Msaada: Nina tatizo la kuwa na mawazo ya kufanya vitendo vya kikatili

baharia 1

JF-Expert Member
Sep 13, 2019
1,255
1,268
Habari wakuu,

Nina tatizo, tatizo langu kubwa, stori fupi.

Naweza kukaa sehemu na watu mara ghafla akili inakuja nifanye kitu kibaya, na nikiona silaha pembeni akili ndio inahama kabisa. Natamani nitumie hiyo silaha nifanye mauaji kama kisu, panga, nahiyo sehemu kwa hofu huwa naondoka. Akili inanisukuma nifanye vitu vya ovyo, kama mauaji na vitu vingi.

Hata nikiwa barabarani, natamani niingize gari nipate ajali, tugongane na mtu uso kwa uso.

Ila hii hali ilikata miaka miwili iliyopita nyuma, baada ya kutoa uzi hapa JF nikielezea hilo. Nilipata comment nyingi mno, ila mtu aliniambia nitumie dawa fulani, na kweli nilitumia. Hali ile ikakata kabisa, ila sasa naiona inarudi kwa kasi sana. Muda wowote naweza kufanya jambo baya sana kwa jamii.

Ile ID yangu ya mwanzo nimepoteza. Sasa sina njia nyingine, naomba msaada wenu. Naogopa kukaa na watu karibu.

Naombeni msaada wenu wa madaktari. Muda unakuja, nitafanya ya ajabu.

Asanten.
 
Kwanza pole. Lakini vipi hakuna stimu yoyote unatumia? Hapa stimu imetumika kama kilevi, kama ndio acha hiyo kitu.

Ushauri wangu jikabidhishe kwa Mungu kwa hali uliyo fikia sioni haja ya kuwa mbishi wakati mungu anakutaka mtete.

Tafuta madhabau yeyote onana na huyu mkuu wa vyote ulimwenguni ,anaitwa Mungu mwenye nguvu, atamaliza ako katatizo unaweza zani ni tatizo kubwa ila kwake ni dogo sana. Usichelewe... usichelewe... kufanya hili.

Kila kheri kaka
 
Mawazo ni matokeo ya kile ambayo umelisha akili yako. Au kwamaana nyingine ni kila yajazwayo ndio yamwagikayo. Lakini pia waweza kuiondoa hali hii kama ukiamua kuilisha akili yako yale mambo mazuri uyatakayo.

Akilii yako waweza ituliza wewe mwenyewe na kuondoa kila aina ya mawazo yanayokujia....

Jaribu kufanya meditation au ingia YouTube na usikilize hizi binaural beats za mind relaxation...

Uje na marejesho
 
Nenda kwa Yesu kaka akuponye
Yesu anakupeda sna my friend nakuombea sana Mungu akupe Neema
Kila lililobaya lisitokee Kwa Jina la Yesu Kristo
Amen
Alafu watu km nyinyi ndio mmefanya waisrael wamkatae Yesu na wafikirie kufunga SHERIA ya kumfunga mtu yeyote jela mtu ambae anaeleta story za Yesu wa kwenye kitabu kwenye maisha halisi.
 
Kwanza pole . Lakin vp hakuna stimu yoyote unatumia ?? Apa stimu imetumika kama kilevi , kama ndio acha iyo kitu . Ushauri wangu jikabidhishe kwa Mungu kwa hali uliyo fikia sioni haja ya kuwa mbishi wakati mungu anakutaka mtete. Tafuta madhabau yeyote onana na huyu mkuu wa vyote ulimwenguni ,anaitwa Mungu mwenye nguvu ,atamaliza ako katatizo unaweza zani ni tatizo kubwa ila kwake ni dogo sana . Usichelewe..usichelewe..kufanya hili. Kila kheri kaka
Wewe huyu tatizo lake sio ibada huyu tatizo lake ni akili yake Ina vitu Sasa ni vitu gani anahitaji diagnosis ya mda na mtaalamu wa tiba ya akili sio tiba ya sadaka jaribu kuelewa walau kidogo angalia namna nyingine ya kumsaidia lakini sio kumwambia akimbilie kwa manabii utamponza
 
Wewe huyu tatizo lake sio ibada huyu tatizo lake ni akili yake Ina vitu Sasa ni vitu gani anahitaji diagnosis ya mda na mtaalamu wa tiba ya akili sio tiba ya sadaka jaribu kuelewa walau kidogo angalia namna nyingine ya kumsaidia lakini sio kumwambia akimbilie kwa manabii utamponza
Tatizo lake halijaanza Leo kakwambia alisha leta Uzi ,uyo Dr alisha pita Uko ,mpaka dawa alipewa ,sasa ukiona mambo yanajirudia suruhisho siku zote nimaombi na sijamtuma aende kwa manabii nimemwambia atafute madhabahu,inaweza kuwa sehemu yeyote ambapo ataweza kutana na Mungu wake. Period
 
Pole rafiki. Kwa kua umeomba ushauri na mimi nakupa ushauri wangu kama ifuatavyo:

1. Mambo yote yanayoonekana ki mwili, Chanzo chake ni Rohoni. Hivyo rekebisha kwanza mambo ya Rohoni kulingana na imani yako. Ingawa mimi ningekushauri kumtafuta Yesu.

2. Ukija kimwili sasa, tafuta Mtaalam wa kitabibu haraka apate kukusaidia.
 
Back
Top Bottom