Ningekuwa Kikwete ningekimbia Nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ningekuwa Kikwete ningekimbia Nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nguvumali, Oct 25, 2011.

 1. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #1
  Oct 25, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Haya yanayoendelea sasa katika duru za siasa hapa Tanzania bara ni aibu kwa utawala wake kama rais wa Jamhuri ya Tanzania. Rushwa imeshamiri, serikali haikusanyi kodi ipasavyo, kila mtumishi wa umma anakusanya kwa nguvu zake zote kila raslimali iliyopaswa kutumika kwa umma.

  Ukija kwenye nishati hasa umeme/stima utalia, kila siku ni takwimu za Megawati lakini hatujawahi kufurahia umeme mfululizo.
  Madini huko ndio aibu aibu na fedheha kubwa.

  Nimshauri Bwana Kikwete, mzaliwa wa Msoga, ikiwa anahisi nchi imemtumbukia nyongo asione haya kubwaga manyanga, kama hilo pia litamnyima usingizi, achimbe kama Balali kisha tutamtangaza kama walivyomtangaza Balali, na kwakua WaTanzania ni watu wanaoamini kila jambo kirahisi wataishia kusema Rest In Peace.

  Ni ushauri wangu, kama umeshindwa Kimbia mzee.
   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyo Kikwete amewekwa na wananchi sasa unapomshauri akimbie nchi sielewi unamaanisha nini. Unaweza kufanya vizuri kama utawashauri wananchi wasiichague tena CCM 2015.
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Oct 25, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Naogopa inchi ikificha 2015 TUTAKUA KABURINI MAANA nasikia hata humu ICU tulimo leo madaktari wanaweza kuzima mashine za oxgen.
  kufikia jana NBS bado walikua na takwimu za mfumuko wa uchi wa 16% hapo ni baada ya kuchakachua price indeces
  .
  Mbona Balali alipoona mambo yamemzidi nguvu akala chimbo kisha hakurudi tena, ni ushauri tu.
   
 4. k

  kiloni JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Na yale masanduku ya kura mlizochakachua na kujaza ni wananchi wapi hao?!!
   
 5. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  mi nimepata kaulaji ndani ya serikali ya muungano sioni kama kuna haja ya kumtaka huyu dakt akimbie,mh nimeonja utamu wa serikali na nikaona hakuna kama serikali ya jk maana kanafasi nilikokapata kanaruhusu kupata visenti vya kutosha tu kutoka kwa wawezeshaji,raia.
   
 6. O

  Omr JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nyie ndio mnaokimbia familia zenu mambo yakiwa magumu. Wewe ni mtoto wa kiume lazima uyakabili matatizo sio kuyakimbia. Kikwete ni Dume la mbegu na madume ya kweli hayatapi tapi hovyo.
   
 7. O

  Omr JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu unajitangaza kuwa wewe ni mwizi serikalini? Sasa kweli watanzania tumlaumu Rais kwasababu wewe sio muadilifu?
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  wafikiriao kwa masaburi utawajua tu thread zao....sasa huyu meya wa dsm alieleta hii mada hapa, anaweza kuongoza kikao cha waheshmiwa madiwani wa jiji kweli,namuomba kwa kuwa ameshauriwa vibaya na msaidizi wake awe anafikiri kabla hajapost au kama masaburi yanamuwasha apige simu no.1234 atapata huduma popote atakapokuwa.
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Huna tofauti na gazeti moja nimesoma jana linasema KAFURILA azikoromea nchi tajiri, sijui huyu mwandishi alikuwa anaota, lakini ndo taaluma yake iliishia hapo kufikiri kichwa cha kuandika. Hivi kweli Kafurila anaweza kuyakoromea mataifa tajiri. Nirudi kwako sasa hizo sababu ulizoandika hapo juu ndyo za kumkimbiza rais nchini?

  Inaonekana hauna hata takwimu, hebu fuatilia kesi zilizoko mahakamani kuhusiana na ufisadi, nenda TRA upewe takwimu za jinsi tanzania inavyokusanya kodi ukilinganisha na nchi n yingine, tayari megawatt 100 zimeshaingia grid ya taifa kama ulikuwa hujui nakupa taarifa. Jakaya mbona mtamkumbuka tu na chuki binafsi zenu hizo.

