Nina ujauzito - nimekata tamaa

Nina ujauzito - nimekata tamaa

Unapoamua kufanya kitu usifanye kwa kutegemea fulani atakusaidia. Hiyo mimba imekalia mkononi au miguuni? Kwani bila huyo mwanaume huweziishi. Acha kufikiria ndani ya box toa kichwa nje.
 
Zaa tu, mie nitalea mtoto. Ila ukimuacha usigeuke nyuma asilani, pretend kama ulitoa hivi.

Ungekuwa na miwaya je?!
 
Njoo nikupe dawa nzuri ya kufanikisha tukio fasta fasta, huteseki unakwenda ukiwa usingizini.
 
Wewe jack 1, sasa unataka tukusaidieje ili kufikia malengo yako? Tukununulie SUMU?

Hivi wewe kwa akili yako ulishawahi kujiuliza haya? Itakuwaje ikitokea wazazi wako wote wamekufa? Utaishije?

Au, Huyo alokupa ujauzito nae amekufa, inakuwaje?

Na pengine, huyu kidume akakubali kisha mbele ya safri akakunyanyasa. Imekaaje hiyo? Ni bora ukamshukuru Mungu kwani keshakuonesha the guy sio responsible father. Songambele, na huyo mzazi wako hawezi kukutupa.

Ukiona umezidiwa sana ni PM nitakupa ushauri utakaoondoa uwepo wa shetani akili mwako. Kuwa jasiri, wewe ndiye nahodha wa maisha yako, sio baba wala mchumba wako huyo mhuni.

Siku ingine usipende kutanua miguu na kuachia vidume vinaweka tu bila utaratibu.

Onyo: Mimba unaweza kuitoa, Je, vipi kuhusu UKIMWI?
 
sumu siku hizi zimekuwa kama lollipop!

kila anaejisikia analambalamba tu...!
 
Ungekua we wakwanza kukataliwa kweli kwani aliekupa mzigo hana ndugu nenda kwa ndugu zake
 
Ninaujauzito mwanaume kakataa mzazi wangu hataki hata kuniona na kasema nisikanyage kwake sina kazi nimeshindwa cha kufanya nimeona bora ninywe sumu tu nisameheni kwa maamuzi haya sina uelekeo.

Mzazi wako ana hasira tu, zikishashuka atakukubali. Ukweli ni kwamba umemkosea kwahiyo usimuwekee kiburi kwa kuonyesha hasira zake.
Tuliza akili, achana na mawazo ya kujiua na wala usiitoe. Tafuta ndugu(kama shangazi hivi) au rafiki wa karibu huko uliko umuombe ukae nae mpaka mzazi atakapokuita nyumbani.
Wanaume ndivyo walivyo dada, taratibu utajifunza.
Pole sana kwa yaliyokupata, Mungu akupe nguvu.
 
There is never a wrong time to do the right thing jack 1,kuna single mothers wengi ambao wamesurvive hardship kubwa kuliko hata ya kwako ila wamevumilia and went on to raise their kids. Acha negative thoughts, some wise dudes say "in the middle of difficulties times lives opportunity"
 
Last edited by a moderator:
Ninaujauzito mwanaume kakataa mzazi wangu hataki hata kuniona na kasema nisikanyage kwake sina kazi nimeshindwa cha kufanya nimeona bora ninywe sumu tu nisameheni kwa maamuzi haya sina uelekeo.

jacky, mimi mwenzio mamangu alikataliwa na babangu akiwa na watoto watano, kipindi hicho mimi nilikuwa na mwaka mmoja, hakuwa nakazi kama wewe lakini hakuwahi kufikiri kunywa sumu zaidi ya kupambana na maisha na sasa wote tayari ni watu wazima, iwaje wewe ufikirie kujiua kwaajili ya huyo mtoto mmoja ambaye bado hajazaliwa? Tulia,msahau huyo mwanaume, jipange vizuri, anza kuishi maisha mapya, mungu atawasaidia wewe pamoja na mwanao atakae zaliwa na atawafungulia milango
 
jack 1 natumaini umepata ushauri kati ya hizi post zote na mpaka sasa umeamua how to move on.

Maisha yanachangamoto nyingi sana dada wapo wengi waliopitia hayo unayopitia wakavuka na sasa
wana maisha ya furaha na watoto wao.
Huko ulipo huna marafiki? Kama wapo natumaini yupo ambaye atakupa kampani nzuri mpaka hapo
hali yako itakapokaa sawa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom