Nina miaka zaidi ya 30 sina ninachomiliki, nahisi kukata tamaa. Msaada wenu

mkuu pole... Kwamza tambua haupo pekeako, wengine katika hali kama yako wapo na familia pia but life inasonga kikubwa pumzi ... Chakufanya kila siku amka asubuhi na mapema mshukuru Mungu, kisha fanyia usafi chumba chako na mazingira ya hapo nje, kisha washa moto na uchemshe maji nenda oga baada ya kuweka mwili safi chukua maji kunywa then mshukuru MUNGU halafu nenda katembee mtaani.
 
Sasa umeamua nini mkuu?
Je? ulikuwa na plans zozote kabla ya kufika hapo ulipo?
Miaka 5 iliyopita ulikuwa na mipango gani?,

Muda ni rafiki mbaya sana haswa usipoutumia vizuri, muda haujari kuhusu wewe bali utaendelea kusonga mbele, ila wewe ndiye unayetakiwa kuujari muda la sivyo utakuacha na kuja kushtuka baadae sana,

Mimi siamini kama kuna Kuna kitu kinaitwa bahati nzuri Wala bahati mbaya, bali naamini katika mipango ya muda mrefu au mfupi, ukisubiria bahati inaweza isije leo wala kesho na muda haukusubiri.
kabla sijafanya chochote kile haijarishi ni goals au kutatua matatizo,
kwanza huwa napanga/kupiga hesabu za kila kitu kwa umakini kama muigizaji wa kwenye movie, pia napanga njia za kutokea kama mambo yakienda sivyo,
baada ya hapo ndio nafanya hicho nilichopanga (hakuna kukurupuka)na kama sitotoka nje ya niliyoyapanga lazima nifanikiwe, haijarishi ni mipango mifupi au mirefu.

Sasa ndugu kwenye maisha unatakiwa upange kila kitu kuendana na muda au muda utakuacha, na kwenye hiyo mipango uliyopanga Ili ufanikiwe hutakiwi kukiuka hata nukta na lazima ufike.

Anza sasa hakuna kuchelewa katika maisha, tumia muda wako kutafuta solutions na sio kufikiria matatizo, alafu wewe si ni mtoto wa kiume? na una afya?, jiamini na pambana mpaka nukta ya mwisho hakuna kurudi nyuma hakuna kulia,lia wala hakuna kukata tamaa, pambana mpaka uhakikishe mungu amekuita mwenyewe, sio umfuate wewe.

Kumbuka hakuna kitu rahisi katika maisha, anza sasa baada ya miaka10 njoo ulete mrejesho.
 
Naombeni msaada wenu wakuu ambao waliokwisha pitia hali kama hii ninayopitia mimi. Nina miaka 30 na kitu, sina ninachomiliki zaidi ya godoro langu, radio ndogo ya muziki, vyombo vya udongo ndani ya beseni pamoja na nguo zangu.

Nahisi kukata tamaa kabisa na haya maisha. Mliokwisha pitia hali kama hii yangu kwenye umri huu na ukawa kwenye maisha kama haya, ilikuwaje? Naombeni mnisaidie kimawazo.

Kuna muda natamani hata corona ije upande wangu, nahisi kukata tamaa kabisa.

Sina kazi, sina kibarua kabisa. Maisha yamekuwa magumu sana upande wangu.

Karibuni kwa mawazo yenu, wakuu.
Mkuu omba uzima,usikate tamaa tena unaweza wewe ukaja kucheka kwenye fainali uzee kuliko hawa ambao sasa wanashika maburunguta ambayo yanaishia kwenye misambwanda na baadae wanakuwa alosto,hata Piere Liquid alikuwa hajui yajayo mkuu,tafadhali omba tu corona ikupitia mbali huo umri bado sana
 
Pole sana kaka. Lakin nirudie kama walivyosema watangulizi kwanza- usikate tamaa hata nukta moja. Pili -endelea kumuomba mungu. Sisi waislam tuna sema INALLAH MAA SWABIRIIN...!! Hakika ya mungu yu pamoja na wenye kusubir. Ila tatu -anzia hapo ulipo fanya kazi kwa bidii jichanganye na watu tofaut tofaut ili walau upate proper connection. Then am sure utatoboa tu inshallah..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaonesha wazi we ni tegemezi (kifikra na hata ki uchumi) , we ni mvivu wakufikilia, we ni mvivu wakufanya kazi pia mfumo wako wa maisha ni wakulalamika, kulaumu na kutoa visingizio.

Hainingii akilini upo Jf afu unasema huna kazi wala kibarua kwamba una miliki smartphone afu umekosa mtaji wa kuuza hata Balakoa.?

Mwanaume kamili huwa halamiki yanapomkuta magumu ila huwaza solution zaidi. Kaa tafakari unataka Nini na ufanye nini ili upate unachokitaka usipende kuonewa huruma tupo kwenye ulimwengu ambao huwezi fanikisha chochote mpaka upigane vita

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom