Nimetafuta kazi mpaka nimechoka najiona sina faida hapa duniani

Superleta

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
466
538
Naombeni mnisaidie nipate kazi ndugu zangu labda humu jukwaani nitapata msaada

Nimehitimu mwaka 2022 Degree ya maendeleo ya jamii

Nina diploma pia ya maendeleo ya jamii. Nina certificate pia ya maendeleo ya jamii

Nimehangaika sana suala la kazi hadi nimejikatia tamaa nimekua ni mtu wa kushinda geto tu na nimekua nikijikatia tamaa tu

Baada ya kumaliza form 4 wazazi wangu walichangachanga wakanipeleka chuo wakanisomesha kwa shida na dhiki sana hadi nikahitimu diploma. Nilipomaliza diploma tu nikakaa nyumbani kama mwaka nikihangaikia masuala ya kazi kama mwaka huku nikijishughulisha na shughuli ndogondogo ujasiriamali na ufugaji mambo hayakwenda nilivyotarajia nikaenda kujiendeleza kusoma degree

Degree nilipata mkopo ila asilimia 40 tu hapo safari yangu ya kuanza kujitegemea na kujibana ilianza zaidi, ilinibidi sasa nipambane niweze kujilipia ada kodi na kila kitu nimejipambania mwenyewe miaka 3 nasoma huku napiga mishe za hapa na pale mpaka nimehitimu shahada yangu ya maendeleo ya jamii.

Sikurudi nyumbani nikaona niendelee kukomaa tu na kitaa huku nikisaka ajira, na mishe za hapa na pale. Nimehangaika na mishezangu sasahivi mambo yangu yamekua magumu sana, mishe zimebuma, nimehangaika na suala la kazi mpaka nimechoka

Huko kwenye mashirika nimeenda sana nimeaply sana lakini wapiWenzangu kadhaa tulomaliza nao walishapata kazi kitamboo na sahivi wanaishi maisha yao mazuri tu mimi najiona kama mkosi tu na nisiye na faida nyumbani hawaelewi kabisa wanaona kama nawatania nikiwaambia sina kazi.

Sasahiv napitia msongo mkali sana wa mawazo umri unasogea sina mbele wala nyumanajuta kuzaliwa, najuta kuishi najiona sina thamani kabisa, nimekua ni mtu wa kujifungia ndani na kulia tu.

Sasa hivi nyumbani na ndugu jamaa maswali mengi kila mara utaulizwa kwamba hujapata kazi tu?Kwanini hadi sasa hujapata kazi?Baba yangu ni mzee yupo 70+ mama nae yupo 60+ nilitakiwa sahivi niwe nawasaidia sio umri wao wa kuanza kuhangaika kubangaiza roho inaniuma sana najiona sina maana tena kwao najiona kama siwatendei wazazi wangu.

Kweli kazi sikuhizi bila connection mtu hutoboi!! Ananijua nani mimi? Wenzangu mnaopata kazi mnafanyaje mbona kila kitu natimiza lakini sipati?Hali nayopitia sahv ni ngumu ni ngumu mno, naombeni yoyote anayejua hata shirika lolote nikajitolee tu nipo tayar kwa hapa Dar. Mimi nipate tu walau kazi ya kujitolea tu ilimradi niwe bize nishachoka kukaa mtaani.

Mimi nipo tayari hata mtu anitafutie kazi shirika au mahali popote nipo tayari hata mshahara wangu wa mwanzo achukue yeye tu kama malipo ya kunitafutia kazi.

Wenzangu wengi tulomaliza nao wana kazi muda wengine tokea diploma huko walipata kazi wana maisha mazuri kila kitu mimi sina chochote cha maana hapa duniani sazingine naona bora ningekufa tu siku nilizaliwa wapo hadi wanaonicheka wakiona nilikua najifanya napenda sana ndo maana nilijiendeleza zaidi kielimu

Nisaidieni ndugu zangu nipate kazi popote hata kujitolea nipo tayari

UPDATES:Nimeombwa niweke namba yangu hapa namba yangu ni 0624 088 380 ipo watssap pia
 
Pole mkuu, unataka kazi za kiyoyozi??
Kama jibu ni ndio basi kweli utalia sana hapo geto...

Viwandani kuza kazi, kama upo Dar viwanda ni vingi, nyuzi nyingi humu wanaelezea viwanda unavyoweza kupata job.

Upo Dar sio, kule Mabibo ni nguvu zako tu, kama una hulka ya uongeaji jichanganye na wale washusha ndizi, viazi, matunza aloo wale jamaa wanakunja hadi 30k per day, ni nguvu zako na uaminifu.

Kama sio mlemavu, una afya njema basi huo ndo mtaji wako, acha kulialia hapo geto, kufa njaa dar hii ni uzembe wa hali ya juu.
 
Ukishaanza kuwaza kama kichwa Cha habari kinavyosema, basi ni ngumu sana kutoka kwenye huo msoto.

Kwenye haya maisha ili utie huruma, inabidi uwe na uhakika wa uwepo wa watu watakaokuonea huruma, kinyume na hapo tujitahidi kukaza tu.
 
Umeliandika neno "degree" mara nyingi saana,... Sasa ukitembea na hiyo degree utachelewa sana,.. Badilisha fikra ya kutafuta kazi,.. Sasa hivi tafuta pesa! Ukikubali kutafuta pesa, hiyo degree iweke pembeni kwa muda. Kitachotafutwa ni pesa na sio kazi ndg yangu
 
Sasahiv napitia msongo mkali sana wa mawazo umri unasogea sina mbele wala nyuma
emoji22.png
najuta kuzaliwa, najuta kuishi najiona sina thamani kabisa, nimekua ni mtu wa kujifungia ndani na kulia tu
Huo muda unaomalizia kwenye kulia, ushaomba ata intern?
 
