Nina miaka zaidi ya 30 sina ninachomiliki, nahisi kukata tamaa. Msaada wenu

Naombeni msaada wenu wakuu ambao waliokwisha pitia hali kama hii ninayopitia mimi. Nina miaka 30 na kitu, sina ninachomiliki zaidi ya godoro langu, radio ndogo ya muziki, vyombo vya udongo ndani ya beseni pamoja na nguo zangu.

Nahisi kukata tamaa kabisa na haya maisha. Mliokwisha pitia hali kama hii yangu kwenye umri huu na ukawa kwenye maisha kama haya, ilikuwaje? Naombeni mnisaidie kimawazo.

Kuna muda natamani hata corona ije upande wangu, nahisi kukata tamaa kabisa.

Sina kazi, sina kibarua kabisa. Maisha yamekuwa magumu sana upande wangu.

Karibuni kwa mawazo yenu, wakuu.
Ipo siku utapata kazi mradi usichague nzuri na mbaya, duniani hakuna kazi mbaya, hebu tuanze na utopasi, fikiria matopasi wote wache kazi hiyo, nyumba zote hazitakalika, ukisikia nyumba fulani nzuri sana ujue kunatopasi anaisafisha na yeye anapata mshahara wa kuendesha maisha. Kuna siku bahati itakuangukia utapata umeneja mshahara mnono sana, utaona umefika na utaanza maisha ya anasa na kujisahau, yarabi! Asubuhi unafika kazini na tai yako shingoni unakuta barua ya kufukuzwa kazi! Mshituko, ulipanda na umeshuka ghafla na unaanza kuchanganyikiwa kwani ulipokuwa meneja kila kitu cha nyumbani kilikuwa cha mwajiri nyumba pamoja na gari, sasa hauna gari na hauna godoro wala sahani! Ni wewe na tai yako shingoni.
Ninakusihi usichague kazi amini Mungu utapanda Polepole jinsi siku ziendavyo huku ukisahau starehe kwanza na ikiwa na rafiki mwenye uelekeo has a mwanamke atakayeweza kukudhibiti bila yeye kujinufaisha, siyo kila mwanamke ni mbaya wapo waliopigika kimaisha na hawataki yakawarudia waliyopitia.
Usife moto utafanikiwa ila jitahidi mradi angalia hitaji mkubwa mtaani kwako kwa ni maji tafuta madumu uuze maji.
 
Naombeni msaada wenu wakuu ambao waliokwisha pitia hali kama hii ninayopitia mimi. Nina miaka 30 na kitu, sina ninachomiliki zaidi ya godoro langu, radio ndogo ya muziki, vyombo vya udongo ndani ya beseni pamoja na nguo zangu.

Nahisi kukata tamaa kabisa na haya maisha. Mliokwisha pitia hali kama hii yangu kwenye umri huu na ukawa kwenye maisha kama haya, ilikuwaje? Naombeni mnisaidie kimawazo.

Kuna muda natamani hata corona ije upande wangu, nahisi kukata tamaa kabisa.

Sina kazi, sina kibarua kabisa. Maisha yamekuwa magumu sana upande wangu.

Karibuni kwa mawazo yenu, wakuu.
wenzio kwa age ya 23 tulianza kumiliki kiwanja Dar es salaam, kufikia 27 tulinunuwa magari, sio kwamba ninajisifu, maisha ni yako mwenyewe, hakuna mtu atakuja kukuletea kapu la mafanikio, heshimu fedha iwe ndogo au kubwa, matumizi sahihi, maamuzi sahihi, mademu pembeni kwanza, jitume jibidishe, hakuna miujiza katika mafanikio ni juhudi tu! na kumuomba Mungu!
 
Haupo pekee yako bro maisha ndivyo yalivyo yanagawa hisani kwa muda yanaoutaka yenyewe kimsingi ni kuwa imara na kubadili mtazamo wa kusema mm ni wa hivihivi tu maisha yote.
Kwanza jiamini kuwa unaweza kufanya lolote muda wowote hata kama kitachelewa ukitakacho mimi babu yangu nimeshuhudia anajenga nyumba ya ndoto yake late sana akiwa na miaka zaidi ya 60 kanunua na gari juu halafu sio msomi wala mfanyakazi anategemea pensheni.
Jitambue uwezo wa ulipo wa kufanya unachoweza ili kukuingizia kipato hata ni kwakiwango cha chini sana.
Panga mipango yako vizuri na uizingatie kwa wakati muafaka...
Nakuhakikishia ukifuata haya utaishi maisha uyatakayo bro jitahidi kutokata tamaa muda wote..
Mtangulize Mungu pia kwa kutambua uwepo wake maishani mwako sidhani kama kakuacha hivyo ....
Big up u'll.made it.. usisahau kusmile hata kama hujala smile ty
 
Bado una nafasi ya kupambana,umri unakuruhusu kufanya mambo makubwa tu mbeleni. Wapo vijana wengi tu wa umri kama wako tena wenye ajira zao lakini bado hawajafanya chochote mpaka sasa. Panga mipango yako na uwe mwaminifu kwako mwenyewe,kidogo unachokipata kitumie vizuri,kadiri utakavyokuwa na nidhamu ya kutumia pesa kidogo unayopata ndivyo utakavyoyaona mafanikio zaidi. Pambana Mkuu
 
Hahahah hii kitu inapoteza vijana wengi sana mkuu, katika maisha yangu sikuwahi kuwaza ipo siku ntakaanga kitimoto na kuwafungulia watu bia. Ila ilifikia stage nikaona i have to do something for my self-development.

Maisha yatatukaza always cha msingi ni kubadilisha style tu ya kupigwa mashine ili usiumie sana ila kukazwa kupo pale pale.
Heineken bei gan bar kwako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
A
Naombeni msaada wenu wakuu ambao waliokwisha pitia hali kama hii ninayopitia mimi. Nina miaka 30 na kitu, sina ninachomiliki zaidi ya godoro langu, radio ndogo ya muziki, vyombo vya udongo ndani ya beseni pamoja na nguo zangu.

Nahisi kukata tamaa kabisa na haya maisha. Mliokwisha pitia hali kama hii yangu kwenye umri huu na ukawa kwenye maisha kama haya, ilikuwaje? Naombeni mnisaidie kimawazo.

Kuna muda natamani hata corona ije upande wangu, nahisi kukata tamaa kabisa.

Sina kazi, sina kibarua kabisa. Maisha yamekuwa magumu sana upande wangu.

Karibuni kwa mawazo yenu, wakuu.
Angalau wwe unamiliki hata godoro na radio kumbuka wengi tz Hadi wanakufa hawana uwezo wa kumiliki hata hivo.
Anza kushukuru kwa vidogo ili upewe vikubwa
 
Back
Top Bottom