Nini hatma ya TCU baada ya kauli ya Rais Magufuli?

ni kweli kabisa yani mambo yao ya second round mpaka fifth round ni utapeli mkubwa sana na ni wauaji kabisa wa ndoto za wanafunzi...
Hawa walikuwa wakala wa vyuo flani. Wanaanza kujaza vyuo hivyo kwanza alafu ndio wapangiwe wa govt. Kwa sasa ni competence ya chuo ndio itakayo matter kwa wanafunzi na wazazi.

Ile tabia ya watoto wa masikini kuwapangia mavyuo ya private utakuwa ndio mwisho. Mtoto kakomaa amepata one kali unampangia lichuo ada 15m
 
Bora angesema Tcu ifuate matakwa ya waombaji

Mfano mfumo wa Tcu unamruhusu mwanafunzi kupendekeza chuo unachotaka kusoma visizidi vitatu

Katika hivyo vitatu mwanafunzi hata akichaguliwa haina tatizo kwa sababu kachagua yeye

Hivyo mh. Rais angeshaur vyuo vifuate maombi ya mwanafunzi kwenye selection
Tcu haina maana yoyote, ifutwe yote nzima nzima. Kwani si nihawahawa ndio waliovipa sifa ya university taasisi ambazo nikama tuition centers?
 
Unawezaje ku control doublication ya wanafunzi? Ya mwanafumzi kuchaguliwa zaid ya chuo kimoja? Nadhani hii ilikuwa moja ya msingi wa CAS sasa tunaotoa kawqzo yetu jukwaani tufikiri na hii
Kila mwanafunzi ataamua aende wapi. Huko atakapo enda kama ni bodi itamfuata hukohuko. Ukiona umedahili wengi na wamekuja wachache hasa wale wa hovyohovyo ujue ndio uwezo wako wakidahili wahovyohovyo
 
Kuna jambo ambalo wengi hatulielewi. TCU hawampangii mtu course (hili si kweli), TCU wanakupangia kutokana na ulichoomba. Shida iliyopo ni competition kubwa.

Unapoomba kozi flani pamoja na watu wengine 1000 wakati capacity ya chuo ni 70 hutapata. TCU kwa kutambua ndoto ya wengi ni kusoma chuo, wanaangalia wapi demand ilikuwa ndogo na qualification zako zimetimia wanakupangia. Its a matter of stay (wakuache) au go for your dream (walau utimize ndoto ya kusoma chuo).

Mpango unaopendekezwa una athari nyingi ambazo watu hawazioni. Ntaanisha chache;

1. Direct application kwenda chuo itaongeza gharama maradufu kwa maana kila chuo utalazimika kulipa application fees, gharama za stationeries etc.

2. Mfumo huu utapelekea watu wengi kukosa fursa ya kusoma elimu ya juu. Mathalani wote wakaomba UDSM, ARU, SUA na UDOM, kitakachotokea mwenye highest qualifications aweza kupata admission vyuo vyote akaziba nafasi za wengine.

Pili kwa kuwa application hufanyika baada ya matokeo ya F6 na muda mdogo kabla ya kufungua chuo, ni wazi atakaekosa vyuo labda vitatu ulivyoomba utachelewa kujua wapi kuna nafasi ukaombe hivyo mwaka huo kukupita na kukuacha mtaani.

3. Mfumo unaopendekezwa utawaacha watoto wa masikini wengi nje ( mfumo huu unaruhusu kupachikana kirahisi kwani kila mtu awe za kuja na majina ya nduguze chuoni kwake). Sambamba na hili la kupachikana kuna tatizo jingine la fedha, ni kweli kwamba bodi ya mikopo eitha haipeleki au huchelewesha kulipa ada za wenye mikopo, kutatua hili vyuo vinaweza kuopt kuchagua wanaojiweza kiuchumi wengi na kuwatupa nje watoto wa walalahoi wengi.

4. Tutatengeneza tatizo kubwa mbeleni la typology ya wanafunzi. Pamoja na TCU kuwa na matatizo wamejitahidi sana kubalance sana diversity ya wanafunzi vyuoni. Athari za direct entry zinaweza kuleta ukabila, chuo flani kimejaza nshomile wengi au wachaga wengi n.k (hii sio tuhuma mpya). Kuna jingine la udini, mathalani SAUT na associates wake wanaweza kujaza wakatoliki chuoni au MUM wakajaza radical islamist watupu na vyuo vingine n.k

5. Quality assurance itakuwa ngumu sana. Nilitegemea TCU waongezewe nguvu ya kuamua kuhusu ubora ikiwa ni pamoja na kupewa mamlaka ya kuamua entry qualification ili kulinda ubora wa vyuo vyetu. Tunarudi kule kule kwenye kila chuo kujiamulia sifa zake, vyuo vidogo na visivyo fahamika vitalazimika kushusha entry qualifications ili kufetch wanafunzi waliobaki (wenye sifa dhaifu) ili kuendelea kuwapo.

Rais ashauliwe vema kuhusu sera au kauli zake kuhusu elimu. Mara zote anapokuwa Mlimani ameonesha waziwazi kupendelea chuo hicho na kuviacha vyuo vingine kama vile si vya serikali au havina umuhimu. Leo inataka kuanzishwa sera ya ajabu ili kuipa UDSM autonomous ya kujiamulia mambo yenyewe, si sera mbaya ila vipi kuhusu vyuo vingine?

Hostels UDSM, Mabasi UDSM vipi wengine hawahitaji mambo hayo? Kwa nini tusiwe na treatment moja kwenye taasisi za elimu ya juu zote?
Mjomba tcu haina maana zaidi ya kuregulate standard ya elimu ya juu kazi ambayo wameshindwa vibaya sana. Wakaona bora waongeze ada ya udahili ili wapige pesa baaasi. Wafutweeeeeeeeee
 
Kuna hivi vyuo vya St.kama mtu hakuomba kwenda St fulani hasilazimishwe kwenda huko.TCU iendane na mahitaji ya muombaji.
 
Kuna hivi vyuo vya St.kama mtu hakuomba kwenda St fulani hasilazimishwe kwenda huko.TCU iendane na mahitaji ya muombaji.

Yani muombaji ana three ya mwishoni anataka aende Petroleum engineering udsm apelekwe tu kisa ni mahitaji yake

Ubaya wa kuiondoa CAS hamuwezi kuuona leo,time will tell
 
Hii itakuwa nzuri sana. Hawa jamaa wa tcu magumashi tu. Hapa hata wale wa posta watapata kazi za kufanya maana hizo bahasha zitakiwa magunia kwa magunia.

Mambo ya system zakuapply online tz bado sana. Siku nzima unakesha kwenye net mtandao unasumbua bwana.

Turudi kwenye kujaza fomu watoto wengi wanamiandiko mibaya kwa kuzoea mitandao. Unatuma posta unasubiria magazeti watoe majina ukanunue gazeti, sio pesa zote kwenye kapu moja, tcu
 
My dear ulikuwa unachagua mwenyewe COURSES 3 na University 3! Hapo inakuwa lazima upate mojawapo ktk machaguo yako!
Sio lazima upate. Wapi wengi wameomba na zote 3 wamekosa kwenye vyuo vyote 3 badala yake wanakupeleka st.mavumbi na namba ya admission officer tcu wanakupa, huu si uhuni sasa?
 
Watu wanao unga mkono kauli ya Rais juu TCU siyo wataalamu wa elimu juu ya mfumo unaotumiwa vigezo ndo vinaelekeza watu kuchaguliwa vyuo husika ,na TCU hailazimishi mtu leo hii suala la mtu kuchaguliwa vyuo zaidi ya viwili limeisha sasa anataka kuturudisha tulikotoka , kauli nyingine hazifai
Huko ulaya ndiko tunakoiga na hakunaga huo ujinga wa central kama tupo polisi. Ukitaka kuomba vyuo UK au USA unaomba kwa chuo husika. Sio mambo yakibebana kama tff.

Kila chuo kijipange kutangaza ubora wa chuo na kuitroduce course ambazo pengine tz hazipo.

