Nini kifanyike kuboresha Uhusiano kati ya Raia na Vyombo vya Usalama?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
626
938
IMG_20230723_092619_624.jpg


Je, una maoni au ushauri utakaoboresha uhusiano kati ya Raia na Vyombo vya Usalama?

Usikose kujiunga nasi katika mjadala wenye tija utakaolenga kutafuta suluhu ya kuimarisha uhusiano kati ya raia na Vyombo vya Usalama Julai 25, 2023, kuanzia Saa 12 Jioni hadi 2 Usiku, kupitia Twitter Space ya JamiiForums

Fuata 'link' hii kujunga https://twitter.com/i/spaces/1rmGPkkeoVnKN

Pia unaweza kutoa maoni yako kwenye uzi huu yatasomwa siku ya mjadala.

Tunasikiliza sauti yako!

====
MJADALA UMEANZA
Tito Magoti
Hatuna fursa ya kuliwajibisha Jeshi la Polisi, nafasi hiyo ni ndogo sana labda wakati mamlaka inapoamua yenyewe. Jeshi hilo linafanya kazi katika Mazingira ya kizamani na ndio maana linahitaji maboresho

Mfano matumizi ya nguvu, ndio maana ni Watu wachache sana wenye imani ya kutoa taarifa Polisi, kwa kuwa anaweza kufika Polisi na akageuziwa kibao.

Tunahitaji kuboresha kwa kuwa uhusiano baina ya Wanausalama na raia sio mzuri, nitazungumza zaidi kuhusu Polisi kwa kuwa ndio tunahusiana nao kwa ukaribu.

Tulipokea Jeshi la Polisi baada ya Wakoloni kuondoka lakini hatukuwa tumejiandaa baada ya uhuru, uendeshaji uliopo sasa ni kama uleule ambao umekuwepo kabla ya uhuru.

Fatma Karume
Jeshi limeshindwa kujitoa kwenye siasa. Jinsi polisi wanavyotazama watuhumiwa sio professional, wanavyorundika mahabusu, wanavyowatendea watuhumiwa sio vizuri.

Pia jinsi polisi wanavyoandika statements, wanashindwa kuhoji mtuhumiwa hata kwa video? Hivi ni vitu vinaleta matatizo na kufanya polisi wasiaminike.m

William Maduhu
Kwanza niweke wazi kwamba sitaki kutupa lawana kwa jeshi la polisi kama taasisi, mapungufu mengi yapo kwa mtu mmoja mmoja (kwa majeshi yote).

Shida yangu kubwa ni mtu mmoja mmoja, ukisoma sheria zetu tunayo PGO na sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, vyote vinaweka msingi kwa polisi kwenye kufanya majukumu yao.

Mfano, ukamataji na upekuzi umewekewa taratibu nzuri. Sheria ilijua matatizo yetu waswahili ndo maana kukawa na nyaraka ya ukaguzi na mashahidi. Lakini bahati mbaya sana yote hata hayafanyiki.

Hata kwenye kumhoji mtuhumiwa sheria imesema ahojiwe ndani ya masaa 4, lakini wanawahoji baada ya siku 3, 7 au zaidi.

Boniface Jacob (Meya Mstaafu CHADEMA)
Nini kifanyike kuweka uhusiano sawa kati ya Raia na Vyombo vya Usalama ni maboresho ya #Katiba

Mfano Afisa Usalama anapoambiwa nenda kadhibiti Maandamano sehemu fulani, hana uwezo na kinga ya kubisha kuwa hicho anachokifanya kinakiunga Sheria.

Anachoweza kufanya ni kutekeleza kile anachoagizwa bila kujali kuwa alichoagizwa ni sawa au si sawa.

Afisa wa Usalama anapogoma kutii kile anachoambiwa na Mkuu wake kama ni kibaya kuna kinga gani ya kumlinda? Inapotokea hali hiyo imesababisha Askari wengi kuwa upande wa Viongozi wao na kusababisha kutotenda haki hata kama wanajua wanachofanya si sawa.

Kitu kingine kinachotumika kama fimbo ni katika maslahi ya Askari, kuna viongozi ambao wanatumia nafasi hiyo kuwa kama sehemu ya kuwafanya Askari watekeleza kile ambacho ni maelekezo hata kama wanajua wanachokifanya si sawa.

Afisa wa Usalama anapogoma kutii kile anachoambiwa na Mkuu wake kama ni kibaya kuna kinga gani ya kumlinda? Inapotokea hali hiyo imesababisha Askari wengi kuwa upande wa Viongozi wao na kusababisha kutotenda haki hata kama wanajua wanachofanya si sawa.

Fatma Karume
Uboreshaji wa uhusiano unakuja kama kuna imani kati ya Wananchi na Vyombo vya Usalama, kila uwazi ukiwepo imani inazidi, ukiwa haupo na imani pia inashuka.

