Hornet
JF-Expert Member
- Apr 29, 2013
- 26,121
- 49,495
KiBiashara ukiwa mtu wa matumizi Sana, kupoteza Kwenye game ni dkk sifuri.
KiBiashara,
Unaweza ukawa unaingiza faida ya million kila sikU, kwa mwezi mzima mfulurizo ukagota 30 million profit.
Afu ghafla umepata bingo la mzigo wakusafisha stoo au haujalipiwa ushuru au mwenyewe anahama au kabadilisha biashara anauuza ROBO YA BEI, Anauza million 30 chap.
Na wee unaona kabisa huu mzgo, nikachukua unaleta million 120 chap.
Sasa
Kama bahat mbaya huna akiba ya mil 30 kuulipia Chap (wee faida ukipata unakulaga),
Unakua tayar umeshapishana na BINGO la fasta.
AU BAHAT MBAYA IMETOKEA,
Majanga yametokea (Moto,wezi,kesi n.k) inahitajika mil 30 ikutoke mfukoni chap uweze kuchomoka Kwenye msala, vingenvyo unatangazwa umefilisika.
Sasa Kama mwenzangu na mie,
Mzee wa kulaga faida, Inakua ndio baibai tunasahau kwenye GAME.
MFANYABISHARA UNAPASWA KUSPEND LOW as much as you can.
Biashara hazitabiriki,
Unaeza amka maskini, ukalala tajiri
Au ukaamka tajiri, ukalala maskini.
YOTE YANAWEZEKANA
Kuna mzee pale kkoo sokoni
Yeye mauzo alikuwa anachanganya anachukua mzigo juu ya mzigo
Hili janga la juzi la moto sijui limemuacha katika hali gani!!