Ukiangalia kwenye web za vyuo vingi hakuna online application jambo ambalo ni ujinga. Hakuna hata videos zinazoonyesha umahiri wa chuo, utaona mapicha ya majengo tuuuuuuuuuu
 
Kufutwa udahili wa pamoja inamaanisha gharama zakuaply zitakua kubwa na zitakwenda chuoni moja kwa moja, sasa najua mtu huwezi kuchagua chuo kimoja unless uwe TO, apo kuna kila dalili za kuchagua vyuo zaidi ya vitatu na uwezekano wa kukosa bado upo maana still watu watakimbilia vyuo vyetu pendwa... UDSM, ARDHI, MUHAS, IFM... Watu wanaolalamikia huu mfumo ni wakoloni tu kwakweli wasiopenda mabadiliko yaliyo chanya, kama wanahisi kuna vyuo havina ubora si wa wavifunge tu, tatizo liko wapi.
TCU ni genge la wala rushwa na magu kawastukia mapema. Hakuna haja yakuomba kupitia wakala, tunataka tuombe directly kwenye vyuo.

Magu ifute kabisa hiyo TCU
 
Nasisitiza tena, TCU hawakupangii chuo wao wanachofanya ni kupeleka majina ya watu wenye sifa kama zilivuoanishwa kwenye zile guide books (hizi ni entry points kutoka vyuoni kwenyewe) na kutoka mwenye choices ulizoomba mwenyewe then vyuo vinachagua from majina ambayo wamepewa kutoka TCU.
Sasa kama bawapangi chuo watu wanaomba kwao kufanya nini? Kwani vyuo vimeshindwa kujua nani anasifa na nani hana?

Hao waliosoma zamani walipataje admission zao? Hao jmaa ni moja ya tatizo lakuzorotesha elimu tanzania.

Vyuo nikama klabu za mpira, yanga, azam, simba wanatakiwa wasajili wachezaji wenye viwango qanavyoona vinafaa sio kupangiwa na tff chukua huyu, huyu hafai.

Kila chuo kiweke vigezo vyake ili kufikia malengo yake yaliyojiwekea. UDSM imeshuka vuwango kwa kupelekea magarasa yenye div 3 kwenye kozi za maana. Mitoto haijielewi hata kidogo.
 
Kimsingi Rais hajaifuta TCU,alichosema TCU ibaki na majukumu ya Regulation kwa Elimu ya juu na kuacha swala la Udahili wa pamoja (CAS)
Kwa maagizo hayo system ya Central admission wenda ikafutwa badae na kila mwanafunzi aombe udahili direct chuo husika anachokipenda.

Rejea nukuu hizi;
Mmbea wa jiji:
'Wanafunzi wanalazimishwa kupelekwa kwenye kachuo ambako hakana hata jina'- JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

'Niombe Wizara ya elimu, TCU tubadilishe utaratibu wa kuchagua wanafunzi, wanafunzi wenyewe wachague badala ya TCU'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

'Wakati mwingine wakuu wa vyuo wanaenda TCU kuomba wapangiwe wanafunzi pamoja na kwamba sina ushahidi'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

Rais Magufuli: Ishu si kuwa na vyuo vikuu vingi, ishu ni kuwa na vyuo vichache vinavyotoa wanafunzi wengi wenye vigezo vya juu [HASHTAG]#JFLeo[/HASHTAG]

'Wanafunzi wachague vyuo wanavyovitaka ambavyo havitachaguliwa vife, kwa nini mnalazimisha'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

'Kuna vyuo ambavyo haviko kwenye Standard vina hakikisha vinapata wanafunzi kwa sababu wanapata mkopo'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]
Kujitambua muhimu.kuliko misimamo isiyo na mantiki...
 
Nakuunga mkono si kweli,,
Maana kika chuo kina idadi yake kwa mwaka so kama idadi yao kwa mwaka ni 10 elfu na walioomba ni 15 elfu hao tano elfu watakosa tu na wataomba kwingine so mie sidhan kama kutakua na mlundikano
Kwanza ilivyo aliyepata div 3 hawezi hata kithubutu kuulizia appl form za udsm manake anajua hapati kitu. Ataenda kuomba cert dit ili aje aingie kwa equivalent qualification.

