Nina kila dalili ya muathirika wa UKIMWI

mwakije

Member
Dec 3, 2020
20
20
Husika 'na kichwa cha habari hapo juu

Mimi ni kijana mwenye umri 30 'niliekua na malengo na mipango mbalimbali 'katika maisha moja katika ayo ' ni kuwa na mjengo ili nimefanikisha kwa 70%.

lakini sasa hadi hapa nilipofikia sidhani kama yataendelea na nitafanikisha au kuendeleza palipo baki 'nimesha kata tamaa kabisa ' twende kwenye mada

Nina kila dalili zinazo ashiria 'kua ni muathirika wa HIV.

Hivi karibuni nimekua na mabadiliko kwenye mwili wangu adi yananipa hofu imefikia hatu ya kukata tamaa kabisa na kutamani bora nife

  • Homa kwangu aziishi aipiti wiki bila ya kuumwa
  • Maumivu ya kichwa kwa muda mlefu"adi nachanganyikiwa
  • Joto kupanda
  • kuwa na jasho jingi kipindi cha usiku
  • viungo kukaza na mbadiliko ya ngozi ngozi inakua na muonekano wa kupauka kusinyaa kama mzee inanipa shida hii

Hayo yote yananifanya niwe mtu wa stress mawazo na kujiona sina samani na mlengo yoote kuishia njiani

'Natamani sana kwenda kupima naogopa kuchanganyikiwa kupokea majibu vibaya

Pia waweza nishauri chochote kile kunitoa kwenye hili janga
 
Kuna watu mnajipa stress zisizo na sababu. Nakushauri "Nenda kapime ujue uwe huru" dalili unazozitaja no za lawaida sana hata magonjwa mengine kama typhoid yana dalili nyingi ya ulizozitaja.
 
Aliwazialo mtu ndilo humtokea, ukikili kwa kinywa chako kuwa una UKIMWI lazima uugue kweli kwa maana ya kwamba, sisi wanadamu tuna uungu ndani yetu yaani mungu alitupa nguvu sawa na zake, chochote unachokinena kwa kinywa chako kinaumba katika ulimwengu wa roho, ndipo magonjwa uanza kuonekana katika ulimwengu wa kawaida yaani wa mwili, magonjwa kama.

UKIMWI ni raha ya dhambi za wanadamu kutenda uovu, hivo ukijinenea kuwa una UKIMWI lazima uugue kweli maana hata wachawi ni rahisi kukutengenezea UKIMWI.

Ushauri katubu maneno yako uliyojinenea kuwa unaumwa, fanya toba ukajitakase, kuanzia mwili, roho, nafsi na moyo wako. Kisha katoe sadaka popote aidha kituo cha yatima, wajane au kanisani | msikitini.
 
Umejijaza hofu

Namna unaogopa mpaka nimeshangaa mbona watu wanao wanadunda tu mtaani, ila wewe hata kama ukikutwa+ ninashaka sana kama hata utamaliza mwaka kwa sababu ya hofu.

Halafu mbona umeiweka kama vile huna jinsi kabisaa ya kufahamu ukweli wa status yako,yaani kama vile tunaishi bado enzi za ujima za kuhisihisi.
 
Nenda kapime mzee, ndio suluhu la kila kitu, hiyo kichwa kuuma ni kutokana na kuwaza sana hilo suala lako bila ufumbuzi wa uhakika. Kitu pekee cha kukuweka huru ni kapime tu.

Tunakupenda sana, kesho asubuhi nenda kituo cha afya mbali na unapoishi ambapo hao wahudumu wa afya hawakujui, nenda kapime kwa uhuru, pokea majibu, ukiwa huna, basi badili tabia, ukiwa nao zingatia ushauri wa wataalamu wetu wa afya ili uishi kwa matumaini.

ila kwa kipimo changu ambacho kinabase kwenye maelezo yako, wewe sio muathirika kabisa, kapime tu lakini huna vvu
 
Aliwazialo mtu ndilo humtokea, ukikili kwa kinywa chako kuwa una UKIMWI lazima uugue kweli kwa maana ya kwamba, sisi wanadamu tuna uungu ndani yetu yaani mungu alitupa nguvu sawa na zake..
Well said, hii kitu inaitwa "the power of subconscious mind" ina nguvu balaa ukiitumia postive utafaidika.
 
Back
Top Bottom