zetu haswa swala zima la mafanikio ( owning your assets or business).

Na vipi kuhusu maswala ya kiafya (mwili,akili na roho),je afya zinaimarika au zinazorota?

Lengo ni kujua hasa kwa Sisi tunaotafuta njia za kuingia uku....Ili tujiandae na tufanye maamuzi sahihi.
 
Back
Top Bottom