Watajichuja wenyewe bila kuambiwa,
 
Kuna jambo ambalo wengi hatulielewi. TCU hawampangii mtu course (hili si kweli), TCU wanakupangia kutokana na ulichoomba. Shida iliyopo ni competition kubwa.

Unapoomba kozi flani pamoja na watu wengine 1000 wakati capacity ya chuo ni 70 hutapata. TCU kwa kutambua ndoto ya wengi ni kusoma chuo, wanaangalia wapi demand ilikuwa ndogo na qualification zako zimetimia wanakupangia. Its a matter of stay (wakuache) au go for your dream (walau utimize ndoto ya kusoma chuo).

Mpango unaopendekezwa una athari nyingi ambazo watu hawazioni. Ntaanisha chache;

1. Direct application kwenda chuo itaongeza gharama maradufu kwa maana kila chuo utalazimika kulipa application fees, gharama za stationeries etc.

2. Mfumo huu utapelekea watu wengi kukosa fursa ya kusoma elimu ya juu. Mathalani wote wakaomba UDSM, ARU, SUA na UDOM, kitakachotokea mwenye highest qualifications aweza kupata admission vyuo vyote akaziba nafasi za wengine.

Pili kwa kuwa application hufanyika baada ya matokeo ya F6 na muda mdogo kabla ya kufungua chuo, ni wazi atakaekosa vyuo labda vitatu ulivyoomba utachelewa kujua wapi kuna nafasi ukaombe hivyo mwaka huo kukupita na kukuacha mtaani.

3. Mfumo unaopendekezwa utawaacha watoto wa masikini wengi nje ( mfumo huu unaruhusu kupachikana kirahisi kwani kila mtu awe za kuja na majina ya nduguze chuoni kwake). Sambamba na hili la kupachikana kuna tatizo jingine la fedha, ni kweli kwamba bodi ya mikopo eitha haipeleki au huchelewesha kulipa ada za wenye mikopo, kutatua hili vyuo vinaweza kuopt kuchagua wanaojiweza kiuchumi wengi na kuwatupa nje watoto wa walalahoi wengi.

4. Tutatengeneza tatizo kubwa mbeleni la typology ya wanafunzi. Pamoja na TCU kuwa na matatizo wamejitahidi sana kubalance sana diversity ya wanafunzi vyuoni. Athari za direct entry zinaweza kuleta ukabila, chuo flani kimejaza nshomile wengi au wachaga wengi n.k (hii sio tuhuma mpya). Kuna jingine la udini, mathalani SAUT na associates wake wanaweza kujaza wakatoliki chuoni au MUM wakajaza radical islamist watupu na vyuo vingine n.k

5. Quality assurance itakuwa ngumu sana. Nilitegemea TCU waongezewe nguvu ya kuamua kuhusu ubora ikiwa ni pamoja na kupewa mamlaka ya kuamua entry qualification ili kulinda ubora wa vyuo vyetu. Tunarudi kule kule kwenye kila chuo kujiamulia sifa zake, vyuo vidogo na visivyo fahamika vitalazimika kushusha entry qualifications ili kufetch wanafunzi waliobaki (wenye sifa dhaifu) ili kuendelea kuwapo.

Rais ashauliwe vema kuhusu sera au kauli zake kuhusu elimu. Mara zote anapokuwa Mlimani ameonesha waziwazi kupendelea chuo hicho na kuviacha vyuo vingine kama vile si vya serikali au havina umuhimu. Leo inataka kuanzishwa sera ya ajabu ili kuipa UDSM autonomous ya kujiamulia mambo yenyewe, si sera mbaya ila vipi kuhusu vyuo vingine?

Hostels UDSM, Mabasi UDSM vipi wengine hawahitaji mambo hayo? Kwa nini tusiwe na treatment moja kwenye taasisi za elimu ya juu zote?
Hiki unachosema ni ukweli mtupu..Rais angeshauliwa kwanza ili kuwe na system mbadala wa TCU. Tofauti na hilo tutaona watu wengi wenye ufaulu wa chini wakiendelea kukosa vyuo.
 
Back
Top Bottom