Ninauguliwa na baba watoto wangu

Ninauguliwa na baba watoto wangu

Status
Not open for further replies.
Dada yangu pole kwa kuuguliwa ... tuonane Pm ili nione nikusaidieje japo soda ya njiani.
Mkuu, kama kweli unamoyo na nia ya kumsaidia bimkubwa.... basi mpunguzie ugumu na ujipeleke huko PM kuliko yeye ndie akuanze mkuu.
Kumbuka mama anashida na pengine ningumu kwake kwenda huko PM kwa mawasiliano.
Pia amerahisisha kwa kuweka 0755 557094 kwaajili ya kusaidiwa/mawasiliano
 
@Mandenyi pole sana. Ukweli una moyo wa ajabu sana wa upendo. Yaani umetelekezwa for 17 years na bado una huruma na huyo mtesaji? Ni kipaji cha pekee sana kusamehe na kuachilia mambo ili baraka zikufuate. Kikubwa kuweza kuweka ombi lako hapa ili tukuunge mkono.
 
Mara ya mwisho kwenda Mbeya ilikua 45000. Sina hakika kama imeongezeka au imeshuka.
Ahsante mi nilijua ni kama 70 hivi sasa kumbe ni hela ya kujitolea tu kawaida.
Kulikua hakuna haja ya baadhi ya watu kukejeli, ikiwa mtu hana nia ya kutoa kitu asiwe na maneno ovyo.
Naamini kama kuna demu angekuja na bango la kutaka atolewe out mijanaume tungejaa hapa kuomba nafasi wakati vyuma vimekaza...ila hilo lisingeonekana.
Kuna siku niliweka bango la kumblock dem kwa kuniomba 70 ya kuongezea apate sim nyingine...nikampiga na chini.
Sio kwamba nilikua sina hapana.
Nilisema ikitokea mtu yuko shida iliyo serious humu na nikapata ushahidi wa hilo basi hata laki namchangia.
 
@Mandenyi pole sana. Ukweli una moyo wa ajabu sana wa upendo. Yaani umetelekezwa for 17 years na bado una huruma na huyo mtesaji? Ni kipaji cha pekee sana kusamehe na kuachilia mambo ili baraka zikufuate. Kikubwa kuweza kuweka ombi lako hapa ili tukuunge mkono.
Na katika hili kwa kweli amechagua fungu jema. You can imagine mtu mmehangaika miaka wee afu siku ya siku unaishia kuondoka na watoto wako wanne bila chochote na hujui hata unaanzia wapi. But ona Mungu alivyo mwaminifu kwake, kama Daudi alivyosema "Sijawahi ona mwenye haki ameachwa", na ndicho ambacho Mungu anazidi kumfanyia.

Kuna wakati kusamehe ni kugumu sana jamani; ila uchungu, majeraha na vinyongo vyetu juu ya watu vingine, vinatuangamiza sisi wenyewe zaidi. Yani hakuna mtu anayebarikiwa kwa kubeba watu wengine mioyoni mwake, lakini tunamshukuru Mungu kwa neema yake, tunajifunza kusamehe na kumuachia yote. Trust me hakuna kitu kinaumiza kama kutokufanya amani na mtu, afu huyo mtu akafariki kabla hamjapatana. I had a similar case, my uncle na mkewe, na yeye alimtenda mkewe sana, ila kwa ule uchungu mwanamke na yeye aliishia kuyaharibu sana maisha yake maskini. Unfortunately uncle alifariki kabla hawajapatana, aunt yangu inamuumiza mpaka kesho. So wakati mwingine inatubidi tusamehe tena hata kabla ya kuombwa msamaha, sio kwa sababu tumejisikia au ni rahisi sana au tumeombwa msamaha; ila ni kwa sababu ya amani yetu ya moyo kwanza, na hivyo kufungua zaidi milango yetu ya baraka.
Mama angu Mamndenyi, huyu Mungu na azidi kukutetea.
 
Salaam sana wana MMU wote;

Nimekuja kwenu rasmi kuleta taarifa hii ya kuuguliwa na bwana ambaye nimezaa naye watoto wangu wote wanne.

Kweli tulifikia mahali kimaisha tukatengana tokea 2001. Kila mmoja akiwa na maisha yake huku nikiwa na changamoto kubwa na kali za kulea watoto ambao ilibidi nibaki nao, hayo kwa sasa tuyaweke pembeni.

Hadi ninavyoandika huu uzi hakuna mtoto hata mmoja ambaye ameshapata kibarua wote wapo kwenye kuhangaika kutafuta kazi.

Ilipofikia mwaka jana mwishoni nikapata taarifa ya kuwa yule bwana niliezaa naye anaumwa, nikajuwa ni homa za kawaida tu.

Leo kaka yake ndo ananipigia simu na kusema kuwa mdogo wake amezidiwa sana na alikuwa amezimia ila kazinduka tena juzi.

Kwangu hiki kitu ni kikubwa nimeshindwa kukibeba.

Kwenu wana jamii kwa upendo wenu ninaomba mnichangie nauli ili niweze kwenda huko Mbeya kumwona huyo mgonjwa. Kama mnavyojua mahali penye ugonjwa mkubwa pia panahitajika hela ya matumizi mengineyo.

Kwa wana jamii wa Mbeya mnaweza kwenda kumuuona nyumbani ni Sae.

Naomba tu msinitukane maana nitalia;
POLE Mamdenyi, usiende huko Mbeya na hela nyingi maana mgonjwa hatapona kama ni muhimu sana uza vi kuku vyako au ka kirikuu upeleke kwa mgonjwa.
 
Salaam sana wana MMU wote;

Nimekuja kwenu rasmi kuleta taarifa hii ya kuuguliwa na bwana ambaye nimezaa naye watoto wangu wote wanne.

Kweli tulifikia mahali kimaisha tukatengana tokea 2001. Kila mmoja akiwa na maisha yake huku nikiwa na changamoto kubwa na kali za kulea watoto ambao ilibidi nibaki nao, hayo kwa sasa tuyaweke pembeni.

Hadi ninavyoandika huu uzi hakuna mtoto hata mmoja ambaye ameshapata kibarua wote wapo kwenye kuhangaika kutafuta kazi.

Ilipofikia mwaka jana mwishoni nikapata taarifa ya kuwa yule bwana niliezaa naye anaumwa, nikajuwa ni homa za kawaida tu.

Leo kaka yake ndo ananipigia simu na kusema kuwa mdogo wake amezidiwa sana na alikuwa amezimia ila kazinduka tena juzi.

Kwangu hiki kitu ni kikubwa nimeshindwa kukibeba.

Kwenu wana jamii kwa upendo wenu ninaomba mnichangie nauli ili niweze kwenda huko Mbeya kumwona huyo mgonjwa. Kama mnavyojua mahali penye ugonjwa mkubwa pia panahitajika hela ya matumizi mengineyo.

Kwa wana jamii wa Mbeya mnaweza kwenda kumuuona nyumbani ni Sae.

Naomba tu msinitukane maana nitalia;
Siamini kama ni wewe dadangu pole sana! Huo mchango tunatumaje?
 
Mama hebu kuwa na akili komavu. Kama huna pesa za kusafiri huhitaji kuchangiwa ukamuone ex tena usikute ameoa utakuta kebehi huko.

Kama anaongea mpigie simu umpe pole Na muombee Mungu ampende zaidi ili na wewe uolewe wenyewe wanasema 'oa single maza kama mumewe kafa'
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom