Ninauguliwa na baba watoto wangu

Status
Not open for further replies.
Mm sina hela lakni nikisema pole ni zaidi ya pesa makaratasi. Ngoja wachange nami nitakuchangia nauri ya kurudi. Pia nko mbeya nambie sehemu gan mgonjwa yupo maana matapel nao wapo kila kona
Amesema SAE karibu na kwa Sugu mbunge, ulizia kwa Siame!
 
Umeanza lini kumjua mleta mada au kupitia post hii!?...mbona huwa hamjaribu kufanya background cheki vitoto vya siku hizi!?..



ID ya Mamdenyi naifahamu.

Na mimi sio mtoto.Unapogeuka mganga wa kienyeji kupiga ramli ndio unapofeli!

Background check ya nini na anajulikana muomba misaada sio mara ya kwanza!Ni ombaomba kwa lugha rahisi kabisa!

Mtu mwenye tabia ya kuombaomba ni mtu mkwepa majukumu na he/she will never get any respect no matter the ID you have on JF!
 
Wewe ndio una akili?

Kugeuka ombaomba ndio akili!?

Waomba misaada wakubwa!
Mzee ambacho hakikufai kilie pin,hutakiwi kua na roho ya kwa nini,kwa nini unaumia binadamu mwezako akisaidiwa.imemtokea dharula tu hii .au alishakuomba ela yako.na wewe ukijiskia weka matatizo yako haujanyimwa ,dont loose yourself,au land lord anakusumbua anadai mkwanja nini?
 
Mkuu inaonekana we una matatizo kidogo ya kuto kuelewa nadhani unge mwelewa unge kaa kimya

Kukaa kimya ni busara pia

We umeeleweka kama ulivyo taka ueleweke sasa inapo fika wakati umeendelea kuzungumza vitu ambavyo wenzio hawakuelewi unaonekana una lako na mhusika

Mpinga wengi.......... Utajaza mwenyewe hapo
 
Oi wakuu siku zote mtu anapokuja mbele yenu kuomba msaada msikejeli na kudharau.

Kama una uwezo wa kusaidia basi fanya hivyo, kama huna uwezo basi hata maneno ya kufariji na sala inatosha. Lakini ukikejeli na kutukana na kudharau, kesho yako huijui ndugu.

Mungu huyu ni wetu wote, yaweza kuwa ni jaribu kwako, dhihaka hizo mnazofanya na kejeli kesho yaweza kuwa zamu yako na usipate msaada wowote hata wa maneno ya kufariji tu.

Tuchunge midomo yetu jamani na vidole gumba vyetu. Hata kama leo upo katika nafasi nzuri kimaisha huwezi kujua kesho yako, kuna wengi walikua matajiri leo hawana kitu, vipi kama walikua wanawadharau watu waliokua wanawazunguka? Wataishije?

Aheri kukaa kimya kuliko kukejeli. Hakuna anaeijua kesho yake.

"Tajiri mmoja alilima mazao na kisha kuvuna kwa wingi sana mpaka akakosa mahali pa kuhifadhi mazao yake, basi akajiambia kuwa atajenga ghala kubwa na kuhifadhi mazao yake humo kisaha yeye atakuwa mtu wa kula na kunywa tu maisha yake yote maana alikua na kila kitu, lakini Mungu akamwambia " mpumbavu wewe, naitaka roho yako usiku wa leo!"

Kumbe mambo unayopanga wewe sio final, Mungu nae anakuangalia, haifai kujiona fahari duniani kisa umefanikiwa kupata maisha mazuri wakati huwezi kusaidia wengine.

Hiyo story ya tajiri ipo kwenye bible ila sikumbuki ni injili ya nani! Hii ni kutokana na kuwa retired seminarian. Nakumbuka mafundisho yote ya neno la Mungu.
 
Acha uswahili mkuu....[emoji45] [emoji45] [emoji45]
Mbona skuhizi sote tunatambua kwamba popote unaweza hamisha fedha toka mtandao wowote na kwenda mtandao wowote.....[emoji16] [emoji16] [emoji16]
Acha mbwembwe comrade....
Hakia Mungu mkuu unafaa kuwa mpiga debe na abiria wote wanapanda gari lako.
 
Achana huyo mchawi, roho mbaya hiyo si ya nchi hii
Kanikera sana kumuita mtu ombaomba wakati si ajabu linamtegemea baba yake bado!..
Mtu hajaomba hela ya kula kila siku ni kwamba ameona hela inayohitajika ni kubwa kwa yeye kuipata haraka iweje amuite msanii na mnafiki kisa kaja kutushirikisha ishu ya mzazi mwenzie!!..
Hili dogo linaona watoto 4 kuzaa pamoja kitu kidogo!..
 

Mzigua90
 
Acha uswahili mkuu....[emoji45] [emoji45] [emoji45]
Mbona skuhizi sote tunatambua kwamba popote unaweza hamisha fedha toka mtandao wowote na kwenda mtandao wowote.....[emoji16] [emoji16] [emoji16]
Acha mbwembwe comrade....
Hakia Mungu mkuu unafaa kuwa mpiga debe na abiria wote wanapanda gari lako.
 
Na wasi wasi kama wewe ulishawahi kusaidia hata ndugu zako huko kijijini kwenu.
Em jaribu kuwa na kifua ikiwa hauwezi kumsaidia mtu usimtupie maneno ya ovyo:

Wewe hauna tofauti na mfanyakazi mwenzangu mmoja, siku moja tupo sehemu moja tumekaa sehemu, alikuja mbaba mmoja akawa anaomba jero tu ili akapate japo kitumbua...

Basi maneno aliyomjibu sikupendezwa nayo ilibidi niingilie kati, maana sipendi ujinga kama ule.
Nilimwambia pale pale ni afadhali mtu umwambie hauna kuliko kumjibu mbovu, kwamba "wewe vipi kazi zote hapa mjini unashindwa kupata hero" hujui mtu ana masahibu gani.

Sio uungwana hata kidogo, kitu kama hautaki kutoa usiweke vigingi ili na wengine wakuamini na roho yako mbaya.
Kuwa na roho ya kibinadam japo kidogo. Sio kila mtu kwamba anataka kuwa omba omba.
Na wasi wasi na wewe sio Mtanzania.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…