Nina hasira na wife, ushauri wenu please

Nina hasira na wife, ushauri wenu please

Umenikumbusha mbali sana,Nyumbani am first born na wazee walikuwa wanashughuli zao za biashara wanafanya, hvyo majukumu ya kulea wadogo zangu tulikuwa tunasaidiana na wazee sababu hamna house girl,Most of the time lazima nimfunge mdogo wangu mgongoni ili shughuli zingine zifanyike-Nilikuwa nachoka sana,na hapo unakuta muda wa kulea wadogo zangu ndo muda marafiki zangu wanacheza michezo huko nje yan nilikuwa stressed vibaya kwa sababu sina nafasi ya kushiriki nao kama mtoto mwenzao na hapo mtu unajikuta unajifunza mambo mengi sana juu ya maisha.Mwanamke kupewa uhuru ni lazima lasivyo ndoa inaweza kuingia kwenye changamoto.
Hahaha.
unatoka shule saa 9, mmekubaliana mkutane kwenye mechi ya mpira jioni, unafika home, maza anakuambia anaenda kazini mahindi ameandaa nikayasage. So unamfunga dogo mgongoni, mahindi kichwani mdogomdogo hadi mashineni. Ukirudi hakuna kutoka upike ugali, mshua akija ale uoshe vyombo.

hii experience inasaidia sana.
Nyie sasa ndio wanaume hodari[emoji7]
 
Binafsi nachukia umwinyi sana.Ndoa nyingi nw days wanaume wanalalamika changamoto lakin ukiangalia kiundani vijana wengi sana wameandamwa na mambo ya kijinga na uvivu,mwanaume unakuta amekaa anabet mkewe anapika alafu anamwita ampelekee maji bafuni-This is bullshit.Since naoa biashara ya kuwekewa maji bafuni niliikata unless ni mgonjwa sana
Bora wewe useme.. akiongea mwanamke anaonekana mkorofi plus jeuri..
Wajifunze kwenu the real meaning of partnership maana wako kwenye master and servant mode..
 
Kwa uzoefu tu, Hapa ndugu yangu mkeo analiwa/ anatafunwa kimyakimya na jirani au 'njemba' flani.

Mwanamke wa hivi 'anazuga' ili kuficha madhambi yake.

Take it brother.

usikariri! Yawezekana pia mwana anajam zake zinazomkera m'ke ndio maana ana behave hivyo. Ni ngumu kujudge kwa maelezo ya upande mmoja.
 
Hebu ngoja kwani ukiwa unaleta hela ndan ya nyumba, ba mkeo akawa buzzy na kuhudumia nyumba kwa mambo mengine mengi, je kupika mwanaume hapo ni kosa au dhambi? Au hasara huyo ni ipi?
Huna time management ndo maana zinakushinda ungelikuwa unajipanga na ratiba ukafuata usingeshindwa kumpikia mumeo chakula cha jioni kwani maids huwa wanawezaje kukamilisha kila kitu on time? ina maana unapitwa uwezo na mfanyakazi wa ndani? sasa si utoke abaki yeye nijue moja tu. Huo ni uzembe na kujiendekeza na kutokujua majukumu yako ndani ya ndoa kwa kifupi ndoa imekushinda
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Hahahaaa ukweli Mchungu.....Kweli Maji ni Bwerere kwasasa angevuta maji kupeleka chooni akaondoa tatizo la kutengewa maji kwenye ndoo na kopo ,pia kuhusu kufua angenunua washing mashine au awe anapeleka Dry Cleaner/Laundry.
kuhusu simu aweke fingerprint

na swala La kutokujibu straight ni hurka tu

Mimi pia sipendi maswali ukinikuta kwenye mood mbovu ukiniuliza nitakujibu tu sijui/sielewi nimemaliza.
Mtu wangu anaelewa Hivyo ataachana na Hiyo mada till next time
 
Hahaha.
unatoka shule saa 9, mmekubaliana mkutane kwenye mechi ya mpira jioni, unafika home, maza anakuambia anaenda kazini mahindi ameandaa nikayasage. So unamfunga dogo mgongoni, mahindi kichwani mdogomdogo hadi mashineni. Ukirudi hakuna kutoka upike ugali, mshua akija ale uoshe vyombo.

hii experience inasaidia sana.
alafu ukipita ground washikaji wanacheza mpira wanakuita dada huyo...basi full hasira kisa umebeba mdogo wako mgongoni.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Wandugu mimi ni mfanyakazi katika taasisi binafsi ya elimu, nna mke na watoto wawili, nimeishi na mke wangu Sasa mwaka wa 4 baada ya kumzalisha baadae nikamchukua awe mke wangu,

Mwaka Jana mwishoni nlilipa mahari kiasi Cha tsh 1.5m na tumeishi maisha ya amani mpaka leo ila Ana matatizo haya ndio yamenifanya niwaone wakuu:

Mosi, huwa anapata wakati mgumu kunijibu ninapomuuliza kitu

Pili, ni muongo, anaweza kukueleza kwamba alikueleza kitu Fulani wakati hakusema kabisaaa

Tatu, amekuwa mvivu kunifulia hasa baada ya Mimi kufanya kufua nguo kipindi akiwa mgonjwa, now anahisi ni wajibu wangu kufua

Nne, Jambo la Mimi kuoga Wala usimuulize, nna Zaidi ya mwezi sijatengewa maji ya kuoga najitengea mwenyewe

Tano, anapenda Sana kunichunguza Kama nachepuka, juzi tumegombana kwa kusachi simu yangu japo hapakuwa na pa kunikamatia ila kuona sms ya mdada kanisalimia ilikuwa Vita.

