Nina wivu nashindwa hata kumeza mate! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nina wivu nashindwa hata kumeza mate!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Annina, Jan 7, 2010.

 1. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wapendwa,
  Nipo kwenye serious mahusiano na kwa mapenzi ya Mungu tunaweza kufunga ndoa. Tatizo nina wivu kupita maelezo, yaani saa zote nahisi kuibiwa...kwa mfano kuna siku nilikuta amempa lift zilipendwa wake na alikuwa amekaa kwenye siti ya mbele ya abiria, niliumia kupitiliza nikaacha kuitumia ile siti, kuanzia siku ile nikawa nakaa siti ya nyuma kama balozi! Baada ya muda akabadili gari -thanx God sasa nakalia siti yangu!

  Nyumba anayoishi nimebadili karibu kila kitu kwani nahisi vina uhusiano na mpenzi wake aliyepita na vinaweza kumkumbusha waliyokuwa wakifanya - siwezi kuvumilia, nimembadili hata yeye - mavazi, perfume, sehemu za kutembelea nk nk yote hii ni kuhakikisha mimi ndio natawala mawazo yake na si vinginevyo, lengo ni kwamba kila kitu kinachomzunguka kiwe kinamkumbusha mimi! Akisafiri tunakesha kwa PC na simu... kuhakikisha yupo peke yake nitamtaka afanye mambo kadhaa ili nijiridhishe siibiwi... msg zikiingia kwenye simu yake mapigo ya moyo yanabadilika...huwa najitahidi kujizuia kusoma msg hizo lakini asiponiambia nani ametuma na kuniruhusu kusoma naweza kukosa usingizi siku kadhaa!

  Jamani nisaidieni, ni mimi tu au na wengine wako hivi? Nina wasiwasi atachoka, kuna wakati naona namnyima uhuru, najaribu kujizuia lakini nashindwa, nifanyeje?

  Annina
   
 2. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mara nyingi wenye wivu mkali hata wao huwa si waaminifu. Na huhisi yale anayomfanyia mwenzake na yeye anafanyiwa hivyohivyo. Jichunguze kwanza mwenendo wako. Or huyo uliyenaye alishakujeruhi na hupendi arudie tena.

  Kama hayo yote hayapo na bado una wivu, basi kuna kazi kubwa. Manake huo sasa ni wa kurithi kama si kuzaliwa nao. Na mbaya zaidi utakayekuwa unaumia kila siku ni wewe na siyo yeye.
   
 3. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Asante Vangi,
  Namshukuru Mungu mimi ni muaminifu kwa asilimia zote. Huyu nilie nae hajawahi kunijeruhi - ila niliwahi kujeruhiwa huko nyuma. Tatizo jingine nawekeza rasilimali zangu zote kwenye mapenzi - siwezi kupenda kwa kiasi au nusunusu kama wengine wanavyofanya, labda hili nalo linachangia.
   
 4. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kwa jinsi ulivyojieleza inaonesha wazi unalitambua tatizo na hata nini cha kufanya unajua pia. Cha muhimu jitahidi usimjengee mawazo ya kutokujisikia huru anapokuwa na wewe manake hii hali inaboa na itamfanya akuchoke mapema.
   
 5. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2010
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mapenzi bila wivu hayaendi lakini huu wako umezidi sasa, noma tupu!!
   
 6. m

  madule Senior Member

  #6
  Jan 7, 2010
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana, you are focusing so much in what may not be existing. chagua tuu kumuwazia yaliyomema mwenzio. maana kila unaloliwazia huwa ndilo linatokea hivo ukimuwazia kuwa anamahusiano ina maana kwa kufanya hivo utafanya awe na mahusiano na ww ndiye utakuwa umeleta hiyo hali.Jipe raha nayo itawatawala wote na mwenzio. hiyo halia ya kuumia moyoni na kujikaza kujifanya upo ok haimaanishi kuwa hatambui hiyo hali, maana fikra zina mawimbi na mawimbi husafiri bilA KINGO YOYOTE NA HIVO HISIA ZAKO KUWA HUPO NA AMANI ZINAFIKA KTK FIKRA ZAKE, na hapo ndio mwanzo wa kuhalibu. what you feel is much important than what you think!
   
 7. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Kama ni una wivu basi achana ma mchezo wa mapenzi, kwani jinsi mtakavyo funga ndoa ndio mtakavyo tua ule mzigo wa kuact kwamba nyie ni wazuri kwa kila kitu, sasa hapo ndipo uhalisia hujitokesa na hali yakuzoeana inapo ibauka na kusababisha kuona unaibiwa zaidi na zaidi.

  Kifupi kama unaingia kwnye mapenzi na ndoa jaribu kupunguza wivu la sivyo ndoa na penzi itakua ni hell
   
 8. shejele

  shejele Senior Member

  #8
  Jan 7, 2010
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mwana FA alishawahi kuimba hivi "unafanya nijitambueee dunia niijueee, naamini unaniamini na we amini naamini"
  ukiachilia mbali wivu wako huo uliopitiliza lakini pia inaonekana humuamini mwenzako. Jifunze kumuamini utafurahia maisha.
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Wivu ni kama ugonjwa vile. Kama hajakupa sababu ya kutomuamini, basi omba Mungu akusaidie upate nguvu za kumwamini. Lakini kwanza lazima ujiamini mwenyewe. Na ukishajiamini na kujua na kuamini kuwa anakupenda basi utapata nguvu za kuushinda wivu wako.
   
