Nini hatma ya TCU baada ya kauli ya Rais Magufuli?

Nini hatma ya TCU baada ya kauli ya Rais Magufuli?

Vyuo vilikuwa vinadahili wanafunzi serikali ndiyo ilifuta wakati huo jmp alikuwa kwenye baraza la mawaziri! Kila wakati elimu ina mhanga wake
Kuwa kwenye baraza la mawaziri ndiyo kuamua jambo au mambo?
 
Ni kweli kabisa , kwani wengine enzi zetu miaka kadhaa iliyopita wakati wa mkuu GEORGE @Nyatega akiwa HESLB tulichaguliwa vyuo zaid ya 3 na mwisho wa siku kuchagua ni chuo gani wataka kujiunga kwa kozi husika uliyoipenda.
 
Hata sasa hivi watu huomba chuo wanachotaka (kuna restriction ya course mbili kwa chuo kimoja), issue kubwa ni grades /point za waombaji. Kama huna point nzuri na chuo kina competition hata ukiomba chuo moja kwa moja hutapata. Sioni kama wazo au agizo la raisi litasaidia na tusipoangalia wengi watatoka na vilio na wataishia kuikumbuka CAS. Wenye ufaulu mzuri watapata watakacho (watachaguliwa kule walikoomba na kujaza nafasi kwenye vyuo vyote walivyo omba, wale wa kawaida itabidi wasubiri vyuo vikifunguliwa wajaze nafasi zilizo achwa na hilo kundi la kwanza, bahati mbaya vyuo vina dead line ya kudahili na ku-register hivo kundi hili kama sio makini watahangaika na admission.
Na hilo la competition kwenye vyuo vizuri ni jambo jema.

Hiyo itamfanya mwanafunzi anayetaka kwenda chuo chenye jina kubwa kufanya bidii zaidi ili aishinde competition iliyopo.Lakin ukitaka ubalance tu moja kwa moja utawavunja moyo wenye bidii.

Hata anayetaka kusoma Cambridge au Harvard lazima awe na marks tofauti na wale wa vyuo vyenye rank ya chini.
 
Ni hotuba nzuri ya leo, ila vyuo vya umma navyo visichukue fursa hii kujiwekea kiburi kwa kuweka alama ngumu ya wanafunzi kudahiliwa. Wangejiandaa kuongeza uwezo wao wa kusomesha Watz wengi zaidi, kushindana katika mchakamchaka wa jumuiya ya afrika mashariki, uwekezaji na soko la ushindani
 
Yaani hapoo.....kasema vizurii ila akomae na TAKUKURU maana Rushwa itakayo kuwepo pale UDSM....Rushwa itakayo kuwepo muhas.....Sua Mzumbee sio ya nchii hii.....ada za Vyuo vya private itashuka kuvutia wanafunzi na comption itakuwepo
 
sidhani kaul ya Maguful ni ya kufuta TCU au kufuta CAS, mwanafunzi hata kupitia CAS anaweza kuomba chuo/vyuo anavyotaka, cha msingi achaguliwe ktk among vyuo alivyoomba, na baadhi ya vyuo viache kwenda kufanya robbing maana wakiona kuna mtu kachagua chuo chao hata kama ni last option na ana sifa ya kupata kile cha first anapangwa huko, hicho ndicho amekata Mh President
 
Ni hotuba nzuri ya leo, ila vyuo vya umma navyo visichukue fursa hii kujiwekea kiburi kwa kuweka alama ngumu ya wanafunzi kudahiliwa. Wangejiandaa kuongeza uwezo wao wa kusomesha Watz wengi zaidi, kushindana katika mchakamchaka wa jumuiya ya afrika mashariki, uwekezaji na soko la ushindani
we unataka watu wafe, kuna Chuo kama Mzumbe unaujua mziki wake? kupita one semester kwenda nyingine ni ngumu kuliko mafunzo ya Jeshi, hlf waongeze na ugumu zaidi kwenye udahili? kha
 
Kimsingi Rais hajaifuta TCU,alichosema TCU ibaki na majukumu ya Regulation kwa Elimu ya juu na kuacha swala la Udahili wa pamoja (CAS)
Kwa maagizo hayo system ya Central admission wenda ikafutwa badae na kila mwanafunzi aombe udahili direct chuo husika anachokipenda.

