Ushauri: Vituo vya Polisi viitwe Vituo vya Usalama wa Raia na Mali zake

Swahili AI

JF-Expert Member
Mar 2, 2016
6,195
46,806
Naona kila kona vituo vya polisi vimeandikwa " Kituo cha Polisi" kisha kufuatiwa na jina la mahala lilipo.

Sasa swali la kujiuliza, raia anamfuata polisi ama usalama wake pamoja na mali zake.

Nashauri vibadilishwe majina na kuitwa vituo vya usalama wa raia na mali zake.

Hii iitaboresha uhusiano kati ya raia na polisi.

Kituo ni mahala pa kupata usalama na sio kukutana na polisi

Ova.
 
Nashauri vibadilishwe majina na kuitwa vituo vya usalama wa raia na mali zake.
Pale Magomeni walishaanza kitambo panaitwa Magomeni Usalama
Nahisi usalama upo kikweli maana kwa pembeni kidogo kuna jogoo hana wasiwasi ya kufanywa chochote
 
Bila ya kubadilika kwa mentality ya hao Walinzi wa Usalama wa Raia na Mali zao, hata waite nini hivyo vituo vitaendelea kuwa majanga tu.

Anaepaswa kukulinda anakuona wewe muhanga kama fursa. Unaenda kushtaki umeibiwa na mwizi unamjua, anakwambia ongeza Maziro kwenye kiasi ulichoibiwa, cha juu chake. Sasa hao walinzi au madalali.

Ingeleeta maana zaidi wangeandika Kituo cha Madalali wa Jinai.
 
hao wenyewe ukienda ndani ndg zako wamekuletea pilau hawakupi wanakula wao afh we wanakumegea ugali😂😂 wanakupa mikate na juis
 
KUINGIA POLISI NI BURE, KUTOKA NI HELA

Back
Top Bottom