Nini hatma ya TCU baada ya kauli ya Rais Magufuli?

Lakini kwa muhimbili ni mwisho wa chuo,sup huku zinaogopeka sana hasa kwa 1st na 2nd yr
vipo vyuo pendwa ambavyo vina jali ada yako na si kkuingiza kwenye ma tuition centre tena mfano KIU,IMTU,KAIRUKI,ST JOSEPH na tcu wanavipenda sana hivi vyuo...
 
Kuna jambo ambalo wengi hatulielewi. TCU hawampangii mtu course (hili si kweli), TCU wanakupangia kutokana na ulichoomba. Shida iliyopo ni competition kubwa.

Unapoomba kozi flani pamoja na watu wengine 1000 wakati capacity ya chuo ni 70 hutapata. TCU kwa kutambua ndoto ya wengi ni kusoma chuo, wanaangalia wapi demand ilikuwa ndogo na qualification zako zimetimia wanakupangia. Its a matter of stay (wakuache) au go for your dream (walau utimize ndoto ya kusoma chuo).

Mpango unaopendekezwa una athari nyingi ambazo watu hawazioni. Ntaanisha chache;

1. Direct application kwenda chuo itaongeza gharama maradufu kwa maana kila chuo utalazimika kulipa application fees, gharama za stationeries etc.

2. Mfumo huu utapelekea watu wengi kukosa fursa ya kusoma elimu ya juu. Mathalani wote wakaomba UDSM, ARU, SUA na UDOM, kitakachotokea mwenye highest qualifications aweza kupata admission vyuo vyote akaziba nafasi za wengine.

Pili kwa kuwa application hufanyika baada ya matokeo ya F6 na muda mdogo kabla ya kufungua chuo, ni wazi atakaekosa vyuo labda vitatu ulivyoomba utachelewa kujua wapi kuna nafasi ukaombe hivyo mwaka huo kukupita na kukuacha mtaani.

3. Mfumo unaopendekezwa utawaacha watoto wa masikini wengi nje ( mfumo huu unaruhusu kupachikana kirahisi kwani kila mtu awe za kuja na majina ya nduguze chuoni kwake). Sambamba na hili la kupachikana kuna tatizo jingine la fedha, ni kweli kwamba bodi ya mikopo eitha haipeleki au huchelewesha kulipa ada za wenye mikopo, kutatua hili vyuo vinaweza kuopt kuchagua wanaojiweza kiuchumi wengi na kuwatupa nje watoto wa walalahoi wengi.


4. Tutatengeneza tatizo kubwa mbeleni la typology ya wanafunzi. Pamoja na TCU kuwa na matatizo wamejitahidi sana kubalance sana diversity ya wanafunzi vyuoni. Athari za direct entry zinaweza kuleta ukabila, chuo flani kimejaza nshomile wengi au wachaga wengi n.k (hii sio tuhuma mpya). Kuna jingine la udini, mathalani SAUT na associates wake wanaweza kujaza wakatoliki chuoni au MUM wakajaza radical islamist watupu na vyuo vingine n.k

5. Quality assurance itakuwa ngumu sana. Nilitegemea TCU waongezewe nguvu ya kuamua kuhusu ubora ikiwa ni pamoja na kupewa mamlaka ya kuamua entry qualification ili kulinda ubora wa vyuo vyetu. Tunarudi kule kule kwenye kila chuo kujiamulia sifa zake, vyuo vidogo na visivyo fahamika vitalazimika kushusha entry qualifications ili kufetch wanafunzi waliobaki (wenye sifa dhaifu) ili kuendelea kuwapo.

Rais ashauliwe vema kuhusu sera au kauli zake kuhusu elimu. Mara zote anapokuwa Mlimani ameonesha waziwazi kupendelea chuo hicho na kuviacha vyuo vingine kama vile si vya serikali au havina umuhimu. Leo inataka kuanzishwa sera ya ajabu ili kuipa UDSM autonomous ya kujiamulia mambo yenyewe, si sera mbaya ila vipi kuhusu vyuo vingine?

Hostels UDSM, Mabasi UDSM vipi wengine hawahitaji mambo hayo? Kwa nini tusiwe na treatment moja kwenye taasisi za elimu ya juu zote?
Umeelezea kitu cha msingi sana kama serikali ikifuata angalau hiki kidogo ulichokiandika na kuacha ushaabiki itasaidia sana shida tulio nayo kizazi cha sasa hivi hatupendi kushughulisha vichwa mpaka yatokee ya kutokea ndiyo tusituke nadhani umeeleweka kwa wanaotaka kuelewa
 
Watu wanao unga mkono kauli ya Rais juu TCU siyo wataalamu wa elimu juu ya mfumo unaotumiwa vigezo ndo vinaelekeza watu kuchaguliwa vyuo husika ,na TCU hailazimishi mtu leo hii suala la mtu kuchaguliwa vyuo zaidi ya viwili limeisha sasa anataka kuturudisha tulikotoka , kauli nyingine hazifai
pole sana hazifah wakat wenzako wanafuata maelekezo...
 
Rais ashauriwe vizuri utaratibu wa kuomba chuo directly una mapungufu mengi

Central admission system imehakikisha wanafunzi wenye sifa za kusoma kozi flani ndio wanasoma
kwan mkuu ze hebby ukifanya direct admission utapelekwa kozi usiyohitaj nothing at all ....
 
Central admision system isifutwe bal ifanyiwe marekebisho tu.

Tukiiondoa bas wanafunzi wengi watakosa chuo na procedure itakuwa ndefu bcz kuna ambao watapata chuo zaid ya kimoja huku wengine wakikosa.

