NAOKUAMBIA USIENDE DODOMA WANA MAMBO HAYA:
Kuna makundi matatu tu ya watu wanaokataa uje Dodoma:
1. Wamefanikiwa wakiwa Dodoma.
Hawataki competition. Wamejenga biashara zao, wamepata kazi nzuri, hivyo hawataki mtu mwingine aje achukue nafasi. Watakuambia "kule hakuna kitu" kumbe wanailinda keki yao.
2. Waliishi Dodoma wakajivuruga wenyewe.
Maisha yaliwashinda sio kwa sababu ya Dodoma, bali kwa sababu ya maamuzi yao. Walitumia vibaya hela, hawakuwa na nidhamu, mwisho wakarudi kwa wazazi. Sasa wanasingizia mji.
3. Hawajafika huko
Wanasikia kwa watu. Anasema kule kuna joto hajawahi kufika hata Bahi. Anasema kule ni mbali kumbe hata ramani ya Tanzania hajui.
UKWELI KUHUSU ISSUE YA "MAISHA MAGUMU DODOMA
Watu wengi wanapofika hapa ndipo wanakosea. Wanakimbilia nyumba za bei rahisi bila kuuliza mtaa gani.
Ukifuata huu ndio ukweli:
1. Kila mji una mitaa miwili.
Kuna mtaa wa kawaida na mtaa wa kishua. Dodoma sio tofauti. Ukienda Ilazo, Area D, Medeli utakuta bei tofauti na ukienda Ntyuka au Swaswa.
2. Nyumba nyingi ni mpya.
Tofauti na miji mingi ambapo nyumba ni za zamani, Dodoma nyumba nyingi zina tiles, hazina fangasi, ni mpya. Ndio maana zinaonekana kama ghali, lakini unalipia ubora.
3. Chakula cha 1,500 kipo na ni kingi.
Mipango, Mnada Mpya, Machinnga Complex, CBE, Area 77... vyakula vya 1,500 - 2,500 vipo kila kona. Hata ukienda Restaurant kama Chief Asili bei bado ni nafuu sana ukilinganisha na restaurant kama hizo Arusha au Dar.
4. Usafiri ni rahisi.
Miji mingi usafiri ni bajaji. Hamna boda buku. Dar ndio unaona boda nyingi kwa sababu ndio lango la mafuta.
Dodoma kuna fursa nyingi kuliko unavyofikiria:
Ofisi za Serikali, Vyuo vikuu, Kilimo & Ufugaji, Biashara ya Usafirishaji, na Biashara ya Chakula.
U
SHAURI WANGU BINAFSI:
Watu waliokuambia Dodoma chakula ni bei? Wewe nenda kafungue biashara ya chakula.
Waliokuambia usafiri ni bei? Wewe nenda kafungue biashara ya usafiri.
Usisikilize maneno. Nenda kaone fursa.
Sio salary city bana ni kweli ni pagumu ila side hustle zipo kibao na unatoboa.
Furniture, maduka ya hardware, viwanda vya ufyatuaji matofali, mini supermarket za mitaani, restaurants
Restaurants za dom zinawapa sana wafanyakazi wao utajiri
Yaani Ukitoa Dar ni Dodoma au Mwanza sehemu ya kutafuta maisha.
Sehemu nyingine zote kazi au pesa ni seasonal.
Mfani, Arusha - Hadi msimu wa utalii( high season)
Mbeya /mikoa ya nyanda za juu - Msimu wa mavuno
Kusini, Msimu wa korosho.
Faida, unaweza kuoiga pesa ndefu kwa muda mfupi, lakini sio kama cash flow.
Dar & Dom utapata pesa za kawaida kwa kipindi kirefu, hapo nidhamu yako ndio itaamua,
Kanda ya ziwa, Mwanza, Shy, Geita & Mara - Madini.