Ningejua nisingeoa maishani mwangu

Mkuu,

bila kuingilia uhuru wa baba yako kutoa maoni yake, na bila kupima uwezo wake wa kujenga hoja, naomba nikushauri kuwa ukishasikia maoni yake, tumia akili yako kuchambua, kupima na kufanya maamuzi. Wewe kwa mujibu wa maelezo yako, hujafikiri wala kupima, unakimbilia kufanya maamuzi yanayohusu maisha yako for the next 50 years kwa mtazamo wa baba yako wa miaka 40 iliyopita.

Japokuwa wanawake ni wale wale, lakini watu tofauti...si kweli kwamba utakayemuoa atakuwa na tabia mbaya au nzuri kama za mama yako ambazo zimemfanya baba ajute...au, si kweli kwamba mtakavyoendesha ndoa yenu ndivyo walivyoendesha wazazi wenu kwa miaka 40 iliyopita...na si kweli kwamba wewe uwezo wako wa kufikiri ni sawa sawa na wa baba yako...jitahidi utumie akili yako...usitumie ya baba yako kwa 100%
 
Kijana, kama huna mpango wa kuoa bora hata masuala ya kupata mtoto uachane nayo kabisa, maana hutoweza kumpatia malezi yanayostahili. Kauli ya baba yako usiifanye msingi wa kujengea maisha yako, wengi wetu tungefuatisha kauli za wazaza wetu tungefail vibaya sana, badala yake tunatumia mapumgufu tuliyoyaona kwenye ndoa za wazazi wetu kuboresha ndoa zetu. Sisi wanaume tumepewa jukumu la kuiongoza ndoa/familia kwa maana hiyo ndoa ikifail wanaume yatupasa tujiangalie japo kupo baadhi ya wanawake ni wakorofi na wababe, na wanaweza kulazimisha ya ndoa yakawa mbaya. Cha msingi ni kuamua anataka kuwa na ndoa ya aina gani na juhakikisha unakuwa na aina hiyo ya ndoa kwa kupata ushauri kwa waliofanikiwa kwenye ndoa, pamoja na kusoma vitabu vyenye miongozo mizuri ya ndoa.
 
..loneliness mbaya sana, kuzeeka pekeyo mbaya sana...bira liende tu kibishi, hatutagombana kila siku, zipo simu tutacheka, tutacheza, tutashikana mikono njiani, tutafarijiana kwa mengi..
faida ni nyingi kuliko hasara kwa hiyo bora kuwa na mtu..

umeona ehh..
 
Mmh hivi mbona mnaiongelea ndoa negatively mmeambiwa koseeni kujenga!! Aaagh mtuwache tunaoelekea kwenye ndoa!!
 
Mhh i hate loneliness kwa kweli..nikiwaza kuzeeka sina a family of my own,hapana aisee,tuzinguane tu ,family is so important,tatizo ni over expectations mtu unadhani unaoa malaika kumbe binadamu wa kawaida tu ka wewe...

Come this way tuliongelee hili kinagaubaga shem..!
 
I dont think that is what he meant both are my parents I have been with them almost all my life I do understand what he is going through sikutaka weka wazi everything coz kuna baadhi ya watu humu wanajua who I am.

Ungetumia ID nyingine ili ufafanue kwa kinagaubaga
 
usipende kuingilia yasiyokuhusu unauvumilivu? Nakuangalia tu ntakuibukia hapo usianze kulalamika ohoo!

utaishia kwenye ban tu bora uwe mpole, hunijui sikujui sioni connection yoyote yakutoana mishipa ya shingo for what reason?

hili jukwaa mwanzo halikuwa hivi lakini tangu kiwekwe kile kitufe cha share Facebook nashuhudia vituko vitupu tu.
 
Mimi ni kati ya wanaojuta kuoa kaka... hivyo mzee wako yuko sahihi , tafuta mtoto kisha songa mbele , utakuwa umeepuka vitu vingi sana kaka.
 
Mimi naona maisha ya ndoa ya wazazi wako yamekuadhiri kisaikolojia, unahitaji ushauri tu na kutiwa moyo.

Ni kweli kuna watu wanajuta kuoa/kuolewa na wenzi walionao kutokana na mifarakano ya hapa na pale na isiyoisha, ila watu hawaishi kuoa/kuolewa eti kwa vile kuna mifarakano kwenye ndoa fulani hata kama ni wazazi wako, wewe unapaswa kujifunza kutokana na makosa hayo na kudhamiria kutoyarudia makosa hayo kamwe katika ndoa yako, kumbuka wewe ni wewe, wao ni wao na sisi ni sisi.

Ukizaa bila kuishi na mwanamke utamuathiri sana mtoto kwani atapata malezi na makuzi ya ajabu sana na atakosa upendo wa wazazi wake wakiwa pamoja, na mwisho utakuja kujuta utapogundua mwanamke uliyezaa naye amaolewa na mtoto wako anateswa na baba wa kambo kiasi cha kunyimwa chakula. Usifanye hivyo ndugu yangu, wewe ni mtu mzima
(i hope so), jenga familia yako wewe mwenyewe, na usiige mtu hata kidogo maana ndoa hutengenezwa na wanandoa wenyewe kwa msaada wa Mungu.

Zaidi sana nakushauri mpokee Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako, utawaombea wazazi wako na wewe utaomba Mungu akupe mke mwema na wewe uwe mume mwema, barikiwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom