Nina hasira na wife, ushauri wenu please

indundidotcom

JF-Expert Member
Mar 4, 2017
220
250
Wandugu mimi ni mfanyakazi katika taasisi binafsi ya elimu, nna mke na watoto wawili, nimeishi na mke wangu Sasa mwaka wa 4 baada ya kumzalisha baadae nikamchukua awe mke wangu,

Mwaka Jana mwishoni nlilipa mahari kiasi Cha tsh 1.5m na tumeishi maisha ya amani mpaka leo ila Ana matatizo haya ndio yamenifanya niwaone wakuu:

Mosi, huwa anapata wakati mgumu kunijibu ninapomuuliza kitu

Pili, ni muongo, anaweza kukueleza kwamba alikueleza kitu Fulani wakati hakusema kabisaaa

Tatu, amekuwa mvivu kunifulia hasa baada ya Mimi kufanya kufua nguo kipindi akiwa mgonjwa, now anahisi ni wajibu wangu kufua

Nne, Jambo la Mimi kuoga Wala usimuulize, nna Zaidi ya mwezi sijatengewa maji ya kuoga najitengea mwenyewe

Tano, anapenda Sana kunichunguza Kama nachepuka, juzi tumegombana kwa kusachi simu yangu japo hapakuwa na pa kunikamatia ila kuona sms ya mdada kanisalimia ilikuwa Vita.

Na hii ndio shida kuu, ananivizia usiku anasearch simu yangu Sana na sometime anawapigia wadada nilowasave namba zao, KEROOO

NATAMANI SANA AMANI LAKINI NAHISI ANATAFUTA SHIDA

NISHAACHA UJINGA JAPO HATA YEYE NILIMPATIA UJINGANI LAKINI NAHISI ATANIRUDISHA UJINGANI

USHAURI WENU PLEASE....
 

Pablo Jr

JF-Expert Member
Sep 12, 2018
452
1,000
Huyo mpe psychological tocha, fanya hivi Kama umeshamuonya Mara kibao hasikii.! Nguo zako peleka dry cleaner Kama hazifui ongea pale ambapo Kuna ulazima ...Kama anaona uvivu kukujibu hizo Ni dharau ..... Simu yako ipige password mpya na kamwe usiruhusu mwanamke ashike sim yako Kuwa Mwanaume usikae kizembe Mwanamke usikae nae kimazoea .

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom