Nina mashaka na Bwana Inayat Kassam wa Kenya

Nina mashaka na Bwana Inayat Kassam wa Kenya

Shida alivyomalizia utaelewa tu kuwa ni mtu mwenye religious sentimetals sana
Wewe ndiye hujamwelewa rudi tena kusoma, au hukuona alama ya kuuliza pale. Si kauliza

Mtu kamfafanulia mtoa post kumtoa shaka kisha akamuuliza kama shaka yake ni kuhusu dini, maana Uislamu huandamwa pia na matukio hayo.

Umeshambulia bure
 
Je jamaa alifika kabla ya Vyombo vya usalama???? Au unatumia hisia zako kusema alifika haraka eneo la tukio?? Unajua alifika muda gani baada ya tukio kutokea???
Jamaa anafanya mafunzo ya ishu za usalamaa so Sioni shida hapoo yeye kujumuika na hiyo timu ya Uokozi... Huwezi jua uwepo wake uliokoa roho ngapi zaidi labda alisaidia kuokoa wengine ambao kimsingi ilibdi wafe.. Hii attitude ya wabongo kutokuwa na imani na watu ndo inafanya hata watu wenye roho nzuri washindwe kusaidia watu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siwezi kushangaa watanzania wengi umbea mbele lakini hawajijui kama ni umbea wao hudhani ni ugenius... Wahanga wasihoji hayo sie ndio tuhoji.
lol.

Be crazy, Be Weird, Be whatever coz life is too short to be anything but HAPPY.
 
Unafikiri kuna asiye Muislam anaweza jitolea maisha yake kuokoa watu namna hiyo? Wakati watu wanakimbia tukio yeye ndiyo analifata. Jina lake tu linaeleza kila kitu.
Dah mama una tabu sana[emoji23] [emoji23]
 
hapa una prove wewe kilaza na hukuelimika. jibu swali uliloulizwa usijishuku. unadhani dini yake ni tatizo kivipi maana sasa ndo unaanza kuwapa watu maswali kwa nini uhusishe na dini? je dini yake inahusishwa vipi na ugaidi? haya maswali watayaelewa waliosoma falsafa au sheria. ungekuwa una uelewa ungejibu kama ambavyo umeulizwa ukakomea hapo sasa kutaka kuzungumzia dini maana yake ni kuwa unaiweka dini yake jamaa katika kikaango. why should you do that? mbona zamani vyuoni tulikuwa tunafundishwa ku reason na kujibu logically? nyie wa siku hizi mnakuaje lakini? ndo maana mnafanya kazi ya ualimu iwe ngumu sana.walimu wanalalamika watu hawajibu maswali wanayoulizwa.wanaleta na yasiyokuwepo. which is bad and irrelevant.
Jifundishe kuandika maneno machache, hakuna mashindano ya ngonjera hapa.
 
Kama ni kweli ulikwenda shule kuelewa na sio kujifunza kusoma then alicho sema mleta uzi kinafikirisha, tuachane na suala la dini yake but je hi just coincidence au jambo linalo pangwa!? Kwamba matukio mawili makubwa tena ya kigaini na magaidi hao ni wale wale wa kundi moja na matukio yote jamaa awepo? No mama, hili linafikirisha sana, wala sio kidogo ingawa pia, jamaa anawezaje pia kujiweka wazi hivyo maeneo 2 tofauti kwa nyakati tofauti, hakudhani pia kama anaweza kutengeneza maswali kwa watu na hata wana usalama!? Achana na mambo ya dini kwanza hapa, tumfikirie huyu jamaa kwanza
Kanisome tena.
 
Huyo ni Mwalimu wa maswali ya intelijensia na usalama na ana kampuni binafsi ya mambo ya ulinzi na usalama. Utakuta hizo sehemu zote kampuni yake inahusika kutoa ulinzi. Likitokea yeye ni kati ya watu wa mwanzo kujulishwa na ni mtu asiyengoja amri ya mtu mwengine.

Au kwa Dini yake tu?

Dah!
Hivi bado hujaacha udini!!!????
 
