Nina swali kuhusu Elimu ya Secondari ya miaka miwili, nisaidieni majibu

Mtu Alie Nyikani

JF-Expert Member
Nov 9, 2022
714
1,527
Habari wakuu.

Natumai hali zenu zote ni nzuri. Kwa wale wenye changamoto, Mungu awajalie.

Nina swali kuhusu kusoma elimu ya sekondari kwa miaka miwili. Mfumo huu wa Elimu ya Secondary upo hivi yani katka mwaka Mmoja unasoma Madarasa mawili (form 1&2) and next year form 3&4 jumla miaka miwili.

Ningependa kuuliza vigezo vya kuipta hii Elimu vipoje, je pale ambapo mtu kama alifulu darasa la 7 lakini hakuendelea na Elimu ya Secondary anaruhusiwa kusoma hiyo Elimu ya miaka miwili?

Au kamaliza La 7 ila akahitaji kusoma hiyo Elimu ya Miaka miwili inaruhisiwa?

Na taratibu zake zipoje za Kuipata hiii Elimu.

Naombeni mnisaidie juu ya hili Wakuu.

Mbarikiwe kwa wale watakao toa maoni.
 
Elimu siyo miaka ya kukaa shuleni bali ni maarifa yanayopatikana shuleni
Upo sahihi kabisa.

Ila mimi nimeomba kupata mwongozo juu ya hilo la Miaka miwili ya secondary lipoje hasa Kwa wale wanaohitimu La 7, je wanaruhusiwa kuchukua Elimu ya aina hiyo?
 
Mkuu kwanini usifuate mfumo rasmi? Hii njia ni kama kuanza kuharibu maisha kabla ya kuyaanza
 
Hapana siwezi yaharibu. Ila umri sasa na Nina Imani kama hili lipo basi litaleta matokeo chanya.
Vipi Mkuu una uelewa wowote juu ya hiyo Elimu ya Miaka miwili?
 
Elimu ya sekondari kwa miaka 2, inatakiwa uwe na cheti cha la saba na baadaye unafanya mtihani unaitwa QT yaan qualifying test kwa mwaka wa kwanza yaan 1&2, then ukifaulu unafanya mtihani wa form four kama private candidate.
 
Elimu hii inafahamika kama QT (Qualifying Test)

Vigezo
Mtu yeyote aliyehitimu darasa la saba au chini ya hapo, Mimi nilisoma sikuulizwa cheti cha darasa la saba pia nilisoma na ambao hawakuwa wamehitimu darasa la saba.

Utaratibu wa Masomo
Mwaka wa kwanza:'
Utajifunza masomo yote tisa ya kidato cha kwanza na pili kisha utafanya mtihani wa QT ili uweze kuendelea na mwaka unaofuata kusoma Masomo ya kidato cha tatu na nne.

Mtihani wa QT unafanyika siku moja, na ni mtihani unaojumuisha Masomo yote tisa kwenye karatasi moja ila mtahiniwa atachagua masomo matano tu kati ya tisa Ndiyo atakayojibu.

Mtihani unavyofanyika
Mtihani unamasomo tisa na unafanyika ndani ya masaa matatu, English, Kiswahili, Civics, History, Geography, Mathematics, Chemistry, Biology, Physics

Kwenye mtihani huo Kiswahili, civics na English ni lazima kujibu. Kisha utachagua masomo mengine mawili yanayoendana ili kukamilisha masomo matano

Iko hivi so utachagua mwenyewe ufanye kundi lipi
-English, kiswahili,civics Geography na History

-English, Kiswahili, civics Chemistry na Biology

-English, kiswahili, civics Mathematics na Physics

Unahitaji maksi kama 50-60 kwa masomo matano uliyofanyia mtihani kufaulu.

Mwaka wa pili
Ukishafaulu mtihani wa QT utaendelea na masomo ya kidato cha tatu na nne kisha utafanya mtihani wa kidato cha nne.

Gharama
Niliposoma mimi walitoza 500,000 kwa mwaka na ada ya mtihani isiyozidi 50,000. Walikuwa na madarasa, walimu wa masomo yote, na nyenzo za kujifunza kwa vitendo kwa masomo ya sayansi.

NB; Mwaka wa kwanza ni rahisi sana, usipofaulu ni uzembe wako, ila mziki upo mwaka wa pili unaposoma Masomo ya kidato cha tatu na nne.
 
Hiyo kufanya mtihani wa form four si inabidi usome kwanza form 3&4 kwanza kwa mwaka mmoja au hii imekaaje Mkuu?
 
Mkuu habari nashukuru sana kwa Maelezo yako haya angalau nimepata mwanga.
Vipi Sasa kama mtu amefaulu hiyo QT kuendelea mbele atasoma masomo yote au atasoma Yale ambayo ameyafanyia mtihani?
Kingine pia hizo Marks 50 inabidi afikishe kwa Kila somo.au total ndo umechukulia.?

