Nina kila dalili ya muathirika wa UKIMWI

Nina kila dalili ya muathirika wa UKIMWI

Bora uugue UKIMWI kuliko magonjwa mengine kama kansa n.k. Nenda kapime, kama unao jikaze we mwanaume, pima viral load na CD4, kama zimeshuka sana anza ARV faster, kama ziko poa anza kula balanced diet kama ulikuwa hufanyi hivyo, ishi healthy life.

Maisha ni fumbo, hakuna aijuaye kesho yake, kwa hiyo pambana mwanaume as long as bado unapumua, kuna wenzio wamepata vilema vya kutoweza kutembea lkn hawajakata tamaa sembuse wewe una nguvu na kutembea unatembea? Acha tabia za jinsia isiyo yako kijana, amka fanya maamuzi magumu for your bight future.
Unforgetable
 
kwenye hii dunia ya leo, UKIMWI siyo issue kivileeee, kuna watu tunasumbuliwa na magonjwa makubwa mara 10 zidi ya huo UKIMWI lakini tupo tunadunda …………...mzee piga konde moyo na maisha yaendelee kama kawaida,
 
hujaeleza km umeshaoa au una mwenzi
hapo ni Dalili za Corona iliyoikuta Diabates (sukari)
 
Api bila shaka umetoka kunyanduana na demu mwezi mmoja nyuma sasa unahisi atakuwa na ukimwi....ondoa shaka huna ukimwi wewe... Hiyo ni Hofu tu...na ukiendelea na hofu utashangaa unapata dalili zotee ..relax subiria baada ya miezi mitatu nenda taratibu kituo cha afya kapime... Hata usiogope...

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Anxious (wasiwasi) ni tatizo linalo develop stress (mkazo) na tatizo lako kuu ni your (Subconscious mind) kile unacho waza kile unacho weka concentration kweny Subconscious Mind ndio kina leta result kweny conscious mind Anza Sasa badili tabia yako within one week utakuwa OK kila ukiamka asubuh Sema kichwan mwako niko Sawa kila utembeapo Sema nipo Sawa kabla ya kulala Sema nipo Sawa jenga Imani hiyo kwa week moja Anza kufanya mazoezi asubuh saa 12 na jion kula vizur milo 3 mpaka 4 kwa siku usisahau matunda karanga kiganja kimoja yai 1 per day na maziwa kikombe kimoja kumbuka kile mtu anacho kiwaza ndicho humtokea mtu huyo choose happy choose life now maisha yako yatabadilika
 
Kuna watu mnajipa stress zisizo na sababu. Nakushauri "Nenda kapime ujue uwe huru" dalili unazozitaja no za lawaida sana hata magonjwa mengine kama typhoid yana dalili nyingi ya ulizozitaja.

Awe huru au afe kabisa?🤔 Braza usipime
 
Nenda kapime mkuu,,,,,,,,,matatizo mengi tu mwili husababisha home za mara kwa mara.....yapo mengine mengi tu husababisha kichwa kuuma.....na yapo mengine husababisha joto Kali mwilini

Sio virusi vya ukimwi pekee......kapime ujue afya yako ujitoe kwenye hicho kifungo
 
Nenda kapime Mimi niliugua nilikua na dalili Kama zako Hasa kichwa kuuma na jasho usiku, malaria kila ikifika jioni hali ndo inakua mbaya zaidi, nilikata tamaa nilikua nikivuta hisia njia nilizopita ndo nazidi kujuta nikajua tayari Nimeukwaa,
nikawa nalia kila siku majirani wakawa wananinyapaa wakajadiliana na rafiki yangu kwamba wachange, wanirudishe nyumbani wakampigia mwenye nyumba nilipokua nimepanga kwamba inabidi nirudishwe nyumbani kabla sijafa nisiwape mzigo nilikua na kilo 69 nilibakiza 32 nilifanya maamuzi magumu nikaenda kupima nilipima kila kitu nikakutwa na TB na pia ubavu wa kushoto ulikua na Maji nilitumia Dawa Miezi sita saivi nimepona niko fiti kabisa
 
Aya ya pili haiko sahihi! Wale walio ambukizwa kwa njia ya kurithishwa na wazazi au kuokoa binadam katika ajali, au kubadilisha damu hospital?

Aya yako ina element za unyanyapaa, tafadhari rekebisha, watu hawapati H.I.V kwa njia moja tu
 
Mkuu nenda kapime , usikute una minyoo
 
Hiyo hofu ndiyo inakufanya unazidi kuumwa na kujihisi dalili hizo zite,usikute hata si ukimwi kuna magonjwa mengine mkuu! Nenda kacheki na hata ikitokea ni Ukimwi kweli wala si mwisho wa maisha watu 20yrs sasa na wanadunda tu!ndoto zako zote utazitimiza usihofu.
 
Ndo shida ya kichwa kidogo(kile cha kule chini ya kitovu), saivi kimetulia kimyaaa kama hakihusiki vile. Mambo yooote sasa yameachwa kwa kichwa kikubwa (hiki cha juu cha kubebea matenga).
 
Mbona hiyo hali ndo tulizo nazo watu wa ukanda wa pwani?
Yaan unajijaza hofu hivi? Hili joto limekoma kwasababu ya mvua ya jana tu. Ila mwili unavuja maji ya jasho kama bomba. Kuumwa kichwa ni kuwaza sana. Na hii ni mbaya sana kwani mwili haupumziki na ubongo kuendelea kufanya kazi 24/7.
Kunywa maji mengi na chakula vzr. Halaf suala la ngozi upake mafuta mazuri ya nazi kama parachute etc. Ondoa shaka hizo usije kuzidi kujigharimu. Zaidi kapime ili uondokane kbs na hofu maana sasa hata nguvu ya utafutaji utapotea kabisa.
 
Mbona Kama dalili za UTI ukimw hauko ivyo ungekua unatapika na kuharisha Sawa plas kukohoa
Nenda tu kapime hofu ni mbaya Sana sababu hata mimi ulisha wahi kunikuta kitu kama io na sababu ya stress nikaanza kuzitengeneza dalili zote za ukimw hakika nilipata tabu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom