Mahusiano na huyu mwanamke siyaelewi kabisa, sielewi ananichukuliaje

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,458
99,098
Habar wakuu,

Huyu mwanamke amejiajiri Ni fundi cherehani, ana miaka 27 hajaolewa na anaishi mwenyewe na mtoto wake mmoja wa kike.

Tulikutana vipi?

Kwenye fremu wanakoshonea nguo na wanawake wenzie, jumla Kama watano hivi.

MKE Wangu alishonesha sare za chama kipindi kile Cha mwanzoni mwa kampeni za Uchaguzi 2020, ila kwa mwenzie ambae Ni fundi mwenzie katika majengo ya ofisi za CHAMA.

Sasa Katika fika fika pale na MKE Wangu kufatilia nguo zake ikatokea nikavutiwa nae. Ila sikuonesha ishara yoyote ile.

1. Kuna siku nmefika pale wenzie wote washaondoka, nmechukua namba yake, tumewasiliana nmempa mwaliko wa dinner, alivokubali tu, usiku huo huo wa dinner nikatembea nae lodge ya jirani. Na kwasababu alilewa Sana, tulifanya TU Ila sikuenjoy kivile ukzingatia tulitumia kinga.

Baada ya kufanya nae mapenz, nikaondoka pale saa 7 usiku kurud nyumban kwangu, mezan nikamuachia posho yake nakuondoka pale. Kesho yake nmekuta sms yake kanitext kunishukuru kwa dinner na jinsi nilivo.jali. Nikasema ntamjib sms zake baadae Mambo yakaingiliana nikasahau. Baadae akanipigia sikupokea sim zake, sms akatuma tena nazipotezea sizijibu, hivyo Hatukuwasiliana Tena.

2. Tumekuja kutana Tena baada ya miez 2 kwenye harusi moja usiku. Niko na wife tumetulia akanitext kua kaniona. Ule muda wa shamra shamra za zawadi alivovalia akanitamanisha.
Nikamtext kua nimuone Mara moja nje kwenye gar tusalimiane.

Alivokubali nikampeleka mbal kdg na pale Kuna kigiza nikapaki, nikanunua Kinga duka la jirani, tukafanya fasta fasta ndani ya gari Kisha nikampatia posho yake tukaagana nikarudi ukumbini kumchukua wife na kwenda nyumban. Baada ya Hapo akawa ananitumia sms najibu kidg nyingine nazipotezea sizijibu. Nadhan alichoka akakaa kimya, hivyo hatukuwasiliana Tena.

3. Tumekuja kukutana tena baada ya ugomvi na mchepuko wangu mamaJ, nikawa nmezidiwa ikabd nimtext nmemmiss nataka nmuone, akasema sawa na kanimiss pia. Tumekutana lodge, ikabid nimwambie kua nmechoka kutumia kinga maana sienjoy.

Kama uwezekano tupime ili Tufanye nikavutiwa kavu. Akasema sawa. Nmempima Yuko salama, tumefanya, tumemaliza, nmemwachia posho yake, tumeagana na kila mtu kaondoka zake. Baada ya Hapo akawa ananipigia sim kila Mara kunijulia na akitaka tuonane Tena. Namkwepa.

Nadhan yeye mwnyw alijiongeza kwamba namkwepa, hivyo alipunguza mawasiliano,hakunitafuta na hivyo hatukuwasiliana Tena.

4. Imepita miezi Kuna siku mteja wangu mmoja akawa na tatizo la kifund kwa bidhaa nilomuuzia, nikasema ntakuja niione uko nyumbani kwake. Akasema Ni kwake ni mbagara kwa ndani ndani kdg.

(Jina la mtaa Kunaitwa kwa Bibi ***)
Nikasema huko nitakuja kuliona tatizo lako baada ya mda wangu wa kazi kuisha. Mteja Akasema sawa.

Nmefika DARLIVE, mteja kaja kunipokea aniongoze mpk kwake (Ni ndani ndani sana uko). Nmefika kwa mteja Niko nashughulikia tatizo lake, sms ya huyu mdada ikaingia kua "leo naona umeamua kututembelea mtaan kwetu" nikauliza kivipi. Akasema kaiona gar yang imepak sehem flan na plate number anaijua.

Basi Nikampa mwenyej wangu amwelekeze nilipo aje tusalimiane,kweli akalelekezwa na akafika mpk pale nilipo.

Nilipomalizana na mteja akasema, kabla sijaondoka nifike na kwake nitie baraka kidg. Nikasema sawa. Nmefika kwake nikakuta kapanga chumba kimoja. Nyumba Ni ya udongo (makuti) ila imepigwa plasta ya udongo Na chokaa kwa nje, afu imepauliwa na bati.

Sakafu ni ya vumbi, Ina ceiling ya mianzi (zile za kizamani). Hana hata Kochi nilikaa juu ya kitanda Cha ft 4×6.Nmekunywa maji glass moja pale, nikamuachia elfu 5 nikaondoka zangu.

5.Kesho yake tumechat Sana kwa sms, akanambia anaomba nimsaidie Ela ya Kodi, nikamuuliza kwani analipa sh.ngap kwa mwez pale, akasema elfu 9 tu (yaani 9,000) jumla kwa miez 6 Ni elfu 54.

Akilini nikajua uyu keshaanza vizinga, ila mm mwnyw nnamhitaji maana tumezinguana na mama J (ukitaka kula lazima uliwe kdg). Basi nikamwambia tuonane Jion ukishafunga, tukutane lodge yetu Ile ile, ukifika kalipie chumba kabisa nkukute ndani, ntakurudishia Ela yako ya chumba nkishafika. Ukishachukua chumba nipigie. Akasema sawa.

Nmefika lodge tumefanya mapenzi tumemaliza, Nikampa jumla elfu 50 wa mchanganuo wa
-elfu 20, yakulipia chumba
-elfu 10, nauli yake
-elfu 20, posho yake
Kuhusu Ela ya Kodi tulokubaliana, nikamwambia ntamtumia kesho yake kwenye simu, akasema sawa. Tukaagana kila mtu akaenda zake.

Kesho yake alfajir nikaamka nmeSafir,
Niko safarini kanipigia kukumbushia ile ela ya kodi, nikamwambia Niko Safar ila narud keshokutwa (baada ya siku 2) ntakupa Iyo pesa, akasema sawa.

Nmerudi nikasahau kabisa kumtafuta na khs ile pesa aliyoniomba, nikaendlea na ratiba zangu. Na yeye hajanitafuta Wala kukumbushia Tena khs ile ahadi.

6. Kuna siku mchana wa adhana Niko dukani (ni zaidi ya mwezi tangu nmerudi) nastuka mtu huyu hapa (yule mwanamke). Kiukweli nilijiskia aibu Sana, huku yeye akiwa anatabasamu.

Ikabd tusalimiane na nmuulize anamishe gan mjini MDA huu, akasema kaja kununua nguo za mwanae kaona apite anisalimie. Anataka ampeleke mwanae kwa Bibi yake (mama Yake mzazi) kibaha.

Ikabd nimtoe pale dukan
nimwambie twende tukale kwanza maana nna njaa Sana hapa, baada ya Hapo ntakusindikiza uko kibaha. Akasema sawa atashkuru.

Nmempeleka mgahawani
Tumemaliza kula, ikabd tukamfate mtoto. Nmenyoosha Njia ya mbagala mpk pale kwake, akasema hapana hajamuacha pale. Bali alimuacha na saiti kwake na mafundi. Ikabd twende mpk huko huko (Ni chamazi ndani ndani kdg).

Nmefika saiti kwake,
Tumemkuta mwanae anacheza na wenzie nyumba ya jirani. Aisee kumbe mwanamke yule kajenga kimoja tu, ila kina choo ndani. Kainua kuta zote ila Kabakiza kupiga bati,madirisha na milango . Ikabidi nimpongeze sana kwa mapambano na hatua aliyofikia.

Akanionyesha bati 3 alitunza kwenye hiyo nyumba ya jirani aliko mwanae, akasema Bado bati 7 zitimie bati 10 alizoambiwa na fundi wake. Ananiomba nimchangie.

Nikasema "sawa, ila kwanza naomba nitimize ahadi yetu Ile ya kodi, sorry Mambo mengi nilijisahau (nikamkabidhi elfu 60). Izo bati 7 ntakupa mwisho wa mwezi"

Akasema "sawa nmekuelewa Asante sana sema kwny kodi ushachelewa maana nishamwambia mwenye nyumba atafute mtu nahama mwezi huu nihamie kwangu, Kwaiyo Hii Ela ntalipia mbao niweze kufunika Hapa"

Nikasema "sawa, VIP khs madirisha"

Akasema "Haina shida, ntaweka mbele ya safari. Kwasasa ntapanga matofali yalobaki na kufunika na pazia"

Nikasema "sawa"
Nikampelekea kibaha, Kisha nikamrudisha.
tukapitia lodge tukafanya yakufanya, nikamuachia posho yake na tukaagana kila mtu akaenda zake.

Mwisho mwezi ulipofika,kanitext kunikumbusha ile Ela ya bati. Nmewaza sana na kuwazua khs kumchangia bati kwenye nyumba yake, aisee Moyo wangu ukawa mzito sana. Nikampotezea sikujibu, akinipigia sikupokea. Nayeye hakunitafuta Tena.

7. Baada ya Miezi hivi Niko dukan kwangu asbh nmetulia,ikaingia Simu namba ni ngeni. Kupokea akajitambulisha Ni yule mdada, anaomba aje anione mara moja Apo ofsin amenimiss. Nikamwambia sipo ofsin MDA huu. Akasema mbona ananiona ofsini, yeye Yuko upande wa pili wa barabara nitizame ntamuona.
Kuangalia barababani upande wa pili, aisee kweli Ni yeye ananipungia mkono, mwnyw nikaona aibu, nikamwabia basi njoo TU.

Amefika tumesalimiana vizur,
namuuliza anamishe gan mjini mida Hii, kanambia kaja kununua madirisha 2 na mlango 1 wa chuma (geti) anaomba nimsaidie usafiri vifike saiti kwake, hapa kabakiwa na elfu 10 TU. Watu wa kirikuu wanataka elfu 25 mpaka vifike saiti kwake.

Ikabd nimuitie kirikuu wa pale kijiwen ofsn kwangu amplekee, ntamlipa Mimi. Elfu 10 yake nkamwambia atakunywa maji. Akashkuru Sana, tukaagana na akaondoka zake.

Alivofika akanishkuru Sana, nikasema sawa, akasema anaomba nije nimtembelee maana keshahamia kwake tayari. Nikasema sawa jion nkishafunga ntakuja. Jion imefika ratiba zikaingiliana, sikwenda kwake Wala hata taarifa sikumpa. Naye hakunitafuta. Ikawa tumepotezeana.

8. Wikendi moja asbh nmevurugana na mamaJ, kanuna kaninyima unyumba. Ikabd nimtafute kwenye simu.
Nikamwambia nmemiss, akajibu kanimiss pia.

Nkamwambia Kwaiyo inakuaje, akasema ananiskiliza Mimi.
Nikamwambia tukutane basi lodge,pale pale pa siku ile. Akasema "sawa". Kufika lodge Niko nje nampigia nmefika ili aje, ananambia yeye keshafika tayar mm nipitilize moja kwa moja Hadi chumba namba flani.

Nmeingia, tumefanya ya kufanya,
Nmempa elfu 50 kama Ela ya posho, nauli na fidia yake ya chumba.

Akanirudishia elfu 30 akisema nae leo hiyo elfu 20 kaamua kuchangia ela ya chumba na elfu 10 anaomba nibaki nayo achangie mafuta ili nimrudishe kwake Mimi mwnyw . Leo kachoka hajiskii kabisa kupanda daladala au bodaboda. Nikasema sawa. Nikampeleka mpk kwake.

Kufika kwake, nikakuta keshafanya maendeleo makubwa sana tangu nilivopaacha Mara ya mwisho nmekuja pale. Keshafunga milango na madirisha ya grill (Bado nyavu), kapiga plasta kuta za ndani na kusakafia chini kwa rough floor. Nikampongeza Sana. Akashkuru Sana na akanionyesha na chooni kua keshafunga sinki tayar na Bomba la kinyesi katolea nje, ila anaogea chooni TU na sio kujisaidia (anajisaidia kwa jirani yake) maana bado hajafunikia na mfuniko wa zege juu.

Kwaiyo akaniomba nimchangie kidg laki afunikie maana mchanga na kokoto anavyo, nikamwambia "sawa ntaliangalia". Basi kapika chakula Cha usiku, nmekula kias nmeshiba, tumefanya ya kufanya tena, nikaaga nikaondoka zangu. Ikawa kila siku ananijulia hali,ananambia kanimiss. sms nyngn nazijibu nyingine nazipotezea. Tukapotezeana

9. Baada ya miez 2, nikaja mtafuta nikamwambia nmemmiss.
Bila kunilaumu wala kunihoji maswali mengi akanambia kua kanimiss pia. Nikamwambia inakuaje sasa, akasema Yuko blidi, ila nimsubir kesho kutwa anamalizia. Atakua fresh, Nikasema sawa.

