University of Dodoma (UDOM)
Public Institution
- Feb 24, 2024
- 50
- 55
Chuo Kikuu cha Dodoma ( UDOM) kupitia Ndaki ya Sayansi za Ardhi na Uhandisi (CoESE) imeendelea kudhihirisha ubora wake kitaifa baada ya andiko lake kuingia katika miongoni mwa maandiko matatu bora kati ya 561 yaliyowasilishwa kwenye shindano la ubunifu wa kupunguza msongamano wa magari mijini lijulikanalo kama Wanafunzi Challenge 2026.
Hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi imefanyika leo, tarehe 10 Mei 2026, katika Ukumbi wa Mabele jijini Dodoma, ikiwakutanisha washiriki kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya juu nchini.
Shindano hilo lilizinduliwa kufuatia changamoto iliyotolewa tarehe 23 Februari 2026 na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega( Mb), wakati wa ziara yake katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Katika ziara hiyo, alitoa wito kwa wanafunzi wa fani za uhandisi, ukadiriaji majengo na ubunifu wa majengo kuja na suluhisho la kudumu la tatizo la msongamano wa magari mijini.
Mafanikio haya yanaendelea kuonesha uimara wa Chuo Kikuu cha Dodoma katika kukuza ubunifu, ushindani na mchango wake katika maendeleo ya kitaifa na kimataifa.