Nina sebule ina urefu wa 6m na upana wa 4m, je, ninunue TV (screen) ya nchi ngapi na brand gani ni nzuri?

Mshua's

JF-Expert Member
May 22, 2013
801
546
Habari wakuu?

Nimehamia kwenye nyumba ambayo ina sebule yenye vipimo kama nilivyoainisha hapo juu (Ur 6m kwa Up 4m). Naomba ushauri ninunue flat screen ya nchi ngapi na brand gani ina quality nzuri za picha na inadumu kwa muda mrefu bila kuleta matatizo?

Natanguliza shukran za dhati wakuu!
 
Nunua ya uwezo wako mkuu.!
Labda ungetuweka wazi una bajeti kiasi gani ya TV angalau tungetoa mawazo.
Kama ni ushauri wa brand basi kamata LG
 
Nitaiuza! Nahamia kwenye nyumba yangu. Nataka niweke vitu vyenye ubora, sihofii kupandishiwa bei ya pango hata kama nikiweka vitu vyenye ubora!
"uhofii kupandishiwa kodi ya pango hata ukiweka vitu vyenye ubora".
mkuu endelea kupanga acha mbwembwe
wenye nyumba hatuna akili hizo uweze kujenga nyumba halafu uje jf uulize eti ununue tv ya ukubwa gani?
seriously kabisa?
 
Mkuu kwa sebule yako tv isipungue inchi 43" so inatakiwa inchi 43 na kuendelea mana sebule ya 6x4m ni kubwa iisee.
Kuhusu Brand nzuri yenye picha very quality na isiyopungua with time nunua
1.Sony
2. Samsung
3.LG
kwa hizi brand za kawaida nunua TCL kidogo ukashindwa kabisa nunua HISENCE inajitahidi sio mbaya.
Ultra HD, 4k TV picture quality zina ubora wa hali ya juu sanaa.

ila kwa bajeti yako nadhani itabidi ununue brand za quality ya kawaida hizo tatu zipo juu kidogo mkuu ila ukinunua utaenjoy sana aisee
 
afu ukiwa unanua TV mkuu make sure quality ya picha inakua sawa kila pande unayokaa kuitazama. maana kuna TV siku izi zina vioo fake ukikaa pembeni unaona watu kama wanafifia au kama zile negative kwenye camera za kizamani au mara watu kama watu wameungua daah
 
USINUNUE TV YA 4K. WASTAGE. ISHIA FHD UNLESS UNA PS4 PRO AU 5 NA UNACHEKI MOVIE ZA 4K ILA KM NI KING'AMUZI ONLY 1080P
afu mkuu mimi naona TV nyingi tunauziwa ni FHD hizi 4k wanaandika kwenye maboksi tu kuipamba unless zile za OLED TVs zile kweli zina 4k hadi 8k
 
Mkuu kwa sebule yako tv isipungue inchi 43" so inatakiwa inchi 43 na kuendelea mana sebule ya 6x4m ni kubwa iisee.
Kuhusu Brand nzuri yenye picha very quality na isiyopungua with time nunua
1.Sony
2. Samsung
3.LG
kwa hizi brand za kawaida nunua TCL kidogo ukashindwa kabisa nunua HISENCE inajitahidi sio mbaya.
Ultra HD, 4k TV picture quality zina ubora wa hali ya juu sanaa.

ila kwa bajeti yako nadhani itabidi ununue brand za quality ya kawaida hizo tatu zipo juu kidogo mkuu ila ukinunua utaenjoy sana aisee
Mkuu nashukuru kwa ushauri. Huwa napenda kununua vitu vyenye ubora. Nitaongezea kidogo bajeti yangu ili nichukue kati ya Sony au LG. Naona LG pia watu wengi wameshauri. Vitu vya Sony pia nina uzoefu navyo. Niliwahi kununua radio flani ya cd plate tatu kitambo sana mziki wake ni mzuri kuliko wa subwoofer. Hizi brand za kichina huwa siziaamini sana!
 
Back
Top Bottom