Wanasema bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi
Sina maana kuwa maumivu ya baba yako na mama yako yanaweza ku9wa yako
Watu huwa tunajifunza kutokana na makosa na kutokana na kile kilichotokea. Umeshaona may be mara kwa mara ugomvi wa baba na mama yako na unajua kabisa na kwa kipimo chako wewe kama mtu mzima ushajua tatizo liko wapi na nani msababishi wa hayo
Sidha,ni kama hujajifunza kitu katika muda wote huo ambao wewe na dada yako mnasema mmezoea maugomvi ya baba yenu na mama na kisa chake na nini suluhisho lake
Pima mwenyewe maji kwa kina cha miguu yako na ujue unatarajia nini maishani mwako
Kujikatia tamaa kuwa kutokana na hili na hili mimi sitaoa si jambo la busara wala jema
Unaona mke wako wako wewe na kamwe hawezi kufanana kitabia na mzazi wako yoyote ni mke wako una uwezo wa kumshape na kumtengeneza na kutengeneza ffamilia yako namna unavyotaka
hatuishi kwa kuwa fulani aliishi hivi na mimi maisha yangu yatakuwa kama ya kwake ila tunaishi kwa kuwa una uwezo wa kujitengenezea namna ya kuishi na kupanga maisha yako yaweje
Uamuzi kuwa sitaoa kwa kuwa mama na baba wana maisha haya ni uamuzi wa ajabu sana ambao haupaswi kusemwa na mtu ambaye anajitambua na ana uwezo wa kujitengenezea maisha yake mwenyewe
Kwa nini wewe usioe na ukaprove wrong kwa baba yako kuwa ndoa ni mateso
Kwa nini usiwe mfano kwa maisha mazuri na ya mfano ukamwonyesha baba na mama kuwa ndoa ni tamu na nzuri bila maugomvi