Na hii ndio shida kuu, ananivizia usiku anasearch simu yangu Sana na sometime anawapigia wadada nilowasave namba zao, KEROOO

NATAMANI SANA AMANI LAKINI NAHISI ANATAFUTA SHIDA

NISHAACHA UJINGA JAPO HATA YEYE NILIMPATIA UJINGANI LAKINI NAHISI ATANIRUDISHA UJINGANI

USHAURI WENU PLEASE....

Nina maswali ya kukuuliza:

Umesema ulikutana nae ujingani? JIbu: bado ana mawazo ya wewe kuchepuka kwa sababu ya njia uliyompata
Umesema una miaka 4 pamoja, je miaka hiyo minne unaishi nae au ni miaka ambayo mmefahamiana ukijumlisha ya kukaa?
Je hii tabia ya kutokuwekea maji bafuni imeanzaje? Aliwahi kuwa anakuwekea maji?
Mkeo ni mfanyakazi au ni mama wa nyumbani?
Kabla ya kuanzisha mahusiano, amewahi kukudanganya?
Hii tabia kuchunguza simu yako imeanza baada ya kukaa nae au mkiwa uchumbani alikuwa akishika simu yako.

Mkeo umemuoa kwa mapenzi au umemuoa baada ya kuwa umezalisha, ukamuonea huruma ili mlee watoto?

Ukinijibu vizuri haya maswali, ukawa genuin, naweza kushauri kitu hapa. ikawa funzo kwa wanaume wengine wanaopitia changamoto kama yako.
 
Ungesema hakutengei chakula ningeshangaa, lakini kufuliwa na maji ya kuoga ulalamile?
Yeye ana majukumu mangapi?
Hayo mengine na uongo na upekuzi wa simu kaeni muyazungumze au weka simu password.
 
Kwa uzoefu tu, Hapa ndugu yangu mkeo analiwa/ anatafunwa kimyakimya na jirani au 'njemba' flani.

Mwanamke wa hivi 'anazuga' ili kuficha madhambi yake.

Take it brother.
Hii ni kweli kabisa, kuna aina nyingi sana za wanawake na tabia zao, ila ukituliza akili kwa hii comment utaelewa

Mimi yalinikuta haya nikaja tambua kumbe mwenzangu anamtu kwa siri sana hua anaongea nae kwa miaka miwili na tangu kajuana na huyo mtu ndo dharau zikaanza ( huyo jamaa alikua nje ya nchi)
 
Duuh hivi ni kwamba mabafuni hamuwekagi mabomba ya maji au mnapenda tu kutengewa maji kwenye ndoo
 
Hii ni kweli kabisa, kuna aina nyingi sana za wanawake na tabia zao, ila ukituliza akili kwa hii comment utaelewa

Mimi yalinikuta haya nikaja tambua kumbe mwenzangu anamtu kwa siri sana hua anaongea nae kwa miaka miwili na tangu kajuana na huyo mtu ndo dharau zikaanza ( huyo jamaa alikua nje ya nchi)
Kuna baadhi ya wanawake wana 'trik' hatari sana ya kumzubaisha mwanaume ili 'asimshukie' kama anapigwa nje, sasa usipotumia uzoefu na 'intelejensia' kwa jicho la tatu, umeumia!
 
Polee mkuu,hawa watu tuishie nao kwa akili,nachotaka kukwambia huyo wako yupo vizuri tu hana shida kabisa,kuna watu wanaishi na wanawake na wamedumu kwa muda mrefu lakini kwa haraka ni pasua kichwa kiwango cha SGR wanatofautina kidogo tu kila mmoja anakuwa na namna yake na kuna watu wameoa wanawake wanatukana hatari,ukifanya mchezo na makofi unachezea[emoji23][emoji23][emoji23],ukichelewa kurudi hafungui mlango,yaani ni full vituko.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kwani Kuna sehem kasema Hana hela [emoji38]

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa viumbe wa kike utafikiri wana pepo, wanataka kuishi uzungu wanaouona kwenye tv. Ukifuatilia kwa umakini utagundua anaandika kwa jazba sana. Wadada wasm dizaini hii wanazidi kuongezeka, ujinga umewatawala sana
 
Bora wewe useme.. akiongea mwanamke anaonekana mkorofi plus jeuri..
Wajifunze kwenu the real meaning of partnership maana wako kwenye master and servant mode..
Dada ukiolewa wewe ni mtumishi wa mwanaume,mwanaume akipika au akipeleka maji bafuni ni choice yake tu au sign of appreciation kwako.kwahyo asipo fanya haimaanisha ni mkorofi ila wewe usipofanya huo ni ukaidi.kama unaolewa na haujui kwamba unaenda kumtumikia mwanaume basi bora ubaki na maisha yako tu
 
Back
Top Bottom