Maana Nina Dogo ndo nataka akapge hii Elimu kahitimu La Saba ana miaka 20 so naona hii Elimu itamfaa zaidi Ili kuendana na umri wake.
Nisaidie hapo na Ushauri wako n mhimu zaidi kiongoz
 
Ndyo maana ikaitwa elimu ya sekondari kwa miaka miwili, it means 1&2 mwaka mmoja, 3&4 mwaka mmoja pia. Huo mwaka unaosoma 3&4 ndyo mwaka huo huo utakaofanya mtihani wa kidato cha nne.
 
Mkuu habari nashukuru sana kwa Maelezo yako haya angalau nimepata mwanga.
Vipi Sasa kama mtu amefaulu hiyo QT kuendelea mbele atasoma masomo yote au atasoma Yale ambayo ameyafanyia mtihani?
Kingine pia hizo Marks 50 inabidi afikishe kwa Kila somo.au total ndo umechukulia.?

Maana Nina Dogo ndo nataka akapge hii Elimu kahitimu La Saba ana miaka 20 so naona hii Elimu itamfaa zaidi Ili kuendana na umri wake.
Nisaidie hapo na Ushauri wako n mhimu zaidi kiongoz
Kwa kuongezea hizo alama ni jumla siyo kwa kila somo. Kuhusu masomo kwa kidato cha 3&4 atasoma masomo ya kawaida kama wanavyosoma wengine.
Lkn nimesikia (sina uhakika) kuwa mtihani wa QT umefutwa badala yake watahiniwa watafanya mtihani wa kawaida wa form two maana yake ni kuwa mfumo wa QT uko palepale ila format ya mitihani ndo omebadiliswa badla ya kufanya paper moja kwa siku moja watafanya kama wanavyofanya form two.
Ngoja nifuatilie zaidi.
Unachopaswa kufanya nenda shule yyt ya private wenye hiyo huduma au any open school (tuition centres ) watakupa utaratibu mzuri na kipindi cha usajili ndiyo sasa hadi mwisho wa mwezi Machi(for late registration)
 
Kwa kuongezea hizo alama ni jumla siyo kwa kila somo. Kuhusu masomo kwa kidato cha 3&4 atasoma masomo ya kawaida kama wanavyosoma wengine.
Lkn nimesikia (sina uhakika) kuwa mtihani wa QT umefutwa badala yake watahiniwa watafanya mtihani wa kawaida wa form two maana yake ni kuwa mfumo wa QT uko palepale ila format ya mitihani ndo omebadiliswa badla ya kufanya paper moja kwa siku moja watafanya kama wanavyofanya form two.
Ngoja nifuatilie zaidi.
Unachopaswa kufanya nenda shule yyt ya private wenye hiyo huduma au anya open school (tuition centres ) watakupa utaratibu utaratibu mzuri na kipondi cha usajili ndiyo sasa hadi mwisho wa mwezi Machi(for late registration)
Ah, nashukuru sana Ubarikiwe ngoja nifuatilie
 
Mkuu habari nashukuru sana kwa Maelezo yako haya angalau nimepata mwanga.
Vipi Sasa kama mtu amefaulu hiyo QT kuendelea mbele atasoma masomo yote au atasoma Yale ambayo ameyafanyia mtihani?
Kingine pia hizo Marks 50 inabidi afikishe kwa Kila somo.au total ndo umechukulia.?

Maana Nina Dogo ndo nataka akapge hii Elimu kahitimu La Saba ana miaka 20 so naona hii Elimu itamfaa zaidi Ili kuendana na umri wake.
Nisaidie hapo na Ushauri wako n mhimu zaidi kiongoz
Ushauri wangu,

Sometimes ni ngumu kumaliza topic zote za kidato cha kwanza hadi cha nne ndani ya miaka miwili.

Msaidie apate,
-Tuition ambayo atajifunza na kupitia past papers. Huku hatusomi kuelewa tunasoma kujibu mtihani, akipitia mitihani ya kutosha atakuwa na ufanisi mzuri.

-Muda wa kutosha wa kusoma na kupumzika. Kama ana majukumu mengi nyumbani apunguziwe.

-Ufatiliaji wa karibu kuhakikisha anasoma nasio kurundika vitu, kwasababu ndani ya muda mfupi tu atakuwa amefundishwa mambo mengi, asipokuwa na utaratibu mzuri wa kupitia ataelemewa na mwisho wa siku asijue ashike lipi aache lipi.

-Kumtia moyo kwasababu kuna wakati masomo yatamuelemea. Hapa hakikisha anapata kuelewa umuhimu wa elimu unayompa na maisha yake ya badae, hii itamsaidia kuwa na msukumo wa ndani na kusoma kwa bidii.

-Zingatia umri wake ni umri wa mihemko na wazo la kusoma umelitoa wewe halijatoka akilini mwake hivyo basi usichoke kumvumilia na kuendelea kumuelimisha kuhusu elimu. Usije kudhani umelipa ada basi umemaliza.
 
Mkuu Ubarikiwe sana kwa Mawazo yako haya sikutarajia nitakutana na haya Mawazo, kwa hakika umenipa mwanga mkubwa naamini kupitia haya nitamsaidia Dogo pakubwa mno.

Again be blessed Mkuu.
Pia nitakufuata PM kama ikija kutokea shida basi utanishauri
 
Back
Top Bottom