SoC01 Nini kifanyike Tanzania iwe miongoni mwa nchi zilizoendelea duniani?

Stories of Change - 2021 Competition

The patriotic

Member
Aug 7, 2021
25
22
Tanzania ni nchi katika dunia au Bara lá afrika ambayo ina kila rasilimali zinazohitajika katika maendeleo mfano madini,Ardhi nzuri, watu wachapakazi na vivutio vingi vya utalii

Pamoja na hayo bado nchi ya Tanzania umaskini ni jambo lililokithiri sana hususa ni kwa vijana jambo linalopelekea pamoja na kuwa na rasilimali bado watu wake hawanufaiki kutokana na rasilimali zilizopo katika sehemu mbalimbali Jambo ambalo nimeona vema nitoe mawazo ya namna gani nchi inaweza kusonga mbele

Yafuatayo ni mambo yanayoweza kutusaidia Tanzânia kuendelea na kuwa nchi ya uchumi mkubwa duniani
nitaelezea mikakati inayohitajika kiuchumi,kijamii na kusiasa:

KISIASA

Ili Tanzania iendelee na kuwa miongoni mwa nchi zilizopo duniani lazima yafanyike mambo yafuatayo;

Serikali ianzishe mchakato wa katiba mpya ili kuthibiti nidhamu kwa viongozi, Tanzania fedha nyingi ambazo zilikuwa zitumike kwa ajili ya maendeleo ya wananchi zimekuwa zikitumika kwa wajanja wachache kwa maslahi yao binafsi ndo maana katiba itaweza kuwabana viongozi juu ya nidhamu ya uwajibikaji katika jamii kufanya hivyo kila kiongozi atakuwa anafanya vizuri ili kuhakikisha fedha za wananchi zinatumika kwa malengo sahihi .

Serikali iwekeze katika ubunifu, sayansi na teknolojia

Katika ulimwengu wa Sasa suala la maendeleo linahitaji ubunifu na pia teknolojia katika kugundua, kuanzisha au kuendeleza teknolojia iliyopo vijana au watu wengi Tanzania wamekosa watu wa kuwashika mkono katika ubunifu wao

Serikali iunde tume ya kuchunguza umuhimu wa miradi kabla ya kuanzisha, Tanzania Kama umekuwa ukifuatilia miradi mingi ya serikali baada ya kujengwa imekufa kwa sababu sio kipaumbele kwa wananchi.

Mfano mkoa wa Njombe baadhi ya masoko mfano Dodoma na Joshoni watu wamegoma kwenda kwa sababu wamesema maeneo hayo sio mazuri kibiashara hapo tunaona upotevu mkubwa wa rasilimali za Kitanzania kwa hiyo ni vema iundwe bodi ili kuhakikisha kabla ya ujenzi kunamaelezo sahihi

Viongozi waache kutumika kisiasa kwa mrengo wa nchi zilizoendelea na kuathili maslahi kwa wananchi,nchi nyingi duniani na zilizoendelea mfano Uingereza,Marekani na Ufaransa zimekuwa zikitumika kuleta migogoro na agenda zao binafsi kwa lengo la kuthibiti na kudumaza maendeleo nchini

Mfano,Mkakati wa uzazi wa mpango nchi isipokuwa na maono inaweza kuwa chanzo Cha umaskini Afrika hususa Tanzania swali la kujiuliza.

Je, kweli Tanzania nchi imejaaa? Mbona China wanaongeza idadi ya watoto na mtu azae watu watatu? Lazima Serikali ije na majibu

Ziundwe tume zitakazo simamia ubora,kufanyika na utekelezwaji wa miradi .Tanzania miradi mingi huanzishwa lakini ukaguzi wa miradi mala nyingi Hadi apitie Raisi,Waziri mkuu au makamu wa Raisi kwa hiyo miradi mingi ya serikali inapotea pamoja na kutumika fedha nyingi kwa hiyo iwepo tume za kusimamia miradi

Serikali iunde mfumo utakaofanya siasa isiwe propaganda na iwe mfumo rasmi utekelezaji wa ilani iliopo, Kwa Tanzania hii mtu anaweza kuongea Jambo baada ya mda anaenda kinyume na alivyozungumza Bila ya kuwa na maelezo maalumu kwa sababu siasa imekuwa mchezo mchafu hata kwa mambo ya msingi

Mfano: Suala la Corona halihitaji siasa Bali ni utekelezaji tatizo siasa zimeingia hadi kwenye taaluma.

