Nina miaka zaidi ya 30 sina ninachomiliki, nahisi kukata tamaa. Msaada wenu

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
889
1,000
Naombeni msaada wenu wakuu ambao waliokwisha pitia hali kama hii ninayopitia mimi. Nina miaka 30 na kitu, sina ninachomiliki zaidi ya godoro langu, radio ndogo ya muziki, vyombo vya udongo ndani ya beseni pamoja na nguo zangu.

Nahisi kukata tamaa kabisa na haya maisha. Mliokwisha pitia hali kama hii yangu kwenye umri huu na ukawa kwenye maisha kama haya, ilikuwaje? Naombeni mnisaidie kimawazo.

Kuna muda natamani hata corona ije upande wangu, nahisi kukata tamaa kabisa.

Sina kazi, sina kibarua kabisa. Maisha yamekuwa magumu sana upande wangu.

Karibuni kwa mawazo yenu, wakuu.
 

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
21,444
2,000
Pole Sana Kwa Changamoto

Kwasasa Unaweza Kufikiria Upo Pekee Yako. Ukweli Kuna Idadi Kubwa Sana Ya Watu Ambao Hawajapata Uelekeo. Kubwa Sana Usikate Tamaa.

Kuna Mtu Mmoja Mwaka Jana Alifikia Hatua Kama Yako Yaani Afe! Mungu Ni Mwema Wakati Wote.

Nilimsihi Avute Subira, Tatizo Lake Tulipoweza Kulitatua Mwaka Huu Oops, Maneno Aliyosema Kwa Waliomsaidia Aibu.

Kwanza Kawa Mtata, Uzuri Waliomsaidia Wameamua Kumwacha Aendelee Mbele Mwenyewe.
 

Intl inc

Member
May 12, 2020
9
45
Aaaaaahhhh acha utani bhana mbona unataka kuchekesha msiban father 14 years anamiliki simu na redio mpaka sas tena ana kadem pembeni sasa wewe au umeibiwa/ umepoteza?

But usikate tamaa endelea kupambana labda ndvyo ulivyoandkiw na Muumba
 

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
10,341
2,000
Wengi tumepitia huko mkuu,mpaka 40 bado huoni hata mwanga na unaona kabisa miaka 60 unaikaribia, usiogope, mtangaulize Mungu wako katika kila njia unayoipitia atakupa ujasiri.Utakuwa huna hofu na moyo wako utakuwa na Amani, kumbuka popote penye nia hapakosi njia,usikate tamaa ya kutafuta, hiyo ndio sumu pekee itakayokufanya usifanikiwe maisha yako yote....
 

0ozg Tz

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
577
1,000
Bora wew una godoro na vyombo,mim nna 30 yrs sina chochote zaid ya shuka na simu navyo nilvipata kwa pesa ya wazazi ni kwel kama unavyosema huwa nataman hata kufa tu.

Naishi na kutembea kwa pesa za baba ,afu unakuta kuna binti ananing'ang'ania nimuoe wakat sjaweza kusaka pesa zang mwenyewe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom