Nini hatma ya TCU baada ya kauli ya Rais Magufuli?

24hrs

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,622
5,952
Naombeni tuchangie hatma ya TCU juu ya kufutwa kwake..
----------

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutowachagulia vyuo wanafunzi wa elimu ya juu na kuwaacha wanafunzi hao kuchagua vyuo wanavyovitaka wenyewe.

Agizo hilo limetolewa leo, Jijini Dar es Salaam Rais Magufuli alipokuwa akizindua Mabweni mapya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa Chuoni hapo Juni, mwaka jana.

“Ninaamini kama wanafunzi wangepewa nafasi ya kuchagua vyuo wanavyovipenda wenyewe, vyuo vya Serikali kama vile Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo Kikuu cha Mzumbe vingekuwa na wanafunzi wengi sana,” alisema Dkt. Magufuli.

Aliendelea kwa kusema kuwa TCU imekuwa ikiwachagulia wanafunzi vyuo visivyo na sifa na makazi ya wanafunzi hivyo kusababisha wanafunzi hao kusoma katika mazingira magumu na wanapomaliza masomo yao hukosa ajira kutokana na vyuo hivyo kutokuwa na sifa.

Aidha, Rais Magufuli ameuagiza uongozi wa UDSM kutoza wanafunzi gharama ya shilingi mia tano(500) kama malipo ya makazi ya mabweni hayo kwa siku badala ya shilingi mia nane(800) inayotozwa kwa mabweni mengine yaliyopo chuoni hapo.

Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kuwekeza katika elimu hivyo itahakikisha wanafunzi nchini wananufaika kwa kupata elimu bora kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu.
“watanzania walinichagua ili kutatua changamoto zinazowakabili na hivi ndivyo ninavyofanya kutatua changamoto hizo” alisema Rais Magufuli.

Naye, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amempongeza Rais Magufuli kwa kutoa shilingi bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni hayo ambao kwa kiasi kikubwa yatatatua changamoto ya makazi iliyokuwa ikiwakabili wanafunzi wa chuo hicho.
Prof. Ndalichako amesema kuwa mabweni hayo yamejengwa kwa kipindi cha miezi 8 ambayo yatachukua wanafunzi 3840.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Rwekaza Mukandala ametoa rai kwa wanafunzi wa chuo hicho kuhakikisha wanaimarisha usalama katika maeneo ya mabweni hayo na kulinda miundo mbinu yote iliyoweka.

“Ni lazima mzingatie matumizi sahihi ya kila kifaa kilichofungwa katika majengo haya, majengo haya ni mapya na yamejengwa kwa gharama kubwa kwa lengo la kutusaidia kuondokana na changamato iliyotukabili kwa muda mrefu,” alisema Prof. Mukangala.

Wakati huohuo Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi magomeni “QUARTERS”, mradi ambao kwa asilimia kubwa unawagusa watanzania wa hali ya chini.

Aidha Rais Magufuli ameendelea kusisitiza juu ya ahadi aliyoitoa kwa wakazi 644 waliokuwa wakiishi maeneo hayo kupewa nyumba ambapo wataishi bure kwa muda wa miaka mitano.
Pia, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA) Msanifu Majengo Elvis Mwakalinga amesema ujenzi wa mradi huo umezingatia miundombinu yote iliyohitajika ambapo itakuwa na sehemu za makazi, biashara, maegesho ya magari na bustani ya kupumzikia.

Ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja ambapo ujenzi wake ulianza rasmi Octoba mwaka jana.

Na Lilian Lundo na Beatrice Lyimo
 
naombeni tuchangie hatma ya tcu juu ya kufutwa kwake ....
Kimsingi Rais hajaifuta TCU,alichosema TCU ibaki na majukumu ya Regulation kwa Elimu ya juu na kuacha swala la Udahili wa pamoja (CAS)
Kwa maagizo hayo system ya Central admission wenda ikafutwa badae na kila mwanafunzi aombe udahili direct chuo husika anachokipenda.

Rejea nukuu hizi;
Mmbea wa jiji:
'Wanafunzi wanalazimishwa kupelekwa kwenye kachuo ambako hakana hata jina'- JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

'Niombe Wizara ya elimu, TCU tubadilishe utaratibu wa kuchagua wanafunzi, wanafunzi wenyewe wachague badala ya TCU'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

'Wakati mwingine wakuu wa vyuo wanaenda TCU kuomba wapangiwe wanafunzi pamoja na kwamba sina ushahidi'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

Rais Magufuli: Ishu si kuwa na vyuo vikuu vingi, ishu ni kuwa na vyuo vichache vinavyotoa wanafunzi wengi wenye vigezo vya juu [HASHTAG]#JFLeo[/HASHTAG]

'Wanafunzi wachague vyuo wanavyovitaka ambavyo havitachaguliwa vife, kwa nini mnalazimisha'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

'Kuna vyuo ambavyo haviko kwenye Standard vina hakikisha vinapata wanafunzi kwa sababu wanapata mkopo'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]
 
ohooooo lakini tcu bado ipo ila system yao inafutwa.... cas dah ahueni kwa wanafunzi
 
Tcu haifi Kumbe CAS ndo Umekufa
 
ohooooo lakini tcu bado ipo ila system yao inafutwa.... cas dah ahueni kwa wanafunzi
Nilichelewa mwaka kwa ajili ya tcu

Ila naona elimu inayumba, udahili wa kila ngazi ya elimu lazima uwe mastered na wizara yaan taarifa zote za mwanafunzi ziwe mastered na wizara hapo udahili wa elimu haitayumba
 
ni kweli kabisa yani mambo yao ya second round mpaka fifth round ni utapeli mkubwa sana na ni wauaji kabisa wa ndoto za wanafunzi...
 
Bora angesema Tcu ifuate matakwa ya waombaji

Mfano mfumo wa Tcu unamruhusu mwanafunzi kupendekeza chuo unachotaka kusoma visizidi vitatu

Katika hivyo vitatu mwanafunzi hata akichaguliwa haina tatizo kwa sababu kachagua yeye

Hivyo mh. Rais angeshaur vyuo vifuate maombi ya mwanafunzi kwenye selection
 
naona mwaka wa masomo 2017/2018 utakuja na version mpya kabisa duhh dili la 50,000 kwa kila kichwa linabak chuoni sasa...
Wakati wa kuapply direct kila chuo application fee haikua 50000 bali nakumbuka km ilikua 10000 km sijasahau.
Hata nyakati CAS ikianza application fee ilikua 30000 hivo gharama hizi itakua zinabadilika kulingana na mabadiliko ya kiuchumi.Hivo nadhan application fee itakua regulated ili watu waweze kuapply vyuo mbalimbali
 
ni kweli kabisa ndugu hawa tcu wana maovu hatanikitafakali naona prof mgaya walimuonea sana.. hivi kweli mwaka wa masomo 2016/2017 takribani wanafunzi zaidi ya 8000+ hawakuwa na sifa za kuffanya application kwa mabadiliko ya alama za kujiunga chuo kutoka E mpaka D lakin hajabu yao mwisho wa udahili november yalitoka majina 65,000+ ndio wana funzi waliodahiliwa na tcu haya madudu na wataeleza kiasi hiki chote cha fedha walipeleka wap... kama si kwenye matumbo yao...
 
Back
Top Bottom