Rejea nukuu hizi;
Mmbea wa jiji:
'Wanafunzi wanalazimishwa kupelekwa kwenye kachuo ambako hakana hata jina'- JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

'Niombe Wizara ya elimu, TCU tubadilishe utaratibu wa kuchagua wanafunzi, wanafunzi wenyewe wachague badala ya TCU'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

'Wakati mwingine wakuu wa vyuo wanaenda TCU kuomba wapangiwe wanafunzi pamoja na kwamba sina ushahidi'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

Rais Magufuli: Ishu si kuwa na vyuo vikuu vingi, ishu ni kuwa na vyuo vichache vinavyotoa wanafunzi wengi wenye vigezo vya juu [HASHTAG]#JFLeo[/HASHTAG]

'Wanafunzi wachague vyuo wanavyovitaka ambavyo havitachaguliwa vife, kwa nini mnalazimisha'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

'Kuna vyuo ambavyo haviko kwenye Standard vina hakikisha vinapata wanafunzi kwa sababu wanapata mkopo'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

Sasa tcu si inabalance yeye mwenyewe kaisifia UDSM sasa si kila mtanzania atataka kwenda UD vyuo vingine wakasome ngedere?
 
Hili ni moja kati ya maswali ya msingi sana. Na nashangaa inakuwaje watu walioko vyuoni hawaelewi umuhimu wa hili na kwamba TCU hawafanyi enrolment?
Hii system yakuomba chuon direct weng watatumia Ela kupata nafas na pia uwezekano wakuchaguliwa vyuo vyote ulivyoomba
 
Bora ifutwe tu,yaani watu wazima wanapangiwa wakasome nini na wapi?
My dear ulikuwa unachagua mwenyewe COURSES 3 na University 3! Hapo inakuwa lazima upate mojawapo ktk machaguo yako!
 
Kuna jambo ambalo wengi hatulielewi. TCU hawampangii mtu course (hili si kweli), TCU wanakupangia kutokana na ulichoomba. Shida iliyopo ni competition kubwa.

Unapoomba kozi flani pamoja na watu wengine 1000 wakati capacity ya chuo ni 70 hutapata. TCU kwa kutambua ndoto ya wengi ni kusoma chuo, wanaangalia wapi demand ilikuwa ndogo na qualification zako zimetimia wanakupangia. Its a matter of stay (wakuache) au go for your dream (walau utimize ndoto ya kusoma chuo).

Mpango unaopendekezwa una athari nyingi ambazo watu hawazioni. Ntaanisha chache;

1. Direct application kwenda chuo itaongeza gharama maradufu kwa maana kila chuo utalazimika kulipa application fees, gharama za stationeries etc.

2. Mfumo huu utapelekea watu wengi kukosa fursa ya kusoma elimu ya juu. Mathalani wote wakaomba UDSM, ARU, SUA na UDOM, kitakachotokea mwenye highest qualifications aweza kupata admission vyuo vyote akaziba nafasi za wengine.

Pili kwa kuwa application hufanyika baada ya matokeo ya F6 na muda mdogo kabla ya kufungua chuo, ni wazi atakaekosa vyuo labda vitatu ulivyoomba utachelewa kujua wapi kuna nafasi ukaombe hivyo mwaka huo kukupita na kukuacha mtaani.

3. Mfumo unaopendekezwa utawaacha watoto wa masikini wengi nje ( mfumo huu unaruhusu kupachikana kirahisi kwani kila mtu awe za kuja na majina ya nduguze chuoni kwake). Sambamba na hili la kupachikana kuna tatizo jingine la fedha, ni kweli kwamba bodi ya mikopo eitha haipeleki au huchelewesha kulipa ada za wenye mikopo, kutatua hili vyuo vinaweza kuopt kuchagua wanaojiweza kiuchumi wengi na kuwatupa nje watoto wa walalahoi wengi.