Kenya wawekeze kwenye intelligence ili kuepusha haya matukio kabla hayajatokea. Haina maana kusifia watu baada ya matukio huku vifo na majeruhi ni wengi, tuwasifie kwa kutegua mipango ya magaidi.

Katika matukio yote inaonyesha magaidi wamesuka mipango kwa muda mrefu na inatokea downtown kabisa, hii ina maana intelligence ya nchi imefeli. Wawekeze kwenye intelligence ya nchi
Inawezekana wamezuia mengi ila kwakua haupo kwenye mfumo wao hujui lolote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu kauliza tu baada ya kuto ufafanuzi kuhusu huyo jamaa. Akitaka kujua mtoa mada anamtilia kuhusu dini yake, ili amfafanulie zaidi.

We hujaelewa na ushamtukana mtu kwa chuki zako binafsi

Anamtilia mashaka kuhusu dini yake kivipi?wewe aliyekwambia huyo jamaa ana dini ninani na dini yake hapa kwenye bandiko ilikuwa inahusika vipi ina maana siku hizi humu tunapita tukijadili dini za watu pasinakuangalia content ya uzi inavyosema?

Nimemtukana kwa sababu hajitambui na ni punguani wa dini,that's it!!!

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Hivi bado hujaacha udini!!!????
Kama kwa neno "udini" unamaanisha Uislam basi ninao sana, kwanza ni Uislam wangu kisha mengine.

Lakini kama una maana nyingine kuhusu "udini" tafadhali nifahamishe na mimi nielewe.
 
Wewe ndiye hujamwelewa rudi tena kusoma, au hukuona alama ya kuuliza pale. Si kauliza

Mtu kamfafanulia mtoa post kumtoa shaka kisha akamuuliza kama shaka yake ni kuhusu dini, maana Uislamu huandamwa pia na matukio hayo.

Umeshambulia bure

Alama ya Kuuliza sio issue,lazima ufikirie nje ya box,mwingine anauliza kinafik lakini dhamira yake anaijua mwenyewe na zaidi ya yote huyo unayemtetea records zake katika udini tunazijua fika,labda kama wewe umejiunga humu hivi karibuni
 
Tatizo la FaizaFoxy ni moja tu ameweka Udini mbele ata kwa vitu visivyo hitaji hoja za kidini

Mimi ni mtu ninaye mfatilia sana ni kwamba anatoa hoja nzuri na ni mchangiaji mzuri wa mada tena kwa weledi sana.

Tatizo ana udini mwingi sana kiasi ambacho Jf members wenyewe wamemfaham na itamwia vigumu siku za usoni

Sent from my SM-J530F using Tapatalk

Shida yake ndiyo hiyo,wasiomjua wanamtetea ila wakiangali records zake ndio watamjua vizuri
 
Alama ya Kuuliza sio issue,lazima ufikirie nje ya box,mwingine anauliza kinafik lakini dhamira yake anaijua mwenyewe na zaidi ya yote huyo unayemtetea records zake katika udini tunazijua fika,labda kama wewe umejiunga humu hivi karibuni
Sasa kila ukiwazacho wewe ndiyo kunakuwa hivyo, wewe ni mwanadamu acha kujifanya unaangaza mawazo ya wengine kama Nabii.
 
Alama ya Kuuliza sio issue,lazima ufikirie nje ya box,mwingine anauliza kinafik lakini dhamira yake anaijua mwenyewe na zaidi ya yote huyo unayemtetea records zake katika udini tunazijua fika,labda kama wewe umejiunga humu hivi karibuni
Mnakuwa wanafik nyinyi.

Mnasema magaidi Waislam, mleta mada anamtilia shaka Inayat Kassam, shaka kwa kuwa na yeye Muislam. Hapo hata mjitetee vipi.

Mnatamani ingekuwa nyinyi ndiyo Inayat.

Tukio la kwanza kulikuwa na kijana wa Kisomali shujaa aliyepambana, nae humu humu JF watu wakaanza.

Msitake kuteteana ujinga.
 
Back
Top Bottom