Nini hatma ya TCU baada ya kauli ya Rais Magufuli?

Utaratibu wa kuomba kupitia CAS ulikuwa ni kukusanya elfu hamsini tu na kupotezeana malengo.

Mimi kwetu ni Moshi napenda kusoma MOCU kwasababu najua maisha hayatanishinda sasa TCU wananipangia SAUT nikaishije Mwanza
Haya yamekukuta au ni hali inayoweza kukupata (hypothetical scenario). Jibu langu kama hukuchagua SAUT Mwanza sioni watakupelekaje huko. Wewe Jaza MOCU hayo mengine achana nayo. Ufaulu wako utaamua.
 
na kila kozi itakuwa na ufaulu wake haiwezekani medicine uchukuliwe na point 4 na wakati huo law nayo iwe point hiyohyo tcu ife hashtag....
Mkuu kwa hili huitendei haki TCU. Point kutoka masomo mawili ni kwamba kama huna hizo pointi basi wewe degree hapa Tanzania (direct entry) sahau. Kuwa na pointi 4 kunakuruhusu kuomba degree lakini lazima uangalie chuo kinataka uwe na point ngapi ili uweze kufikiriwa. Na ukiwa na hizo pointi zinazotakiwa na chuo ndiyo unawekwa kwenye kapu la ushindani. Kama Chuo kinaushindani mdogo na nafasi nyingi unaweza kupenya na point 4 zako.
 
naona mwaka wa masomo 2017/2018 utakuja na version mpya kabisa duhh dili la 50,000 kwa kila kichwa linabak chuoni sasa...
Na kila chuo utakacho omba kinataka hela yake.
 
Haya yamekukuta au ni hali inayoweza kukupata (hypothetical scenario). Jibu langu kama hukuchagua SAUT Mwanza sioni watakupelekaje huko. Wewe Jaza MOCU hayo mengine achana nayo. Ufaulu wako utaamua.
Nataka niende MOCU nijichagulie nasoma nini kulingana na ufaulu wangu wao wapeleke Jina TCU kwisha kama tulivyofanya zamani
 
Kwa sasa ni MUM na Chuo Kimoja Zanzibar ndio wanaotumia style hiyo. Sijui kama MOCU watafuata njia hiyo na kukubaliwa.
 
Hapa naona mheshimishimiwa katereza.
  • Fikiria mwanafunzi anaomba chuo fulani kisha anakosa na muda ukawa ulishakwenda. Haoni kama mwanafunzi huyo atakosa nafaasi ya kusoma mwaka huo?
  • Fikiria mwanafunzi ameomba vyuo zaidi ya kimoja na akachaguliwa ktk vyuo vyote alivoomba, haoni kama atakua ameziba nafasi za wenzake na kuna uwezekano vyuo vikadahili wanafunzi hewa, means wanafunzi waliokwisha chaguliwa na vyuo vingine! hapa kuna vyuo vitadahili wanafunzi, ila muda wa kuripoti, wakajikuta hawaoni wanafunzi wa kuripoti, kumbe walidahii wanafunzi waliodahiliwa na vyuo vingine.
 
Kwa hili nakuunga mkono 100% rais wangu ni huamuz sahihi sana tna sana, tcu ilikuwa ya ajab sana et kisa baba sijui mjomba ni member wa board au nna mamlaka serkal et hupate chuo bora, sasa wasio kuwa na ndugu uko na wana sifa wap waende ,saf sana
 
Hapo umenena
 
Kuziba nafasi kwa Wakati huu haipo tena hiyo ni zamani wakati wa vyuo vitatu Siku hizi vimejaaa

Mtu achaguliwe apewe muda wa kuthibitisha kwamba nakuja hajathibitisha sio wenu huyo na kuwe na list ya Akiba.

Hii itasaidia hata vyuo vingine kushusha bei ili vivutie Wateja sio TEKU inakuwa na bei sawa na Mzumbe kisa wana uhakika wa wateja

Rais alieleza Vizuri kuna vyuo ukipewa cheti chake unageuza geuza lakini ukipewa cha UDSM wala hukagui waache watoto wachague UD kama vingine havishindani vinakufa vife
 
Sio lazima useme, waweza kukaa kimya maana unaonekana hujui CAS ilivyokuwa inafanya kazi na faida zake!
 
Mimi ni mpinzani pure na hua siungi mkono mambo mengi ya mkulu lkn kwa hili naomba nimuunge mkono yuko sahihi kabisa na nimefurahi kwa hilo
Subiri uanze huo mfumo wa maombi wa zaman ndo utajua kuwa haukosahihi kumuunga mkono rais!
Haya yamekukuta au ni hali inayoweza kukupata (hypothetical scenario). Jibu langu kama hukuchagua SAUT Mwanza sioni watakupelekaje huko. Wewe Jaza MOCU hayo mengine achana nayo. Ufaulu wako utaamua.
 
Kuna jambo ambalo wengi hatulielewi. TCU hawampangii mtu course (hili si kweli), TCU wanakupangia kutokana na ulichoomba. Shida iliyopo ni competition kubwa.