Naombeni mnisaidie nipate kazi ndugu zangu labda humu jukwaani nitapata msaada
Nimehitimu mwaka 2022 Degree ya maendeleo ya jamii
Nina diploma pia ya maendeleo ya jamii
Nina certificate pia ya maendeleo ya jamii

Nimehangaika sana suala la kazi hadi nimejikatia tamaa nimekua ni mtu wa kushinda geto tu na nimekua nikijikatia tamaa tu

Baada ya kumaliza form 4 wazazi wangu walichangachanga wakanipeleka chuo wakanisomesha kwa shida na dhiki sana hadi nikahitimu diploma.Nilipomaliza diploma tu nikakaa nyumbani kama mwaka nikihangaikia masuala ya kazi kama mwaka huku nikijishughulisha na shughuli ndogondogo ujasiriamali na ufugaji mambo hayakwenda nilivyotarajia nikaenda kujiendeleza kusoma degree

Degree nilipata mkopo ila asilimia 40 tu hapo safari yangu ya kuanza kujitegemea na kujibana ilianza zaidi, ilinibidi sasa nipambane niweze kujilipia ada kodi na kila kitu nimejipambania mwenyewe miaka 3 nasoma huku napiga mishe za hapa na pale mpaka nimehitimu shahada yangu ya maendeleo ya jamii.

Sikurudi nyumbani nikaona niendelee kukomaa tu na kitaa huku nikisaka ajira, na mishe za hapa na pale.Nimehangaika na mishezangu sasahivi mambo yangu yamekua magumu sana, mishe zimebuma, nimehangaika na suala la kazi mpaka nimechoka

Huko kwenye mashirika nimeenda sana nimeaply sana lakini wapiWenzangu kadhaa tulomaliza nao walishapata kazi kitamboo na sahivi wanaishi maisha yao mazuri tu mimi najiona kama mkosi tu na nisiye na faida nyumbani hawaelewi kabisa wanaona kama nawatania nikiwaambia sina kazi.

Sasahiv napitia msongo mkali sana wa mawazo umri unasogea sina mbele wala nyumanajuta kuzaliwa, najuta kuishi najiona sina thamani kabisa, nimekua ni mtu wa kujifungia ndani na kulia tu.

Sasa hivi nyumbani na ndugu jamaa maswali mengi kila mara utaulizwa kwamba hujapata kazi tu?Kwanini hadi sasa hujapata kazi?Baba yangu ni mzee yupo 70+ mama nae yupo 60+ nilitakiwa sahivi niwe nawasaidia sio umri wao wa kuanza kuhangaika kubangaiza roho inaniuma sana najiona sina maana tena kwao najiona kama siwatendei wazazi wangu.

Kweli kazi sikuhizi bila connection mtu hutoboi!! Ananijua nani mimi? Wenzangu mnaopata kazi mnafanyaje mbona kila kitu natimiza lakini sipati?Hali nayopitia sahv ni ngumu ni ngumu mno, naombeni yoyote anayejua hata shirika lolote nikajitolee tu nipo tayar kwa hapa Dar.Mimi nipate tu walau kazi ya kujitolea tu ilimradi niwe bize nishachoka kukaa mtaani.

Mimi nipo tayari hata mtu anitafutie kazi shirika au mahali popote nipo tayari hata mshahara wangu wa mwanzo achukue yeye tu kama malipo ya kunitafutia kazi.

Wenzangu wengi tulomaliza nao wana kazi muda wengine tokea diploma huko walipata kazi wana maisha mazuri kila kitu mimi sina chochote cha maana hapa duniani sazingine naona bora ningekufa tu siku nilizaliwa wapo hadi wanaonicheka wakiona nilikua najifanya napenda sana ndo maana nilijiendeleza zaidi kielimu

Nisaidieni ndugu zangu nipate kazi popote hata kujitolea nipo tayari
Kinachokuponza ni kampani yako hakuna watu wa maana anza kujipendekeza kwa wazee wazee hawa hata kama hawana kazi wanaconnection basi tu..
 
Kuna kitu kinaitwa trainee Zanzibar. Unapiga miezi 3 unapata cheti na possibility ya kazi ipoo. Mwez wa 6 kunafurika utalii sana Zanzibar hivyo makampuni yanaongeza scope ya operation.

Unaweza kusomea house keeping, barman, chef, front desk miezi 3 tu. Ada Yao ni 150 lakin pia wanalipaga kila mwez. Fikiria katika muktadha huu ili usijionyonge. Dar ngum sana..

Kwa kada hizo mishahra Yao inarange 300-500 kuntegemea na standard za kampuni
 
Toka hayo mazingira nenda sehem nyingine hapo tyr umejenga toxic reality, nenda hata Kwa ndugu mnae elewana then Anza upya. Anza hata biashara au kilimo Kwa mwaka mmoja then utanipa matokeo. Ajira now Ngum Kwa wote hauko peke ako.
 
Kama utabadlisha mtazamo wako kuhusu MAISHA basi utafanikiwa kutoka katika huo mkwamo.

Umeruhusu nguvu hasi kubwa Sana kuliko nguvu chanya.

Soma Kitabu cha "Become better you" by Joel osteen I promise hiyo hali itapotea haraka Sana.

Una negativity Sana .

MAISHA ni kuinuliwa na sio kupanda na ili uinuliwe unabidi kuwa MTU wa kushukuru kwa kila jambo na sio kulalamika .

Ukijfunza kushukuru MAISHA yatabadiika Sana .

Kuwa positive
Bealive in G O D
Stay greatful
 
Back
Top Bottom