Ninataka nikajaribu hustling Dodoma wakuu

Ninataka nikajaribu hustling Dodoma wakuu

Mkuu

Yani ni balaa nilikaa karibu na soko la Mavunde.

Akipata muda aende chako ni chako akale kuku.

nimekumbuka mbali

Maeneo kama Majengo, Chako ni chako, Uhindini karibu na soko la sabasaba
Chadulu, ipagala Kikuyu, Chinangari, gwasa, Chamwino, kikuyu, kilimani, Area C kule mnadani maili mbili, Msalato kule wanapojenga uwanja wa ndege

ila kwa kujitafuta kimaisha sio lazima afikie mjini yapo maeneo kama Kibaigwa, Mpwapwa, Mvumi, Mtumba akipata mwenyeji huko anaweza kuanzia kukaa kwanza pembeni ya mji
 
Ndio hivyo wazee kutokana na umri wangu wa miaka thelathini(30) kunigongea nikiwa sina mfumo mzuri(sijafanikiwa kupata kazi rasmi ya uhakika iwe kuajiriwa/kujiajiri,sjafanikiwa kuoa, nimeamua nijilipue niende DOM.

Nimefanikiwa kuishi Mbeya, Sumbawanga, Katavi, Mafinga-Iringa, yaani huku nyanda za juu kusini ambako ndio kwetu nimepambana kama miaka 7 sasa tangu nigraduate ila ni mwendo wa pesa ya kula na pengine ndiyo yale ya nabii na kwao.

Kama ni CHUNYA huko machimboni nako mambo sio poa siku hizi tu tofauti na zamani, machimboni wanafaidi wale wadosi wenye mashimo au makarasha yao,mchimbaji na mtumia nguvu kitengo chochote sometimes unaishia kula ugali maharage dagaa wa bure huku ukipigwa na jua tu,

Nimechagua DOm na sio ARUSHA au DSM kwa kuwa nimefanya utafiti mdogo kwamba hiyo miji ilikuaga ina fursa zamani, sio leo, na nna ndugu kibao wapo huko miaka na miaka sometime mimi niliepo mkoani huwa nawasevu wanapotingwa, hiyo miji maisha magumu sana siku hizi ila DOm ndio mji unaochipukia japo sijawahi kuishi nna imani life lake kidogo ntatoboa tofauti na dsm au A-town.

AU mnasemaje wazee, wale mliopo DODOMA mje mnishauri basi kijana wenu. Nije Dom pengine ntaotea hata mrangi wa kujenga nae maisha, huku kusini nimepambana a lot.huko ntaanzisha kabizness kokote nione upepo

Wew hata ukienda kasulu,hiyo ndo njia uliyochagua mwenyew
 
Mkuu kwahiyo vyumba vya kuforce hata kwa 30 single hamna
Sina uhakika kama vinaweza kupatikana chumba cha 30,000

Labda kule Mtera ama Mpwapwa, lakini kwa hapo town sio rahisi

Lodge zenyewe standard, zinaanzia 50,000

Wakati kule Mbeya, 50,000 unalala hotelini 🙌

Sijajua mishe unayotaka kufanya, lakini ungekwenda Chunya, kule hela ipo
 
Kama unaanza kupambania maisha, nakushauri ungerudi Mbeya pana fursa nyingi na kama upo serious utawapiga bao vijana wa Mbeya sababu wengi ni wavivu na wakipata kipesa kaduchu wanakimbilia kulewa.
Dom panakua kwa kasi lakini garama za maisha ni ghali sana.
Mimi pia ningeshauri hivyo, kule Chunya hela ipo na mzunguko ni mkubwa pia
 
Dodoma mzunguko wa pesa upo, hilo linapelekea maisha kuwa ghali
Hivyo kwa watafutaji beginners inakua disadvantage ila ukikomaa unatoboa

Unajipanga kufanya shughuli gani/ biashara?
Una pesa ya kuanzia kiasi gani?
Unafikia kwa ndugu au unakuja kuanza moja?
Hapa mkuu nitajaribu kufanya mawasiliano na ndg yangu mmoja kama itakuwa nouma ntapanga tuu, hapa nna kilaki tano tu
 
Kama unaanza kupambania maisha, nakushauri ungerudi Mbeya pana fursa nyingi na kama upo serious utawapiga bao vijana wa Mbeya sababu wengi ni wavivu na wakipata kipesa kaduchu wanakimbilia kulewa.
Dom panakua kwa kasi lakini garama za maisha ni ghali sana.
Kwahiyo ni kama arusha sio
 
Mkuu

Kila la kheri, kwa kukushauri jaribu kuishi maeneo ya chang’ombe, nkuhungu au kwa waziri mkuu kule kidogo vyumba single unaweza pata 50k.

Palinishinda hali ya hewa sema ni pazuri.
Kudadek mkuu, 50 mbeya unapata self pale block t, uhindini na airport ya zaman
 
Zingatia haya kabla ujaenda Domland

uwe na fani yoyote kama ufundi nk
uwe na mtaji wa kutosha kama unaenda kufanya biashara
uwe na ndugu au mwenyeji ambaye utakaa kwake hadi upate chumba chako

elewa kwamba
dodoma inabamba sana kipindi cha bunge na kipindi cha mavuno

dodoma ina mchanganyiko mkubwa wa watu hivyo matukio ya uhalifu yapo sn

kuoa mrangi sikushauri ni wanafiki sana na wanaroho ngumu hao wanaoana wenyewe kwa wenyewe
Duh nashukuru mkuu hii ni comment ya pili bora,kiufupi dom sio kama mbeya au darslaam, mitoto ya kirang mizuri ila duh bac
 
Back
Top Bottom