Raisi aajili au achague viongozi kulingana na taaluma yake, Maajabu ya Tanzania unaweza kukuta waziri wa sheria amesomea udaktari wa madawa kwa hiyo si lahisi kutekeleza majukumu yake vizuri

KIUCHUMI

Nchi ibuni miradi itakayowezesha nchi mbalimbali kiutegemea Tanzania.

Miradi ya kiuchumi itakayowezesha nchi mbalimbali kutegemea Tanzania Mfano kilimo Cha mazao ya kibiashara mfano kahawa, miwa, pamba, maharage hususa ni soya ambayo nchi mbalimbali zinayategemea katika Viwanda

Sekta ya utalii iboreshe, Tanzania ni moja ya nchi zenye vivutio vingi duniani Ila Maajabu yake nchi Kama Rwanda inaizidi Tanzania katika kutangaza vivutio vya watalii ili maendeleo yaje tunayofursa ya kutangaza vivutio duniani kote na kuhakikisha dunia nzima inaifahamu Tanzania na utajiri

20210825_164132.jpg



Rwanda ni nchi ndogo lakini inatuzidi katika utalii.

Uwekwe mfumo wa uwezeshwaji wa maendeleo kwa vijana
Vijana ndio nguvu kazi katika maendeleo ya nchi yeyote, mfuko wa uwezeshwaji utalenga kutatua changamoto za vijana na ajira mfano mtaji,elimu na maisha ili kuweza kukabiliana na changamoto ya umaskini na Ukosefu wa ajira kwa vijana

Kuboresha sekta ya viwanda Tanzania
Tanzania tuna kila malighafi katika kufanikisha shughuli za viwanda tuna vibarua wakutosha pia tuna wasomi pia mazao karibia yote yanalimwa duniani yanastawi Tanzania kwa hiyo nchi iwekeze au watu wawekeze katika Viwanda vikubwa na vidogo

Kuboresha sekta ya uwekezaji, wawekezaji wengi wamekuwa wakija Tanzania na kufaidika wao pamoja na uwekezaji wao
Mfano mwekezaji kutoka Uingereza anakuja Tanzania. Je, nchi inafaidikaje?

Kwa hiyo, tunaweza kumpa vigezo ili awekeze kwenye madini lazima ajenge shule na barabara kufanya hivyo kutasaidia kuleta maendeleo

Elimu ya Kodi ni muhimu kwa wananchi
Tanzânia hii Mara nyingi serikali imekuwa ikianzisha vitu pasipo kushilikisha wananchi ambao ndio wadau muhimu kwa maendeleo

Mfano: Tozo za miamala zimekuwa gumzo na zimeanzishwa pasipo wadau mbalimbali kushilikishwa

NB: TRA ibuni mbinu zitazowezesha wananchi wengi kulipa Kodi .

Kupeleka wapelelezi wa uchumi nchi zilizoendelea(spy)
Hii inaweza kuwa mbinu ambayo viongozi Tanzania kupeleka wasomi wa uchumi kuishi na kujifunza nchi zilizoendelea mfano Uingereza, Italia, Marekani na China

Kutengeneza mfumo wa kimasoko nje ya Tanzania,Jambo hili lihusishwe wataalamu wa uchumi,wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa maendeleo kufanya hivyo kutapelekea bidhaa zetu kuuzika mahalo popote duniani

KIJAMII

Ianzishwe mitandao ya kijamii ili itumike kutambulisha Tanzania na Afrika na serikali iunde mkono. Mfano mtandao kama JF unaweza kupewa promosheni na Serikali kama mtandao wenye nguvu na kutumika Afrika nzima kwa ajili ya kuweka Mambo ya Tanzania

Inaweza kutungwa Sheria kwamba mitandao mingine kama Facebook, Twitter na Whatsapp haitaruhusiwa kutumika pasipo kuwa na ubia na JamiiForums; kufanya hivi kutainua nguvu ya ushawishi.