Baada ya siku 2 nishasahau kabisa, kanitafuta akinambia leo ndo leo kanimiss tukafanye. Nikasingizia kua Leo siko vizur kiuchumi, Sina bajeti ya lodge tufanye wikend. Akasema hapana, leo leo bhana niende Tukafanyie nyumban kwake.

Nikamwambia sio adabu, afu najiskia aibu maana pale kwake sijachangia chochote na kila nilipoombwa kuchangia sikufanya hivyo.

Akanambia nisiwe na wasiwasi niwe na amani, shimo la choo keshafunika tayar, Kama Ni kumsaidia ntamsaidiaga mbeleni maana nyumba yake bado inadai vitu vingi Sana kukamilika. Nikasema "sawa".

Basi nikaenda kwake, tukafanya ya kufanya, ila Sasa baada ya tendo mbu wakawa wamening'ata Sana makalioni na sehemu mbalimbali mpk vipele ukzingatia pale kwake hajaweka umeme na nyavu za mbu hajaweka bado. Basi baada ya tendo nikamwachia posho yake na ela ya kufunga nyavu za mbu. Akashkuru Sana, nikaaga nikaenda kwangu.

Baada Aya Hapo mambo yakaja kua sawa na mamaJ, nikampotezea tena.
akawa anapiga Simu, sipokei, akituma sms sijibu. Mawasiliano yakawa yamekufa.

10. Tumekuja kukutana Tena miezi imeshapita kwny maonyesho ya sabasaba mwaka huu katika pita pita za Hapa na pale mle uwanjani. uso kwa uso mdada huyu hapa Yuko na mwanae.

Ikabd tukae sehemu tunywe juice na tusalimiane, nikamwambia kua nmemmiss ratiba TU zinanibana. akasema anaelewa,nayeye pia kanimiss. Nikamwambia sawa inakuaje Sasa, akasema ananiskiliza Mimi TU. Nikamwambia Basi ngoja nikafunge ofisi,Kisha twenzetu, akasema sawa ila nikimaliza kufunga kwangu na yeye anaomba nimpeleke kwake akamuache mtoto wake ili awe huru. Nikasema sawa.

Nmemfikisha kwake, kampeleka mwanae nyumba ya jiran akacheze, nmebaki kitandani yeye Kaenda kuoga karudi. Dah! Kumuangalia, uchu ukatupanda mechi tukaianzisha pale pale. Tulikuja kustuliwa na mtoto wake anagonga sana kwa nje analia amefungiwa mlango. Ikabd tukatishe tumfungulie mtoto.

Baadae ananambia mwanae ana wiki tangu aje kutokea kwa Bibi ake, anaogopa sana Giza alizoea umeme uko. Usiku ukishaingia tu anajawa na uoga. anataka kua karibu na mama ake TU.

Nikamwabia kinachotakiwa sasa uvute umeme ,akasema umeme anapenda ila tatizo Ela maana mpk kafika alpofikia Kuna sehem nyngn bado anadaiwa madeni. Nikamwambia kwa sasa ntakusaidia sola system utumie kwa MDA (kesho kutwa ntaileta) , ila tafta Ela ya mita ukalipie mwenyewe, vifaa vya wayaring ntakupa Mimi. Akasema sawa atashkuru. Nikaoga, nikavaa, kumwachia posho yake, tukaagana nikaondoka.

Kesho kutwa ilipofika (siku ya kumpelekea Sola) Mambo yakawa mengi, Sola sikuipeleka. Na hata alivonitafuta sikujibu sms zake Wala kupokea Simu zake. Nikawa bize na mambo yangu. Tukawa tumepotezeana hivyo.

11. Sasa ile jumatatu ya tar 25 mwezi wa 7, asbh Niko zangu dukan Simu ya uyu mdada ikaita sana nikaipotezea ( najskia aibu nikiipokea ntajibu Nini). MDA si mrefu akaja kijana na bahasha ya kaki, anasema kapewa na yule mdada Yuko kwenye ile bajaji upande wa pili wa barabara.