4. Tutatengeneza tatizo kubwa mbeleni la typology ya wanafunzi. Pamoja na TCU kuwa na matatizo wamejitahidi sana kubalance sana diversity ya wanafunzi vyuoni. Athari za direct entry zinaweza kuleta ukabila, chuo flani kimejaza nshomile wengi au wachaga wengi n.k (hii sio tuhuma mpya). Kuna jingine la udini, mathalani SAUT na associates wake wanaweza kujaza wakatoliki chuoni au MUM wakajaza radical islamist watupu na vyuo vingine n.k

5. Quality assurance itakuwa ngumu sana. Nilitegemea TCU waongezewe nguvu ya kuamua kuhusu ubora ikiwa ni pamoja na kupewa mamlaka ya kuamua entry qualification ili kulinda ubora wa vyuo vyetu. Tunarudi kule kule kwenye kila chuo kujiamulia sifa zake, vyuo vidogo na visivyo fahamika vitalazimika kushusha entry qualifications ili kufetch wanafunzi waliobaki (wenye sifa dhaifu) ili kuendelea kuwapo.

Rais ashauliwe vema kuhusu sera au kauli zake kuhusu elimu. Mara zote anapokuwa Mlimani ameonesha waziwazi kupendelea chuo hicho na kuviacha vyuo vingine kama vile si vya serikali au havina umuhimu. Leo inataka kuanzishwa sera ya ajabu ili kuipa UDSM autonomous ya kujiamulia mambo yenyewe, si sera mbaya ila vipi kuhusu vyuo vingine?

Hostels UDSM, Mabasi UDSM vipi wengine hawahitaji mambo hayo? Kwa nini tusiwe na treatment moja kwenye taasisi za elimu ya juu zote?
Hoja ya tano(5) mkuu nakujibu moja kwa moja kuhusu university entry qualifications
form six . D mbili (point nne)
Equivalent qualifications (diploma) ni 3.5GPA
Hivyo Ata kama itaamuliwa kupeleka vyeti kwenye vyuo husika, vyuo vitawekewa hili kama sharti na mamma husika.
 
Hivyo Ata kama itaamuliwa kupeleka vyeti kwenye vyuo husika, vyuo vitawekewa hili kama sharti na mamlaka husika.
 
Wajisahihishe. Maana anayosema Rais ni kweli tupu. Na ndiyo maana hata watumishi wake wana ukwasi wa kutosha kabisa. Mkurungenzi wa habari tu kajaza magari makubwa na maghorofa huko Goba. Rushwa rushwa rushwa nchi hii too much. Namuunga mkono Rais.
yani ukija uku heslb utalia sitosahau mwaka 2013 boss wa pale alijiandikisha majina hewa ya wanafunzi takribani 12000 sahivi anakula mema ya nchi na kwa sekeske la magu yupo marekani anakula bata...
 
Sasa tcu si inabalance yeye mwenyewe kaisifia UDSM sasa si kila mtanzania atataka kwenda UD vyuo vingine wakasome ngedere?
Hata wote wakiomba UDSM-chuo kikisha jaza nafasi ilizokuwa nazo waliobaki si watatemwa tu. Tungekuwa na takwimu za University enrollment ndio tungejuwa umuhimu wa vyuo vingine hasa vile ambavyo sio vya serikali.
Alichosema Raisi kinaweza kuwapa faraja wazazi na vijana lakini kiuhalisia hakitaleta tofauti yeyote labda ajenge miundo mbinu ya ziada vyuo vya serikali, aongeze fadha za kuendeshea hivyo vyuo, na waajiri walimu wa ziada kulingana na upanuzi huo wa elimu vinginevyo tutaendelea na mazoea yetu.
 
Back
Top Bottom