Fumadilu Kalimanzila
JF-Expert Member
- Dec 10, 2016
- 1,651
- 5,126
Kuna msemo kwamba, " to every decision you make there is a price to pay or consequences"!Kwa kweli hata mimi🤣🤣🤣 cha ajabu zaidi walimu hao hao wa kata wnaapeleka watoto private yaani kama Nina uwezo siwezi peleka mwanangu kwenye huo upuuzi wa shule za serikali
Kwamba katika kila uamuzi ufanyao kuna gharama utakazolipa au athari zitakazo jitokeza.
Suala la elimu kwa watoto wetu hapa Tanzania linafanyiwa mzaha sana na wazazi walio wengi na hata viongozi wanatuongoza !
Kuna mjadala(thread) uliletwa humu na MwanaJF mwenzetu LIKUD kwamba yeye hawezi kutoa mamilioni kusomesha mtoto wake shule za English Medium!
Mjadala ni mkali na hasa ukizingatia Watanzania walio wengi wanavyopenda vitu vya bure, kasumba ya kijinga tuliyojengewa na mfumo wa ujamaa tulio anza nao kama Taifa baada ya kupata Uhuru!
Haya ni mawazo yangu niliyotoa katika mjadala huo unaendelea.
Elimu siyo kupata division one au kufaulu mitihani tu ! Ni zaidi ya hapo!
Elimu inatakiwa kumpa mtu maarifa ya kupambana na mazingira yake hata kuishi popote duniani.
Shule za m
Msingi na Secondary nyingi za Serikali ni kama VITUO VYA KUZUIA WATOTO wasilete vurugu mtaani wakati wenzao wanasoma!
Jiulize ni kwa nini hata Diwani , Wakuu wa vituo vya Polisi ,Walimu Wakuu wa Shule za Serikali n.k ,watoto wao wanasoma English Medium na hawataki kuwapekeka Watoto katika hizo Shule za Serikali !?
Wabunge na Mawaziri wanasomesha Watoto wao Feza Schools tena hawataki hata mtaala huu wa NECTA! wanasomesha Watoto wao kwa mtaala wa CAMBRIDGE ambapo ada kwa mtoto inafika au ni zaidi ya milioni 20 kwa mwaka!
Elimu ni kitu ghali sana lakini wapumbavu wengi kama wanadanganywa na wao wanakubali eti elimu ni bure!
Ukitaka kuona tofauti ya hizi elimu jaribu kukaa na Watoto wa hizi shule za Kayumba na English Medium uongee nao na kupima maarifa yao katika mambo mbalimbali uone!
Kuna tofauti kubwa mno!
Serikali imeficha aibu yake kwa kuanzisha mitihani ya majibu ya kuchagua (a,b,c,d)! Eti hata hisabati majibu ni ya kuchagua!
Hoja dhaifu wanayokupa eti kurahisisha usahishaji mitihani ,eti wanafunzi ni wengi.
Ushahidi wa upuuzi huo ni kukuta Wanafunzi waliofaulu darasa la Saba kutoka Shule za Serikali wakiwa Secondary huku hawajui Kusoma na Kuandika!
Hata sisi tunaojinyima na kusomesha Watoto wetu English Medium ukilinganisha na wanaosoma mtaala wa CAMBRIDGE kuna tofauti kubwa sana!
Kusomesha Kayumba kwa asilimia kubwa ni kuchagua kuandaa Washabiki wa Simba na Yanga na wapiga kura basi! wenzenu wanaandaa Global Citizens ( raia wa Dunia)!
Kuna Wazazi juzi kati hapa habari zinarushwa eti wanapigana na Walimu kwa kuchangishwa shilingi elfu mbili (2,000) katika hizi shule za Serikali!
Watu tutafute pesa kadri tunavyoweza tuwape Watoto wetu elimu ya maana na tuache kabisa huu upuuzi wa ELIMU BURE!
Ogopa sana kuandaliwa chakula na mtu ambaye yeye hataki kabisa kutumia chakula hicho!
Nionyeshe mtoto wa Waziri au Mbunge anayesoma shule za Kayumba nikuonyeshe udhaifu wa elimu ulioko katika Shule za Serikali!
Angalia matokeo ya kidato cha pili 2023 katika Shule ya Sekondari DIPLOMASIA tena iliyoko Dar es Salaam ! ni aibu! Watoto wanapata Division 4 na Ziro basi!
Angalia shule binafsi kama Feza, Marian, Kemibos,Musabe,Waja n.k.
Hizo shule walishavuka habari za kujadili Division one, wao wanahadili wangapi wamepata Division One za point 7!
Serikali inawadanganya Wazazi masikini na wapumbavu kwamba mtoto mwenye Division Four naye amefaulu!
Shule ya Sekondari kama DIPLOMASIA ina andaa Mama Lishe , Wauza Vocha (Dadapoa), Mashabiki wa Simba na Yanga na wapiga kura basi!
Mwenye maarifa ashtuke wakati wapumbavu wanadanganywa na upuuzi wa ELIMU BURE!