Hivyo, tukitumia vifaa vya digitali itasaidia kupunguza msuguano kati ya Polisi na Watuhumiwa, kwanini Serikali inashindwa kuweka vitu kama hivyo wakati ni gharama ndogo sana?

Tunashindwa kuweka CCTV Kamera kwenye vyumba vya mahojiano ya Watuhumiwa?

Mkuu wa Jeshi la Polisi anatakiwa kusisitiza hilo kwa Serikali, ni jambo muhimu na linaloweza kuwa na msaada mkubwa kwa Jeshi la Polisi.

Elonlust
Askari wengi wanaishi maisha magumu na hao ndio wanatumika kuwabeba Wanasiasa ambao wanashindwa kuwasaidia Polisi kuishi katika mazingira mazuri, hali hiyo inachangia wengi wao wapelekeshwe na kushindwa kusimamia misingi.

Twende Sawa
Jeshi la Polisi na Maafisa wake wanatengenezwa katika misingi ya kinidhamu, popote pale Duniani hivyo ndivyo ilivyo.

Pamoja na hivyo kuna raia wanashindwa kuwapa heshima inayotakiwa ndio maana inapotokea hali hiyo lazima mtapishana.

Ado Shaibu (Katibu Mkuu ACT Wazalendo)
Ili uhusiano ujengeke vizuri kati ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Raia lazima kuwe na hali ya kuaminiana ambayo imepotea.

Hata sisi Wanasiasa tukiona kuna Askari wengi kwenye mikutano yetu tunaona kama uwepo wao ni kwa ajili ya kuvuruga Amani au kuwatisha Raia.

Hali ya kutoaminiana imechangiwa na Jeshi la Polisi kushindwa kubadilika, lilivyokuwa wakati wa ukoloni na ilivyo sasa.

Mtanzamo wa Majeshi yetu ya wakati wa ukoloni na hali ilivyo sasa haujabadilika, kuanzia katika Mafunzo hadi Saikolojia.

Chato 1
Ukiwa mkutanoni ukaona Askari wengi imani inapotea na kujua kuwa hakutakuwa na amani.

Nashauri Jeshi la Polisi na Vyombo vya Usalama kwa jumla wajikite katika weledi kuliko kutumiwa na Wanasiasa ambao mwisho wa siku wanawatengenezea matatizo kati yao na raia.

Pablo East
Saikolojia ya Maafisa wa Vyombo vya Usalama haiko sawa kutokana na mazingira ambayo wanakutana nayo katika majukumu yao ya kila siku.

Hali hiyo inawafanya hata wao kutokuwa na lugha rafiki au uhusiano mzuri na Wananchi kwa kuwa mtaani inaaminika ukianza kushirikiana na Askari basi umejiingiza kwenye matatizo.

Changamoto nyingine ni Vyombo vya Usalama kuwa na mazingira ya rushwa, hiyo ni changamoto kubwa

Kuna mzee wangu mmoja aliwahi kuniambia zamani hata ukipotea unaenda Kituo cha Polisi na unapata msaada, sasa hivi ikitokea hivyo ukaenda utakutana na mazingira magumu sana ikiwemo maswali mengi na hata mwisho wake unaweza kuingia matatizoni.

Wanausalama wamepata mafunzo, wao ndio wana nafasi kubwa ya kujirekebisha na kuhakikisha wanarudisha uhusiano kwa raia kwa kuwa wana mafunzo maalum na wanajua nini kinatakiwa kifanyike licha ya kutambua ukweli kuwa Sheria nazo zina changamoto kadhaa.
 
Uhusiano hauwezi kuboresheka ikiwa vyombo vya usalama havitaacha rushwa na uonevu, kulazimisha makosa, na wasimamizi kutokuacha kubambika watu makosa badala ya kutoa Elimu.
 
Yaani kampeni hii ianzie kwa mods wa jf na members wake. Hakuna Uhuru humu, pia kuna ukabila kwa hawa mods
 
Vyombo vya usalama ni taasisi muhimu mno nchini, tatizo ni matumizi makubwa ya nguvu kuliko Akili, Hizi taasisi zifanywe kuwa service not forces
 
Wapo wanaofanya vema, lakini wengi sio rational,
Wanatakiwa waondoe neno "force" waweke " services" , labda itawasaidia kujua wanapaswa kutoa huduma zaidi kuliko nguvu bila logic
 
Tatizo kubwa ni katiba. Vyombo vya usalama vinajiona navyo ni sehemu ya waliomadarakani yaani kutetea maslai ya wanasiasa. Katiba mpya ni muhimu.
 
Write your reply, Tatizo ni kwamba waliopewa nyadhifa hizo ndiyo wanao haribu kwa mambo yafutayo 1. Rushwa 2 onevu 3. Unanijuwa mi nani. Yakiisha hayo mbona hakuna shida jamani, haki ndiyo kila kitu, fuata haki uone kama kutakuwa na tatizo.
 
Back
Top Bottom