Ninataka nikajaribu hustling Dodoma wakuu

Ninataka nikajaribu hustling Dodoma wakuu

Zingatia haya kabla ujaenda Domland

uwe na fani yoyote kama ufundi nk
uwe na mtaji wa kutosha kama unaenda kufanya biashara
uwe na ndugu au mwenyeji ambaye utakaa kwake hadi upate chumba chako

elewa kwamba
dodoma inabamba sana kipindi cha bunge na kipindi cha mavuno

dodoma ina mchanganyiko mkubwa wa watu hivyo matukio ya uhalifu yapo sn

kuoa mrangi sikushauri ni wanafiki sana na wanaroho ngumu hao wanaoana wenyewe kwa wenyewe
na kipindi cha mavuno

Dodoma wanalima nini?
 
Kule kuikacha Dar tena kwa hoja yenye mashiko,unaonesha unajielewa. Wengi wanaenda huko kwa mkumbo tu.

Juzi tumeona yule jamaa wa Kyerwa aliyefiwa mzazi,kaacha fursa kibao huko kwao kang'ang'ania Dar hata nauli za kurudia kwao tu hamudu na anataka achangiwe kurudi huko!!

Dom fursa nyingi kwa anayejitafuta,asiyechagua mishe.
 
Kule kuikacha Dar tena kwa hoja yenye mashiko,unaonesha unajielewa. Wengi wanaenda huko kwa mkumbo tu.

Juzi tumeona yule jamaa wa Kyerwa aliyefiwa mzazi,kaacha fursa kibao huko kwao kang'ang'ania Dar hata nauli za kurudia kwao tu hamudu na anataka achangiwe kurudi huko!!

Dom fursa nyingi kwa anayejitafuta,asiyechagua mishe.
Dsm saa hv ina overpopulation mkuu, imejaa watu wa mikoani, wote kila anayefika anataka afikie kiwandani, afanye biashara kariakoo, kariakoo yenyewe imejaa mpk chalamila kaingilia kati, dar fursa ilikuwa miaka ile kina harmonize wanakwenda kutafuta maisha sio leo, nna dadaang na mumewe wanaishi kwa shida mno huko
 
Naana watu wengi wanaochangia huu uzi hawaijui dodoma, niko hapa dodoma miaka zaidi ya saba, kama unataka kujitafuta sikushauri kabisa, tafuta miii inayochipukia uende huko, Tunduma, kahama, katoro, masasi, na kwengineko, hakuna msimu wa mavuno hapa, hakuna viwanda wala nn, just a salary city, gharama ya maisha iko juu sana hapa, hakuna bodaboda ya buku hapa
 
Ndio hivyo wazee kutokana na umri wangu wa miaka thelathini(30) kunigongea nikiwa sina mfumo mzuri(sijafanikiwa kupata kazi rasmi ya uhakika iwe kuajiriwa/kujiajiri,sjafanikiwa kuoa, nimeamua nijilipue niende DOM.

Nimefanikiwa kuishi Mbeya, Sumbawanga, Katavi, Mafinga-Iringa, yaani huku nyanda za juu kusini ambako ndio kwetu nimepambana kama miaka 7 sasa tangu nigraduate ila ni mwendo wa pesa ya kula na pengine ndiyo yale ya nabii na kwao.

Kama ni CHUNYA huko machimboni nako mambo sio poa siku hizi tu tofauti na zamani, machimboni wanafaidi wale wadosi wenye mashimo au makarasha yao,mchimbaji na mtumia nguvu kitengo chochote sometimes unaishia kula ugali maharage dagaa wa bure huku ukipigwa na jua tu,

Nimechagua DOm na sio ARUSHA au DSM kwa kuwa nimefanya utafiti mdogo kwamba hiyo miji ilikuaga ina fursa zamani, sio leo, na nna ndugu kibao wapo huko miaka na miaka sometime mimi niliepo mkoani huwa nawasevu wanapotingwa, hiyo miji maisha magumu sana siku hizi ila DOm ndio mji unaochipukia japo sijawahi kuishi nna imani life lake kidogo ntatoboa tofauti na dsm au A-town.

AU mnasemaje wazee, wale mliopo DODOMA mje mnishauri basi kijana wenu. Nije Dom pengine ntaotea hata mrangi wa kujenga nae maisha, huku kusini nimepambana a lot.huko ntaanzisha kabizness kokote nione upepo

Kabla hujaja Dom jiulize kwanza ni kitu gani umetafuta / umefanya uko mikoa mingine umekosa na unaamini utakipata Dodoma .

Usije tu eti unakuja kutafuta maisha. Jua kabisa unakuja kufanya nini , unaanzia wapi, una resources gani.

Ukija njoo na life plan Kama hujui unakuja kufanya nini au unafata fursa ipi usije mkuu.

lengo kuu ni kusettle na kutafuta solution ya kudumu. Unaweza ukajikuta 40s inakukutia Domna bado hujapiga hatua. Utahamia mkoa meingine tena.

Life lina gharama sana apo central zone.unaweza ukaishia kupata hela ya kula tu.
 
Back
Top Bottom