Unapoomba kozi flani pamoja na watu wengine 1000 wakati capacity ya chuo ni 70 hutapata. TCU kwa kutambua ndoto ya wengi ni kusoma chuo, wanaangalia wapi demand ilikuwa ndogo na qualification zako zimetimia wanakupangia. Its a matter of stay (wakuache) au go for your dream (walau utimize ndoto ya kusoma chuo).

Mpango unaopendekezwa una athari nyingi ambazo watu hawazioni. Ntaanisha chache;

1. Direct application kwenda chuo itaongeza gharama maradufu kwa maana kila chuo utalazimika kulipa application fees, gharama za stationeries etc.

2. Mfumo huu utapelekea watu wengi kukosa fursa ya kusoma elimu ya juu. Mathalani wote wakaomba UDSM, ARU, SUA na UDOM, kitakachotokea mwenye highest qualifications aweza kupata admission vyuo vyote akaziba nafasi za wengine.

Pili kwa kuwa application hufanyika baada ya matokeo ya F6 na muda mdogo kabla ya kufungua chuo, ni wazi atakaekosa vyuo labda vitatu ulivyoomba utachelewa kujua wapi kuna nafasi ukaombe hivyo mwaka huo kukupita na kukuacha mtaani.

3. Mfumo unaopendekezwa utawaacha watoto wa masikini wengi nje ( mfumo huu unaruhusu kupachikana kirahisi kwani kila mtu awe za kuja na majina ya nduguze chuoni kwake). Sambamba na hili la kupachikana kuna tatizo jingine la fedha, ni kweli kwamba bodi ya mikopo eitha haipeleki au huchelewesha kulipa ada za wenye mikopo, kutatua hili vyuo vinaweza kuopt kuchagua wanaojiweza kiuchumi wengi na kuwatupa nje watoto wa walalahoi wengi.

4. Tutatengeneza tatizo kubwa mbeleni la typology ya wanafunzi. Pamoja na TCU kuwa na matatizo wamejitahidi sana kubalance sana diversity ya wanafunzi vyuoni. Athari za direct entry zinaweza kuleta ukabila, chuo flani kimejaza nshomile wengi au wachaga wengi n.k (hii sio tuhuma mpya). Kuna jingine la udini, mathalani SAUT na associates wake wanaweza kujaza wakatoliki chuoni au MUM wakajaza radical islamist watupu na vyuo vingine n.k

5. Quality assurance itakuwa ngumu sana. Nilitegemea TCU waongezewe nguvu ya kuamua kuhusu ubora ikiwa ni pamoja na kupewa mamlaka ya kuamua entry qualification ili kulinda ubora wa vyuo vyetu. Tunarudi kule kule kwenye kila chuo kujiamulia sifa zake, vyuo vidogo na visivyo fahamika vitalazimika kushusha entry qualifications ili kufetch wanafunzi waliobaki (wenye sifa dhaifu) ili kuendelea kuwapo.

Rais ashauliwe vema kuhusu sera au kauli zake kuhusu elimu. Mara zote anapokuwa Mlimani ameonesha waziwazi kupendelea chuo hicho na kuviacha vyuo vingine kama vile si vya serikali au havina umuhimu. Leo inataka kuanzishwa sera ya ajabu ili kuipa UDSM autonomous ya kujiamulia mambo yenyewe, si sera mbaya ila vipi kuhusu vyuo vingine?

Hostels UDSM, Mabasi UDSM vipi wengine hawahitaji mambo hayo? Kwa nini tusiwe na treatment moja kwenye taasisi za elimu ya juu zote?
Binafsi nimekuelewa
 
Kuziba nafasi kwa Wakati huu haipo tena hiyo ni zamani wakati wa vyuo vitatu Siku hizi vimejaaa

Mtu achaguliwe apewe muda wa kuthibitisha kwamba nakuja hajathibitisha sio wenu huyo na kuwe na list ya Akiba.

Hii itasaidia hata vyuo vingine kushusha bei ili vivutie Wateja sio TEKU inakuwa na bei sawa na Mzumbe kisa wana uhakika wa wateja

Rais alieleza Vizuri kuna vyuo ukipewa cheti chake unageuza geuza lakini ukipewa cha UDSM wala hukagui waache watoto wachague UD kama vingine havishindani vinakufa vife
jaribu kuweka kijeduari cha muda hapa ili tuone:
  • mwezi wa matakeo ya form 6 kutoka.
  • tarehe ya kuanza kuomba vyuo na tarehe ya mwisho wa kuomba
  • mtu aliyekosa nafasi sehemu ktk chuo fulani, kama atapaa na muda wa kuomba sehemu nyingine.
vipi pia kuhusu mtu aliyechagulia chuo zaidi ya kimoja na akajiunga na kimoja tu, means vyuo vingine vilimchagua vitakua vimechagua mwanafunzi hewa, unadhani ni njia zipi zitatumika kuepuka baadhi ya vyuo kuchagua wanafunzi hewa?

ktk kujibu ujibu kwa kueleza jinsi mambo yatavyokua na kuonyesha kua hakuna litaloharibika
 
Kuna jambo ambalo wengi hatulielewi. TCU hawampangii mtu course (hili si kweli), TCU wanakupangia kutokana na ulichoomba. Shida iliyopo ni competition kubwa.

