Ninakosea wapi? Au biashara ni kipaji?

dimple

Member
Dec 6, 2016
46
125
Ndugu nimeapa mr aliweka mdogo wake alichofanya ku kumimba wadada akiwadanganya yeye ni boss mwisho wa siku hakuna alichoingiza alipata hasara hadi alitaka kupata stroke tena alikua mbion aache kazi sasa baada ya kuona kajikusanya vya kutosha wee sitakaa kusahau ilibidi kama mke nishike usukan nimeshaandaa kombora kwa shem nita mfire hatokaa aamini namlia tyming tu kuhakikisha naelewa everything nikishakusanya kila kitu.
Mtoa mada nakushauri Jambo moja.

Kwenye iyo biashara yako,
Ondoa uyo mfanyakazi.

Weka mkeo,
Kama ujaoa ,oa haraka ili ujipatie cheap labor kwa msimamizi mzuri kabisa wa biashara yako.

NB: ndugu nao sikuhizi Ni magumashi. Niulize kwanini
 

Wanama

Senior Member
Jun 12, 2021
138
250
Kama ukitoa kila kitu kuanzia mshahara/matumizi yote unabakiwa na faida ya 80,000 to 100,000

sikushauri uache hiyo biashara hata kidogo,wewe kilio chako ni faida ndogo ila si kwamba hupati kbsa

wenzako wanaliaga hawapati kabisa,80k usiichukulie poa kwa biashara, hebu jiulize biashara yako hiyo

ukiendaga fata mzigo wa 80k unachukua vitu kiasi gani?! assume huitumiii hiyo hela iache usiiguse kwa

miezi 10 tu Utakuta kibubu kina 800k hivi ukijikaza ndani ya 10month ukichukua ile 800k ukairudisha yote

kwenye hiyo biashara yako unahisi utakua na stationary ya ukubwa gani? Shida yenu watu mliozoea ajira

mnapenda mahela mengi mengi yanayokuja kwa mara moja kama mishahara yenu ilivyo, Biashara/ujasiriamali haupo hivyo.

Huku tunakusanya sh 200 tu sh 100 tu sh 50 tu sh 500 then total tunakuja ipata baada ya miezi kadhaa SO mkuu nikwambie tu kitu, Biashara yako iko vizuri sana komaa hapohapo Punguza matumizi yasio na lazima

graph yako ya income kwa mwezi itaongezeka,Kingine akili yako iruhusu kufanya kazi zaidi unapoona biashara inakupa income ndogo usifikirie kuiacha "utaacha biashara ngapi"?

jifunze kuweka akiba na kujiona kama huna biashara ongeza biashara nyingine na nyingine kupitia hicho kidogo unachokipata kwa mwezi "biashara za mitaji ya laki zipo kibao" zifanye.

kuwa na biashara nyingi ndogo ndogo unapofika mwisho wa mwezi ukikusanya kote Utajikutaa mfukoni una not less ya 3 to 4m (depends na vibiashara vyako) Acha kupasuka kichwa na biashara kubwa kubwa.

Umeingia ktk ujasiriamali Cheza namba zote cheza miguu yote Kuwa kiraka kama mcheza mpira anaetumia left n right...

Mwisho : Usifunge wala usiache hiyo biashara bali itumie kama sehemu ya kupatia mitaji ya vibiashara vyako vingine... Go ahead Champion...
Pesa za mdada yule usharudisha?
 

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
14,299
2,000
ndugu nimeapa mr aliweka mdogo wake alichofanya ku kumimba wadada akiwadanganya yeye ni boss mwisho wa siku hakuna alichoingiza alipata hasara hadi alitaka kupata stroke tena alikua mbion aache kazi sasa baada ya kuona kajikusanya vya kutosha wee sitakaa kusahau ilibidi kama mke nishike usukan nimeshaandaa kombora kwa shem nita mfire hatokaa aamini namlia tyming tu kuhakikisha naelewa everything nikishakusanya kila kitu.
Ndugu Ni sumu Kabisa
 

