Msaada baada ya kuuza mechi nimekuwa mtu wa kuhisi nimeambukizwa UKIMWI

political monger senior

JF-Expert Member
Nov 26, 2020
1,801
5,788
Wiki 2 na siku 5 zilizopita nimetoka kuuza mechi( yani kupiga kavu) na demu ambae tunajuana kwa muda mrefu.. balaa likaja baada ya kupita wiki 1 na siku kazaa nilipata mafua makali lakini yakakata baada ya siku 2.

Siku niliyopata mafua nimelala ghafla tu usiku mawazo yakaja kuwa yule demu atakuwa amekuambukiza ukimwi. Nikaanza kuwa mtu wa mawazo nikaamua ku google dalili za mwanzo za ukimwi lohh karibu 3 au 4 ninazo mwili kukosa nguvu, magoti kuchoka, koo kuuma kama maumivu ya matonsil, pamoja na vipele vidogo vidogo kutoka mgongoni.

Wakuu napata mawazo mpaka kichwa upande wa kisogoni kunawaka moto.. nikaanza kuvurugwa na kuanza kumtumia demu meseji za ajabu kama vile "" kwanini umenifanyia hivi si ungesema tu kuliko kuniua demu aka react na kuniuliza kuwa anielewi ninachomaanisha nikamchana live kuwa kaniambukiza ukimwi.

Nikamwambia kama kweli unajiona uko salama twende tukapime dohhh alikataa kata kata na mimi ndio nikazidi kudata kwa mawazo nimembeleza tukapime wapi.. Nikajipa tiki tu direct kuwa mimi tayari ni muathirika, baada ya kufika wiki 2 nikaenda kupima mwenyewe kwakuwa nilishajikatia tamaa sikuwa naogopa kabisa.

Nilipimwa na kukutwa Negative nikaambiwa nipime tena baada ya miezi sita kidogo nikawa na furaha lakini baada ya muda yakaja mawazo mengine vijidudu ni ngumu kuonekana baada ya wiki 2 nikaanza upya mawazo..nikaenda kupima tena sehemu nyingine majibu yakawa yale yale mpaka nikaanza kubishana na mpimaji na kuanza kumuelezea dalili zangu akaniambia nirudi tena baada ya miezi mitatu..

Ikafika hatua nikatamani nitafute mganga amroge. Yule demu ili nikimwambia tukapime basi asikatae...Najua kuna wataalamu wa afya hapa JF naombeni msaada wenu kwa hili ninalopitia.

Thanks
 
Wiki 2 na siku 5 zilizopita nimetoka kuhuza mechi( yani kupiga kavu) na demu ambae tunajuana kwa muda mrefu.. balaa likaja baada ya kupita wiki1 na siku kazaa nilipata mafua makali lakini yakakata baada ya siku 2 ..siku niliyopata mafua nimelala ghafla tu usiku mawazo yakaja kuwa yule demu atakuwa amekuambukiza ukimwi..nikaanza kuwa mtu wa mawazo nikaamua ku google dalili za mwanzo za ukimwi lohh karibu 3 au 4 ninazo mwili kukosa nguvu, magoti kuchoka ,koo kuhuma kama maumivu ya matonsil,pamoja na vipele vidogo vidogo kutoka mgongoni..wakuu napata mawazo mpaka kichwa upande wa kisogoni kunawaka moto.. nikaanza kuvurugwa na kuanza kumtumia demu meseji za ajabu kama vile "" kwanini umenifanyia ivi si ungesema tu kuliko kuniuwa demu aka react na kuniuliza kuwa anielewi ninachomaanisha nikamchana live kuwa kaniambukiza ukimwi..nikamwambia kama kweli unajiona uko salama twende tukapime dohhh alikataa kata kata na mimi ndio nikazidi kudata kwa mawazo nimembeleza tukapime wapi..nikajipa tiki tu direct kuwa mimi tayari ni muathirika baada ya kufika wiki 2 nkaenda kupima mwenyewe kwakuwa nilishajikatia tamaa sikuwa naogopa kabisa nilipimwa na kukutwa Negative nikaambiwa nipime tena baada ya miezi sita kidogo nikawa na furaha lakini baada ya muda Yakaja mawazo mengine vijidudu ni ngumu kuonekana baada ya wiki 2 nikaanza upya mawazo..nikaenda kupima tena sehemu nyingine majibu yakawa yale yale mpaka
Nikaanza kubishana na mpimaji na kuanza kumuelezea dalili zangu akaniambia nirudi tena baada ya miezi mitatu..
Ikafika hatua nikatamani nitafute mganga amroge
Yule demu ili nikimwambia tukapime basi asikatae...Najua kuna wataalamu wa afya apa JF naombeni msaada wenu kwa ili ninalopitia..thanks
Husingehuza mechi banaa..!!! ANyway, siku nyingine HUSIRUDIE KUHUZA MECHI
 
Mkuu,ondoa wasiwasi,halafu kumlazimisha huyo demu wako akapime,hakuwezi kubadili chochote juu ya afya yako,

Subiri muda ufike ukapime tena,hope huna maambukizo,

Wataalamu watakuja kukupa muongozo.
Yani namlazimisha ili ikigundulika yeye hana basi na mimi ni mzima kwa mawazo yangu ndio yananituma hivyo..
 
Back
Top Bottom