 10. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  angalia sana huo wivu wa haina hio sio mzuri hata kwa afya yako.kama unaona humuamini mpenzi wako basi subiri kwanza mpaka mda muafaka ukifika na unajiona utaweza kumudu ndoa au uhusiano wa karibu wa kimapenzi ndio uanze la sivyo unaweza kufanya maamuzi ya ajabu.
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Control freak
   
 12. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #12
  Jan 7, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo lako tayari unalikjua, ni mwanzo mzuri.

  kwa kiasi kikubwa umeathirika na yaliyokukuta kabla hujakutana na huyu wa sasa. unapaswa kupuuza historia hiyo ya kutendwa na kuamini uwa yalipita na hayajirudii.

  pia kumbuka mwanadamu halindwi. rejea maandiko yasemayo "Bwana asipoulinda mji, waulindao wanakesha bure" kama kweli unampenda muondolee usumbufu uletwao na wivu na zidisha upendo hasa nyumbani ili apaone mahali pazuri pa kuishi.

  pia nasauri kama hakuna sababu ya msingi ya nyie kutofunga ndoa kwa wakati huu, basi fungeni na mzae mara moja kama sehemu ya jibu la tatizo lako. watoto husaidia kupunguza wivu na kuongeza imani baina ya wanandoa.
   
 13. P

  PELE JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 229
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Annina utakufa siku si zako ukiendekeza wivu kiasi hicho. Kumchunga binadamu si rahisi kabisa. Akitaka kufanya madudu yake atayafanya tu hata kama utajitahidi kumbadili kwa kiasi gani. Kama humuamini kutokana na matendo yake ni bora kuingia mitini mapema kabisa.

  Na hiyo ya kumpa lift zilipendwa wake ni NO NO NO, nashangaa uliruhusu kitu kama hicho. Zilipendwa zinabaki zilipendwa mambo ya kupeana lift hayaruhusiwi kabisa au wanaweza kabisa kukumbushia enzi zao.
   
 14. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #14
  Jan 7, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  hapa utakufa siku si zako! ohoo

  hivi ukaa kwenye siti ya mbele ndo aliondoka nayo? si ilibaki? halafu tabia ya kususa namna hiyo si nzuri, sijui kama ulikuwa unampa maelezo gani kwa nini huketi tena mbele? usipoangalia atamrudia zilipendwa wake....ohooo

  Mbona unajidanganya ivo Annina? huwezi kumbadilisha mtu ki ivyo...uliza uambiwe


  hhehehe jamani, kama ugonjwa wa moyo unautafuta mwenyewe...lakini nashindwa kuamini kama hii ni kweli! yeye anasoma za kwako?

  Mi nahisi ni wewe tu, cha kufanya acha mara moja huo utaratibu wako..mwanaume hachungwi ivo kawaulize mabinti wa kitanga waliofundwa.....hiyo 'command and control' haitakufikisha popote na usitarajie ndoa hapo....mwachie uhuru wake kama anavokuachia wa kwako!
   
 15. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #15
  Jan 7, 2010
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nakiri kukuelewa kwa kina kwa jinsi ya tabia yako ya kupenda sana na kuwekeza kwenye mapenzi kwa sana.Sasa ndugu yangu+ kabla mwisho mbaya haujakufika fanya mambo muhimu yafuatayo;

  1.Chagua kuishi au kufa
  2.Kama umechagua kuishi basi usielekeze akili yako kwenye kitu mapenzi
  3.Kama umechagua kufa hakikisha siku anakuacha au unamkuta na mwanaume mwingine kuwe na shahidi wa kutoa maelezo ya kifo chako
  4.Zingatia na.2 na 3 hapo juu
  5.Unahitaji maombi na sala ya toba
  6.Ahirisha kufunga pingu za maisha na huyo mdau hadi hayo hapo juu yametimizwa.
  7.Usisubiri kuambiwa sasa umekata roho bali ukisikia dalili hizi ujue umeondoka duniani;
  i) Moyo kwenda kasi na kukosa usingizi
  ii)Kifua kubana na pumzi kupungua
  iii)Kupiga miayo na kusikia kiu
  iv)Kwenda haja kubwa mara kwa mara nk
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  eeeh madame mbona wivu wako umepitiliza mipaka ...mie nina wivu ila wako ni too much unaweza kufa hivi hivi tunaangalia

  amini unapendwa lakini hayo mengineyo ukiyafatilia utashindwa kuingia kwenye hiyo ndoa
   
 17. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #17
  Jan 7, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  kwani wewe zilipendwa wako umemsahau maoja kwa moja?
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Jan 7, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  hapo kwenye green kweli jamaa anaweza kuona ameruka mkojo akakanyaga mavi ni bora arudi aliko toka kuna pumziko la milele
   
 19. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #19
  Jan 7, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  unajua hutu tubinti tudogo tudogo tunatoangalia tamthiliya na nini TUNASUMBUA SANA HUTU!

  mimi mwanamke wa kunibana hivyo atanipoteza so soon
   
 20. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #20
  Jan 7, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Ni akili ya mtu Geoff lakini ukiwa mwizi na wewe siku zote unawaza kuibiwa tu ..

   
Loading...