Unapoomba kozi flani pamoja na watu wengine 1000 wakati capacity ya chuo ni 70 hutapata. TCU kwa kutambua ndoto ya wengi ni kusoma chuo, wanaangalia wapi demand ilikuwa ndogo na qualification zako zimetimia wanakupangia. Its a matter of stay (wakuache) au go for your dream (walau utimize ndoto ya kusoma chuo).

Mpango unaopendekezwa una athari nyingi ambazo watu hawazioni. Ntaanisha chache;

1. Direct application kwenda chuo itaongeza gharama maradufu kwa maana kila chuo utalazimika kulipa application fees, gharama za stationeries etc.

2. Mfumo huu utapelekea watu wengi kukosa fursa ya kusoma elimu ya juu. Mathalani wote wakaomba UDSM, ARU, SUA na UDOM, kitakachotokea mwenye highest qualifications aweza kupata admission vyuo vyote akaziba nafasi za wengine.

Pili kwa kuwa application hufanyika baada ya matokeo ya F6 na muda mdogo kabla ya kufungua chuo, ni wazi atakaekosa vyuo labda vitatu ulivyoomba utachelewa kujua wapi kuna nafasi ukaombe hivyo mwaka huo kukupita na kukuacha mtaani.

3. Mfumo unaopendekezwa utawaacha watoto wa masikini wengi nje ( mfumo huu unaruhusu kupachikana kirahisi kwani kila mtu awe za kuja na majina ya nduguze chuoni kwake). Sambamba na hili la kupachikana kuna tatizo jingine la fedha, ni kweli kwamba bodi ya mikopo eitha haipeleki au huchelewesha kulipa ada za wenye mikopo, kutatua hili vyuo vinaweza kuopt kuchagua wanaojiweza kiuchumi wengi na kuwatupa nje watoto wa walalahoi wengi.

4. Tutatengeneza tatizo kubwa mbeleni la typology ya wanafunzi. Pamoja na TCU kuwa na matatizo wamejitahidi sana kubalance sana diversity ya wanafunzi vyuoni. Athari za direct entry zinaweza kuleta ukabila, chuo flani kimejaza nshomile wengi au wachaga wengi n.k (hii sio tuhuma mpya). Kuna jingine la udini, mathalani SAUT na associates wake wanaweza kujaza wakatoliki chuoni au MUM wakajaza radical islamist watupu na vyuo vingine n.k

5. Quality assurance itakuwa ngumu sana. Nilitegemea TCU waongezewe nguvu ya kuamua kuhusu ubora ikiwa ni pamoja na kupewa mamlaka ya kuamua entry qualification ili kulinda ubora wa vyuo vyetu. Tunarudi kule kule kwenye kila chuo kujiamulia sifa zake, vyuo vidogo na visivyo fahamika vitalazimika kushusha entry qualifications ili kufetch wanafunzi waliobaki (wenye sifa dhaifu) ili kuendelea kuwapo.

Rais ashauliwe vema kuhusu sera au kauli zake kuhusu elimu. Mara zote anapokuwa Mlimani ameonesha waziwazi kupendelea chuo hicho na kuviacha vyuo vingine kama vile si vya serikali au havina umuhimu. Leo inataka kuanzishwa sera ya ajabu ili kuipa UDSM autonomous ya kujiamulia mambo yenyewe, si sera mbaya ila vipi kuhusu vyuo vingine?

Hostels UDSM, Mabasi UDSM vipi wengine hawahitaji mambo hayo? Kwa nini tusiwe na treatment moja kwenye taasisi za elimu ya juu zote?
Mkuu nyie ndo great great greater thinker ambao nmewahi kuwasoma hapa jamii forum, kiukwel nlipta ukakasi juu ya ili tcu na mapungufu yao still bado wameonesha njia.....
Nakumbka huu mfumo ulianza nikiw njian kujiunga chuo kikuu, kwa ufahulu wangu nilishaambiwa sikustahil kusoma udsm, div one ya mwsho 2010 ulikuw ufahulu wa kawaida tcu ikapeleka wanafunz 5800, wakati tunaambiwa uwezo wa wakati huo (kwenye kutupokea mkandala alilalamika sana kuwa serikal kushrikiana na tcu wamepotez mwelekeo wa udsm kwa kuleta wanafunz wengi wasio na sifa) tukaitwa mpk majina mabaya km container la TCU, jambo ilo lilinipa hali sana, sikuona cha ajabu na nikatoka na green results pale pamoja na kuambiwa hatufai.....

Binafsi naona mfumo wa kuomba vyuon una changamoto nyingi sana kulinganisha na TCU
 
Sio lazima useme, waweza kukaa kimya maana unaonekana hujui CAS ilivyokuwa inafanya kazi na faida zake!
ww ndo hajui chochote kwan hii cas ilikuwa autonomous au, wapo watu waicontrol ambao ndo tcu,ww ilikuwa ukienda pale na hela mkononi watu faster wanakupa chuo, ww ndo hujui chochote bashite ww
 
Back
Top Bottom