Rais umekosea.
bloodful kabisa kusema rais umekosea
 
Yaani TCU na Nacte, wafutilie mbali.....ningefurahi sana...kuna mambo ya ajabu sana kule...
teyali washafanya utekelezaji mkuu bravo ruksa direct chuoni... tena chuo unachohitaj kwani haiwezekani wew mtu upo mwanza na uletwe mtwara edu wakat huohuo st agust ipo karibu na nyumbani...
 
Sasa watakua wanapeleka ombi moja kwa chuo kimoja au maombi kwa vyuo vinne kama zamani? Na vipi ukitemwa endapo unanafasi moja ya kuomba chuo au vipi ukichaguliwa vyuo vyote vinne? Na pia matokeo ya udahili yatakua yanatofutiana muda wa kuwa published kwa kila chuo ili kutoa nafasi ya mwanafunzi kujaribu kuomba nafasi chuo kingine endapo atakosa nafasi chuo fulani?
 
Kwahyo kwa mtazamo huo cutting point zitakuwa hazihusiki? Lakini pia tusikimbie ukweli kuwa wanafunzi wote wanakuwa na ndoto ya kusoma vyuo vikubwa tu ambavyo ni udsm,udom, ifm na mzumbe ambapo hata tukichambua zaidi havizidi vitano.
 
Kimsingi Rais hajaifuta TCU,alichosema TCU ibaki na majukumu ya Regulation kwa Elimu ya juu na kuacha swala la Udahili wa pamoja (CAS)
Kwa maagizo hayo system ya Central admission wenda ikafutwa badae na kila mwanafunzi aombe udahili direct chuo husika anachokipenda.

Rejea nukuu hizi;
Mmbea wa jiji:
'Wanafunzi wanalazimishwa kupelekwa kwenye kachuo ambako hakana hata jina'- JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

'Niombe Wizara ya elimu, TCU tubadilishe utaratibu wa kuchagua wanafunzi, wanafunzi wenyewe wachague badala ya TCU'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

'Wakati mwingine wakuu wa vyuo wanaenda TCU kuomba wapangiwe wanafunzi pamoja na kwamba sina ushahidi'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

Rais Magufuli: Ishu si kuwa na vyuo vikuu vingi, ishu ni kuwa na vyuo vichache vinavyotoa wanafunzi wengi wenye vigezo vya juu [HASHTAG]#JFLeo[/HASHTAG]

'Wanafunzi wachague vyuo wanavyovitaka ambavyo havitachaguliwa vife, kwa nini mnalazimisha'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]

'Kuna vyuo ambavyo haviko kwenye Standard vina hakikisha vinapata wanafunzi kwa sababu wanapata mkopo'-JPM [HASHTAG]#UzinduziHOSTELUDSM[/HASHTAG]
Kwa mara ya kwanza namuunga mkono juma pumba
 
Kwahyo kwa mtazamo huo cutting point zitakuwa hazihusiki? Lakini pia tusikimbie ukweli kuwa wanafunzi wote wanakuwa na ndoto ya kusoma vyuo vikubwa tu ambavyo ni udsm,udom, ifm na mzumbe ambapo hata tukichambua zaidi havizidi vitano.
ifm sio chuo kikubwa mkuu
 
ifm sio chuo kikubwa mkuu

Ni chuo kidogo au sio? Hivi ushawai jiuliza kuwa vyuo pendwa in town ni vipi obviously huwezi acha kukitaja ifm hasa kwa wale kwenye michepuo ya biashara mfano mkubwa ni mimi mwenyewe nilipomaliza advance nilipomaliza my first choice ilikiwa ifm
 
Ni chuo kidogo au sio? Hivi ushawai jiuliza kuwa vyuo pendwa in town ni vipi obviously huwezi acha kukitaja ifm hasa kwa wale kwenye michepuo ya biashara mfano mkubwa ni mimi mwenyewe nilipomaliza advance nilipomaliza my first choice ilikiwa ifm
Basi mkuu nshajua kwanini umekiweka hapo... just ni taasisi tu kile
 
kama ni siasa mbona nacte teyali wamekubali pigo ama....

Bahati mbaya huelewi mfumo wa elimu ya juu unavyofanya kazi. Vyuo vinavyosimamiwa na NACTE viko chini ya wizara ya elimu kwenye masuala ya kitaaluma na viko chini ya wizara mbalimbali na wamiliki binafsi kiutawala.

Vyuo vikuu ni independent kwa kila kitu kitaaluma na kiutawala.
 
naona kwa mbali kila chuo kitakua na cut off point kwa ajili ya udahili hapo chuoni so lazima chuo cha udsm kiwe na cut off point kubwa kujiunga ili na vyuo vingine navyo vipate wanafunzi...
Na huo ndio mwanzo wakufufuka kwa udsm ile tuliyoizoea, inawezekana pia migomo ikarudi upya hata kama haitakuwa na nguvu kama zamani. TCU walikuwa wanarundika manung'aembe kwenye chuo hiki na kuanza kukiua. Haya sasa wale wakupandisha ada hadi 10m tutawaona.

Vijana huko six kazeni buti ili mkakae kwenye magorofa ya magufuli. Bila one kali hugusi mlimani.
 
Nilichelewa mwaka kwa ajili ya tcu

Ila naona elimu inayumba, udahili wa kila ngazi ya elimu lazima uwe mastered na wizara yaan taarifa zote za mwanafunzi ziwe mastered na wizara hapo udahili wa elimu haitayumba
Hakuna cha wizara. Hata huko Ulaya na Marekani ni kila chuo na vigezo vyake.
 
Back
Top Bottom