Kidhibiti Vyombo vya habari vinavyotumika kueneza propaganda za wageni kwa lengo la kudumaza Tanzania,baadhi ya Vyombo vya habari vimekuwa vikitumika kuua siasa za Tanzania na Afrika kwa ujumla Vyombo vya habari Kama hivyo vidhibitiwe.

Jamii ipewe mitaji na elimu ya matumizi ya rasilimali
Ili kuchochea maendeleo jamii ipewe elimu juu ya matumizi ya rasilimali na ianzishe bodi ya kutoa wataalamu namna ya matumizi ya rasilimali.

Mitaala ya elimu ya kikoloni hii ubadilishwe au serikali Ione namna ya kuwa na elimu ya vitendo zaidi itakayowezesha vijana Kujiajiri, Elimu ya mzungu nzuri kwa sababu inatufanya tujue kinachohusisha duniani pamoja na hayo Ina mapungufu katika kufanya vijana kujitegemea na inaongeza utegemezi kwa mataifa ya kigeni Kama Marekani na Uingereza

Hitimisho

Maendeleo kwa nchi Kama Tanzania inawezekana ni suala lá watanzania wenyewe kuamua.

KARIBUNI KURA YAKO MUHIMU
Asante
 
Jibu liko wazi kabisa, ili Tanzania ya leo iweze kuendelea ni lazima CCM itolewe madarakani kwanza. Ni lazima CCM itolewe madarakani, hilo ni kwa sababu mtaji mkuu wa CCM kukaa madarakani mpaka leo hii ni umaskini, ujinga, woga na unyonge wa watanzania.
 
Suluhisho ni moja tu,ni kukamata maccm yote yaliyopo serikalini na kuyatia jera.vunja bunge,fukuza wabunge wote wa sasa hv.
Weka Katiba mpya tuanze upya.
 
Suluhisho ni moja tu,ni kukamata maccm yote yaliyopo serikalini na kuyatia jera.vunja bunge,fukuza wabunge wote wa sasa hv.
Weka Katiba mpya tuanze upya.
Kweli mkuu tunahitaji mapinduzi makubwa sisi tuna kila kitu si maskini na wakuonewa kwenye tozo
 
Jibu liko wazi kabisa, ili Tanzania ya leo iweze kuendelea ni lazima CCM itolewe madarakani kwanza. Ni lazima CCM itolewe madarakani, hilo ni kwa sababu mtaji mkuu wa CCM kukaa madarakani mpaka leo hii ni umaskini, ujinga, woga na unyonge wa watanzania.
Kweli mkuu tufanye Nini ili mapinduzi yafanyike ya uongozi
Pia usisahau kura kiongozi
 
Kazi nzuri na nishaweka tayari kura hapa💪🏻💪🏻👍🏻
 
Serikali iwekeze katika elimu halisi
Achana na hii elimu fake wanayotulisha Watanzania Ili tuendelee kuwa wajinga watutawale kirahisi

CCM na Serikali yake wanajua madhara yatakayowapata Watanzania wakipata elimu shindani {competitive education}
Hii Elimu tunayowapa Wananchi wetu hawawezi kufanya international interview yeyote labda v/s Burundi au Zimbabwe
 
Serikali iwekeze katika elimu halisi
Achana na hii elimu fake wanayotulisha Watanzania Ili tuendelee kuwa wajinga watutawale kirahisi

CCM na Serikali yake wanajua madhara yatakayowapata Watanzania wakipata elimu shindani {competitive education}
Hii Elimu tunayowapa Wananchi wetu hawawezi kufanya international interview yeyote labda v/s Burundi au Zimbabwe
 
Back
Top Bottom