Mwanajamii
JF-Expert Member
- Mar 5, 2008
- 7,063
- 68
kuomba kikwete akimbie hasa kama tatizo ni la kimfumo haitasaidia badala yake hata akija Rais mwingine naye tutaomba akimbie ni bora tukaanza kufumua mfumo kwa kuanzia na katiba
Huyo Kikwete amewekwa na wananchi sasa unapomshauri akimbie nchi sielewi unamaanisha nini. Unaweza kufanya vizuri kama utawashauri wananchi wasiichague tena CCM 2015.
mKWEREE sasa hivi analaumu kila mtu kuwa anamkwamisha katika utendaji wake, anawalaumu wapinzani kuwa wanamkwamisha, analaumu kina Mzee Sita , analaumu waandishi .....Sio ushauri stahiki mkuuu Nguvumali, why should he (Mr President) run away, uliyoyazungumzia kuwa ni matatizo ni mambo madogo besides ni part and parcel ya political life. Hakuna kukimbia bana mpaka 2015 ashuhudie uchaguzi mwingine na labda chama la mafisadi liangushwe kupitia sanduku la kura though pia sidhani maana dhana ya mabadiliko haijawafikia vilivo wananchi (majority) vjjini huko! Upinzani labda wataongeza viti vya ubunge tu which will also be good!
Hakuna haja ya kukimbia kinchompasa ni kufukuza watendaji wote wanaomfanya wananchi wamchukie,anatakiwa awe mkali kama Rais na baba wa nchi aache ushkaji achape kazi kwa weledi zaidi.
Hawezi kwenda mwenyewe bana.Toka lini?Atavuta muda tu hadi hapo atakapopokeza kijiti kwa mwenzake.mKWEREE sasa hivi analaumu kila mtu kuwa anamkwamisha katika utendaji wake, anawalaumu wapinzani kuwa wanamkwamisha, analaumu kina Mzee Sita , analaumu waandishi .....
kama kashindwa anaweza kwenda hata msoga atuache tuendeleze Gurudumu la maendeleo
Mkuu ni wananchi peke yake wanaoweza kumwondoa bila hata ya huo muda kupita.Hii ndoto yako ingeipeleka kwanza kwa mganga wa kienyeji ili ujue kama ni maluweluwe, jinamizi au umeanza kupotelewa na kumbukumbu kwamba kikwete alishaapishwa hakuna kurudi nyuma hadi dr silaha kaacha kusema hamtambui kikwete
Huna tofauti na gazeti moja nimesoma jana linasema KAFURILA azikoromea nchi tajiri, sijui huyu mwandishi alikuwa anaota, lakini ndo taaluma yake iliishia hapo kufikiri kichwa cha kuandika. Hivi kweli Kafurila anaweza kuyakoromea mataifa tajiri. Nirudi kwako sasa hizo sababu ulizoandika hapo juu ndyo za kumkimbiza rais nchini?
Inaonekana hauna hata takwimu, hebu fuatilia kesi zilizoko mahakamani kuhusiana na ufisadi, nenda TRA upewe takwimu za jinsi tanzania inavyokusanya kodi ukilinganisha na nchi n yingine, tayari megawatt 100 zimeshaingia grid ya taifa kama ulikuwa hujui nakupa taarifa. Jakaya mbona mtamkumbuka tu na chuki binafsi zenu hizo.
Mmshukuru siku hizi mnalala milango wazi , hakuna ujambazi tena. Wale jamaa wameacha ujambazi sasa wanajifanya kuzama kwenye siasa. Huko nako watachemsha tu. JK komaa nao usichoke.
usingizie watoto bwana, wale ni malaika. wanaozomea ni wendawazimu wenu wale mnaowalipa kufanyakazi hiyo. Siasa kwli noma yaani ukishindwa hoja unaanza zile za kitoto kitoto mara ohh wazomeeni, tutawashtaki kwa wananchi nani wewe unawashtaki kwa wananchi, mara hakuna kulala mpaka kieleweke, na usilale, Jakaya yupo kikazi zaidi siyo majungu.
wakati mwingine ni bora mara mia, ndio maana Balali alikimbia matatizo yalipomzidia , hahaaah katoweka na koba limejaa mahela kisha akatangazwa kafa, hahaaaah anaishi kwa amani huko Jersey akitumbua mahela yake.kukimbia matatizo sio mwisho wa matatizo.
Again,like i've said,sidhani kama atakubali.Anajua kama akikimbia basi ni kukiri hayo yote,sasa undhani akikimbia kwa namna hiyo msoga ndo pa kwenda?mwambieni jamaa akimbie, akifika popote atoe taarifa kuwa yoyote anaweza kujikaimisha madaraka , na kuwa rais.
Haya yanayoendelea sasa katika duru za siasa hapa Tanzania bara ni aibu kwa utawala wake kama rais wa Jamhuri ya Tanzania. Rushwa imeshamiri, serikali haikusanyi kodi ipasavyo, kila mtumishi wa umma anakusanya kwa nguvu zake zote kila raslimali iliyopaswa kutumika kwa umma.
Ukija kwenye nishati hasa umeme/stima utalia, kila siku ni takwimu za Megawati lakini hatujawahi kufurahia umeme mfululizo.
Madini huko ndio aibu aibu na fedheha kubwa.
Nimshauri Bwana Kikwete, mzaliwa wa Msoga, ikiwa anahisi nchi imemtumbukia nyongo asione haya kubwaga manyanga, kama hilo pia litamnyima usingizi, achimbe kama Balali kisha tutamtangaza kama walivyomtangaza Balali, na kwakua WaTanzania ni watu wanaoamini kila jambo kirahisi wataishia kusema Rest In Peace.
Ni ushauri wangu, kama umeshindwa Kimbia mzee.
Huyo Kikwete amewekwa na wananchi sasa unapomshauri akimbie nchi sielewi unamaanisha nini. Unaweza kufanya vizuri kama utawashauri wananchi wasiichague tena CCM 2015.