  Mmshukuru siku hizi mnalala milango wazi , hakuna ujambazi tena. Wale jamaa wameacha ujambazi sasa wanajifanya kuzama kwenye siasa. Huko nako watachemsha tu. JK komaa nao usichoke.
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ebwanae ulijuaje kuwa huyu jamaa ni masburi type? thehe thehe thehe. Unajua wee waache tu wasanii wao wale. Nilicheka sana siku nasikia sugu anachangia bungeni yaani badala ya aibu yake nikawa naona naona aibu mimi na tv yangu home. Hivi watu wa Mbeya walifikiria nini wakaona anawafaa?. kwa chuki zao utashangaa wanasema wanamsimamisha kugombea urais mwaka 2015. Wakifanya hivyo narudisha kadi yangu ya kura tume manake sasa tutakuwa tunataniana
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  usingizie watoto bwana, wale ni malaika. wanaozomea ni wendawazimu wenu wale mnaowalipa kufanyakazi hiyo. Siasa kwli noma yaani ukishindwa hoja unaanza zile za kitoto kitoto mara ohh wazomeeni, tutawashtaki kwa wananchi nani wewe unawashtaki kwa wananchi, mara hakuna kulala mpaka kieleweke, na usilale, Jakaya yupo kikazi zaidi siyo majungu.
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo unataka kuniambia Mama yetu Mshumbuzi alisababisha familia na watoto wakakimbiwa ndo akaolewa? Kumbe ndiyo maana jamaa anakuja na hoja ya Rais kukimbia nchi , anajua kuwa Dr. wa Karatu ana uzoefu huo. Hivi nikuulize pale ikulu angeingia Bunduki nani angekuwa first lady Phina au NUSU?
   
 13. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #13
  Oct 25, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hatari sana, mwambieni kama maji ya shingo aende zake kule Omani kisha apige simu kuwa mambo yamemshinda , anaetaka kuongoza jahazi hili aliongoze.
  afanye kama Nahonda wa Meli iliyozama kule Visiwani.
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kapata asilimia 61 kwa nini asikimbie yule Dr Balaa aliyepata asilimia 46. sijapata kuona mshindi ndiye anakimbia
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Haikubaliki rais akimbie nchi yake hatujafika huko unakotaka kutupeleka hata wewe unaweza kuikimbia nchi kama unaona utawala wake haupendi utaitwa mkimbizi kutoka Tanzania
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Robert Mugabe bado ni mtawala ndio ikawa Kikwete haaaaaaaaaaa kama hukupiga kura waachie wale waliomchagua wewe subiri ushindi wa kura yako ya hapana ifikapo 2015. Mawazo hayo mgando utatukuta wenzako tunahangaikia masomo ya watoto wewe unagombana na kivuli cha kikwete hadi 2015. unatupotezea muda
   
 17. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sio ushauri stahiki mkuuu Nguvumali, why should he (Mr President) run away, uliyoyazungumzia kuwa ni matatizo ni mambo madogo besides ni part and parcel ya political life. Hakuna kukimbia bana mpaka 2015 ashuhudie uchaguzi mwingine na labda chama la mafisadi liangushwe kupitia sanduku la kura though pia sidhani maana dhana ya mabadiliko haijawafikia vilivo wananchi (majority) vjjini huko! Upinzani labda wataongeza viti vya ubunge tu which will also be good!
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  unaikumbuka ile hadithi ya kale ya fisi anayesubiri mfupa umdondoshe yule mnyama mwingine nimemsahau jina lake lakini linafanana na jina lako kwa helufi ya mwanzo
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kama kijiji kizima kingesema mama yangu mzazi ni mchawi ningekubali lakini kama ningeambiwa nimuue kwa sababu ya uchawi wake ningekataa ni nukuu ya Mwalimu Nyerere wakati anapinga kuundwa kwa taifa la Tanganyika au kuua Muungano badala ya kutatua kero zake.
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Oct 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,898
  Trophy Points: 280
  Ni wananchi tu peke yao ndiyo wanaweza kumkimbiza.Yeye mwenyewe hawezi kimbia,akimbie vila na kila anayemzunguka anampa heshima na kumfagilia huku ulinzi kibao.

  Mtakuwa mnaota mkongoja eti akimbie,nyie kama mambo ni magumu na life tight,basi yeye si hivyo.

  He is in another world.

  Mkuu kwa kifupi madaraka yanaweza kubadilika na kuwa kilevi kibaya sana.
   
Loading...