Nina hasira na wife, ushauri wenu please

Daaah watu siku hizi wanafeli sana yani kuna mambo ambayo hata huwezi kuwaza kama kweli wewe umekulia katika tamaduni za kiafrica yaani ni kutoa maamuzi tu, tatizo mnajifanya uzungu mwingi wakati uhalisia hauko hivyo
 
Kweli kabisa watu tuliokuwa tunafanya hizo kazi tangu utoto ,tulivyooa hatukuwa tunasubiri wake zetu ndio wafanye!! Mimi hakuna kazi ya nyumbani ambayo siwezi kuanzia kupika,kufua,kufagia ndani/nje,kulima majani ,nikiona hakupo sawa narekebisha mwenyewe sisubiri wife au Hg ndio afanye!!
Ndo maana vijana wa saivi wengine wanakimbilia kuoa mapema huku hawajawa tayar kwa maisha ya ndoa, kisa ni wavivu wa kutojua kazi za nyumbani. Wanataka mwanamke awe cheap labour ndan ya ndoa, kitu ambacho hakiwezekan mwshoe ndoa zinavunjika holela tyuuh.
 
Huna time management ndo maana zinakushinda ungelikuwa unajipanga na ratiba ukafuata usingeshindwa kumpikia mumeo chakula cha jioni kwani maids huwa wanawezaje kukamilisha kila kitu on time? ina maana unapitwa uwezo na mfanyakazi wa ndani? sasa si utoke abaki yeye nijue moja tu. Huo ni uzembe na kujiendekeza na kutokujua majukumu yako ndani ya ndoa kwa kifupi ndoa imekushinda
Poleeeh sana, sio kosa lako ni malezi tatizo.
 
Huyo ni katika lile kundi la wanawake wanaoitwa wakorofi,unakuta nyumba imetulia lakini anachokonyoa mambo ili mgombane,na hapo ndio pale mwanaume anapoanza kuona nyumbani kuchungu anatafuta vitu vya kuvutia muda ili arudi nyumbani late hours......
 
Back
Top Bottom