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
14,299
2,000
hii ni kweli mr wangu anahuruma mnooooo na hakuna anachofanikiwaga hadi sasa nimeacha kupartner nae ktk biashara sabab tunaelewana vizuri wafanyakaz wote wanaripot kwangu unakuta wakianza fanya madudu wananikimbia wanaripot kwake na anawasikiliza at tgw end hakuna ni hasara juu ya hasara nakumbuka kuna kipindi kawekeza sehemu zaidi ya mil 10 hajawahi kula hata elf 50 anakuwaga anawapa darasa ila waaapi msimamizi ndo kwanza akaoa na kuzaa kwa pesa zake haki ndo siku nilijivua kufanya nae biashara niliona nikizubaa nimekwisha mm na wanangu now ninachomshaur awekeze ktk nyumba za kupangisha tu biashara hawezi hana roho ya kijasusi kusimamia biashara.
Bwana ako ana tabia za kijamaa na kujuana Juana kwenye pesa.

Pesa haihitaji Ayo,

Pesa na kujuana Juana Ni vitu viwili tofaut, Ukileta za kujuana Unapotea fasta kwenye game.
 

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
4,991
2,000
Bora wewe. Wenzako tulifilisika tulipokopa pesa na kufungua maduka.
Mtafute mfanyakazi mwingine kisha angalia mapato au siku mbili mfululizo kaa ukihesabu mapato asubuhi mpaka jioni.
Kisha uje unishukuru
 

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
14,299
2,000
hapa ni mtaji wa milion 3 mauzo hayafoki elf 20.kwa siku hata muuza.nyanya mtaji wa laki 2 anauza zaidi ya elf 20.huyu hajajiongeza kwanza anatoa mshahara mkubwa pili posho acancel tatu kama ataweza afunge camera ofisini
Analipa kipedeshee Sana,

Kwa mtaji wa mil 3 Kuna vitu Kama printer,photocopier,scanner, lamination,computer.

Vyote hivi vinaupunguza mtaji wake, usikute kinachozungushwa ni mil 1 TU ukiondoa Ayo makorokocho juu
 

sengobad

JF-Expert Member
Aug 13, 2017
4,572
2,000
Hii biashara ya kitambo mkuu ni miaka mitatu sasa, huwa najipa matumaini ipo siku itakuwa ila wapi,

Gharama nlizotumia kuanziha biashara,

photocopy 1,800,000
printer ya rangi yenye scanner - 450,000
computer 400,000
lamination 100,000
kalamu, bahasha, madaftari, n.k - milioni 1

Gharama za kila mwezi

chumba - 100,000
Mshahara - 100,000
chakula, choo, taka, usafiri - 90,000
Umeme - 20,000

Jumla ya mapato yanacheza kwenye laki 4 na kitu, mara chache inazidi
Nikipata sehemu kama hiyo dah! nitapiga hela mpaka baasi. Hiyo hela ni nyingi sana sema kinachokuathiri wewe ni mwajiriwa kama ungekuwepo mwenyewe kipato chako kingegonga 2mln. Huyo mdada ndiye anayekuangusha, hataivyo ndivyo ilivyo mambo mengi hana maamuzi nayo mpaka akupigie simu na wakati mwingine simu unapokea ukiwa umechelewa na mteja alishaondoka.
 

JUDIKAY

Member
Jul 20, 2021
63
150
Hbarini wafanyabiashara.

Binafsi ni kijana nimeingia 31, ni muajiriwa seikalini shirika flani, Nilikuwa navutiwa sana na ujasriamali hivyo na mimi nikaona nisijivunge.

Kwa Biashara yako angalia
Eneo la biashara je linamzunguko wa kuwezesha biashara yako kuuzika kwa wingi?

Kwa kuwa biashara ni mpya , ungetakiwa uanze nayo wewe mwenyewe au umuweke mke wako lengo ni kuijua biashara yako

Na kama faida ndio hiyo unatakiwa kupunguza matumizi kama mshahara , posho , kodi n.k

Pia biashara zetu hizi huwa kupata faida kubwa sana unabidi ukomae mwenyewe yani ujitafutie wateja wako kwa kuwapa huduma nzuri, wafanyakaz ni wachache wanaoweza kumcare mteja hadi anaridhika

Mwisho kama kuna uwezekano ukachukua likizo ukakomaa kipindi chote cha likizo ili ujue changamoto zinazoikabili biashara yako uweze kuzitatua
 

6Was9

JF-Expert Member
Mar 2, 2021
1,200
2,000
Kingine nnachokiona,
Mfanyakazi wako anafaidika San na ofisi yako.

Kumlipa 100,000 afu ukamuongezea posho ya siku, hapo bado hajajiongeza za kwake Apo ofsini.

Binafsi,
Huo mshahara ningetakiwa kulipa kwa biashara yenye mtaji usiopungua million 50, na yenye mzunguko usiopungua mauzo ya millioni 1 kwa siku.
Pia biashara inatakiwa kua na uhakika wa kuingiza faida isiyopungua Laki 1 kwa sikU nzima baada ya Kutoa matumizi Yote ya ofisi kutwa nzima.
Mkuu wewe ni muhindi ?
 

Waterloo

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
22,006
2,000
Biashara zipo nying ndugu chakata ubongo huo...na hapo ndo kwenye kaz nzito...nna ka chemba kangu ka1 mtaj wake ni 1m ila kwa mwez kananipa 160k...na nnaweza nisiende kukazungukia kuangalia hata miez miwil..ila kanajiendesha kenyew tu

Ni lazima uumize akil kwelkwel kupata idea hiz za biashara...msome sana huyo jamaa controla nyuz zake utapata kitu

Mim miaka miwil au mitatu nyuma huyo jamaa alibadil life langu kwenye upande huo wa ujasiriamali...so komaa nae
Kuna uzi humu Controla katapeli hela za watu kwahiyo kuweni makini.
 

Trubarg

JF-Expert Member
Jan 8, 2020
2,372
2,000
nilivyoelewa mm ni kua mauzo ni laki 4 hdi 4.5 kwa mwezi na matumizi kila kitu kwa mwezi ni laki 3 na kumi hapo vitu vinapungua sababu si vinauzwa kama wino karatasi pen daftari n.k sasa sijui kwa nn wanampigia hesab za faida ya elf 80 huyu jamaa anapata hasara sio faida na kuna wizi sana stationary wale watu ni wajanja sana pia wanaweza hata pata tenda za kadi za harusi na wasikwambie huyu kama anapata faida haizidi elf 30 kwa mwez
Upo sahihi
 

dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
4,801
2,000
Hii biashara ya kitambo mkuu ni miaka mitatu sasa, huwa najipa matumaini ipo siku itakuwa ila wapi,

Gharama nlizotumia kuanziha biashara,

photocopy 1,800,000
printer ya rangi yenye scanner - 450,000
computer 400,000
lamination 100,000
kalamu, bahasha, madaftari, n.k - milioni 1

Gharama za kila mwezi

chumba - 100,000
Mshahara - 100,000
chakula, choo, taka, usafiri - 90,000
Umeme - 20,000

Jumla ya mapato yanacheza kwenye laki 4 na kitu, mara chache inazidi

Mkuu mimi nina hali kama yako ila nakomaa tu mwaka wa 5 huu.
 

dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
4,801
2,000
Kuna wakati mwingine tunaona biashara inalipa kabisa ila huioni hiyo hela unayoitegemea

Kama biashara ni ya kumuachia mtu akufanyie hata uchunge vipi kama anataka kupiga anakupiga tu

Unaweza kukuta wateja wengi ila mauzo madogo upande wako kumbe na muuzaji ana biashara yake humo humo akiuza bidhaa zake hizo hizo kama zako
Mwisho wa siku bidhaa zako anauza na zake pia
Sio wote wanaofanya hivi ila wapo wanaofanya hivyo kwenye biashara za watu

Usife moyo bado unafanya vizuri kwa mtaji huo ila angalia mianya yote

Weneyewe wanasema anafungua Duka ndani ya Duka
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom