Nimepanga kuhamia Dodoma, nitoke huku niliko.

Ahmet

JF-Expert Member
Oct 15, 2019
1,537
3,404
Heshima kwenu wakuu,

Bila kupoteza muda, Mimi ni kijana wa miaka 27, kwa Sasa nipo kusini mwa nchi lakini siku za usoni natarajia kuhamia Dodoma ili nipambane mbali na nyumbani.

Nimefanya maamuzi haya kwa kuzingatia Mambo mengi:

Kwanza, Dodoma Kuna fursa nyingi za kiuchumi ambazo zimechagizwa na uwepo wa watu wengi (wanafunzi wa vyuo, wabunge, mawaziri na wafanyakazi wengi wa umma). Huku kusini hasa Lindi, kusema ukweli kumesahaulika kabisa, idadi ya watu ni ndogo na mzunguko wa pesa ni mdogo sana.

Pili, Dodoma ni makao makuu ya serikali na ofisi nyingi za umma ziko Dom. Nikiwa hapo sitawaza tena kuhusu interview za utumishi ambapo awali nilikuwa siwezi kuzifanya kutokana na umbali, yaani kutoka huku kwetu hadi Dom kuja kufanya interview ingenighalimu Sana ukizingatia pia interview zinakuwa nyingi kwa post moja (oral na written)

Tatu, ninapafahamu Dodoma kwa uchache, kwasababu nimemaliza degree yangu UDOM, kwaiyo Dodoma ni jiji nalolijua.

Nne, natamani kukaa mbali na home.

Tano, nimepapenda Dodoma.

Changamoto nayoipata (swali nalojiuliza) kwa Sasa ni nini nitafanya nikiwa Dodoma? Na hapa ndio nahitaji mawazo ya wadau na wenyeji wa Dom mnipe faida na hasara, raha na shida za kukaa Dom.

Mwenyewe niliwaza kufanya shughuli hizi,

Kwanza, Bodaboda (kwakua nina kamtaji kidogo naweza nunua pikipiki yangu hata used na Kuanza nayo biashara)

Pili, kuuza nguo na bidhaa nyengine ndogondogo

Tatu, shughuli yeyote ya mtaani Kama kubeba zege, kufyatua matofari n.k.

Kwasasa najipanga ili nisije mikono mitupu katika miji ya watu, nasubiri kidogo nijichange change ili nije vizuri.

Najua huu ni mpango tu na unaweza usiwe sahihi Sana, hivyo nahitaji ushauri wenu wadau, hali ikoje hapo makao makuu? Bei za vyumba vya kupanga ikoje?
Ushauri wenu ni wamuhimu sana, karibuni wanajamiiforums
 
D meker kama d meker
 
Asante kwa ushauri mzee
Kama kijana mjanja ishi miji mikubwa mana ina fursa sana..ila huko mikoani weka miradi ya mashamba..unaenda kipindi cha msimu tu.

Anza bodaboda uwe na uhakika wa kula..na kulala..

Dodoma ni mji unaokuja juu sana..ni sehemu nzuri ya kupambania kombe pia.

#MaendeleoHayanaChama
 
Inategemea una ndoto gani maishani. Sitarajii kuishi Dodoma milele na milele. Nina uzoefu na kanda ya ziwa, Kaskazini, nyanda za juu Kusini, Dodoma na Pwani. Dodoma maisha ni ghali na hakuna sababu ya kukufanya uishi uko kama hulazimishwi na kazi.

Kwa level zako nenda uko upambane hata mishe za bodaboda naona zina mzunguko sana maana wageni hawakauki mjini na wanachuo wengi tu. Kusanya pesa wekeza uko Lindi kwenu ambako ushamba ni mwingi (hili sio tusi ni uhalisia) hivyo fursa zipo za kutosha na gharama nafuu ya maisha. Dodoma nenda kusaka pesa ila usisake maisha.

Unaishi na wajanja unajifunza na kutafuta kisha unapata ujanja unaenda kwa washamba kupata hela zaidi
 
Nimepata kitu hapa. (Ila sisi sio washamba😂😂)
 
Karibu be ila Gharama za vyumba vya kupanga tu chumba Cha kawaida 60-70 permonth...karibu tulime ALIZETI pia japo sisi wenyeji tunatamani kusogea mbele Zaid kusaka maisha
 
Back
Top Bottom