Kutizama, nikamwona anafunua pazia la bajaji ananipungia mkono uku anatabasamu
Aisee nilijiskia aibu Sana,ikabd nimpigie Simu nimwambie kua nilikua bize sijaiskia ikiita. Akasema sawa anaelewa. Hiyo Ni fomu keshalipia tayar tanesco tangu tar 15 mwez ulopita, tanesco wamemwambia mita Yake iko tayar anaomba nimtekelezee ile ahadi yake ya vifaa ili wamuwashie umeme haraka. Nikasema sawa Haina shida ntakuja kwako jion tuonane na fundi wako anipe tathmini ya vifaa vyako. Akasema sawa asante, kisha akaaga, simu ikakatwa, bajaji ikawashwa na kuondoka.

Jion ilipofika nikaenda kwake, nmeonana na fundi wake kanipa karatasi ya tathimini ya vifaa, kesho Yake nikamwambia uyo fundi wake apitie dukn kwangu atakuta vifaa viko tayar nimpatie akamfungie umeme mdada. Kweli kesho Yake nikafanya kweli. Baada ya siku mbili mdada kanipigia sikupokea. Akanitumia sms Ya kunishukuru sana kua umeme umewaka tayar pia nije nimtembelee kanimiss sn. Nikamhaidi ntakuja.
Kiukweli Mambo yakawa mengi,kwaiyo sikwenda. Tukawa tumepotezeana.

12. Kanitafuta Tena juz wikend ya jumamosi (tar 30/07) akinitext "hellow, nmekumiss". Ikabd nimpigie, nikamwambia nmemmiss pia,inakuaje Sasa. Akasema Yuko kazin anamalizia nguo ya mteja, usiku niende kwake Kama sitojali. nikasema sawa.

Usiku Nmeenda kwake, aisee nmeshangaa sana mabadiliko ndani ya chumba chake alichokijenga.

-Umeme unawaka,
-Keshaweka Hadi tiles chini Hadi chooni, ameskim ukutani bado rangi tu.
-Kanunua kitanda kipya na godoro jipya, kile kitanda cha zamani kakifungua kaweka uvunguni,godoro anasema kaliuza.
Tukafanya ya kufanya nikamuachia posho Yake,nikaaga nikaondoka zangu.

NILIVOTOKA PALE SASA,
Kiukweli wakuu niliona aibu Sana. Maana nilijihisi nafs inanisuta sana kwa ninayomfanyia binti yule,

Nikikumbuka upuuz wangu wote nnaomfanyia huyu mdada tangu kule juu kuanzia safar namba 1 mpaka namba 12 ila bado mdada haoneshi kukasirishwa na mimi, kunilaumu Wala kunung'unika kwa lolote lile. Tena tukikutana ndo anatabasamu kabisa.
Yaani huyu mdada hatujawai gombana kwa lolote lile kabisa, she's always smilling.

Inafikia hatua nahisi anajua kabisa huyu mwanaume huwa ananitafuta anapokua na nyege zake tu, zikiisha anaingia mitini. Ila halalamiki,hafoki Wala kunung'unika yeye anafanya maendeleo yake TU,nimsaidie nisimsaidie yeye anasonga mbele tu.

Afu hapo hapo bado Anapata ujasiri wa kunikaribisha ndani kwake,kunipikia,kunitengea maji ya kuoga na kunipa tendo kabisa Kama mume wake wa ndoa ndani pale pale anakopambana kila siku kwa jasho lake kupajenga na kupaweka sawa.

Tangu juzi ananitext ananiomba niende kwake, anasema kanimiss. Namwambia ntakuja, ila siendi. Moyo unakua mzito Sana, nafs inanisuta.
kiukweli kichwan ananiachia maswali mengi Sana huyu mdada,
Sijajua huwa akikaa ananiwazia nn mm, maana simuelewi elewi kabisa.

Kuna MDA nawaza nimwambie TU atafute mwanaume mwingine wa maana tuachane, nahisi mimi namtesa TU kihisia (sijiskii kumpenda). Ila nikiangalia response kama nnamtesa mbona sipaoni maana yeye anatabasamu TU na tukiwa wote anafurahia sana company na mimi. Hachukii hata nimpotezee miezi kibao.

Hajawahi niomba ela ya kula,saluni, vocha, Wala nimchangie chochote kile kwa mwanae mdogo. Huwa Nampa Ela ya tunapokutana TU nakufanya mapenzi. Hii nikijitathimini naona sio fair kabisa.

Anatumia kisimu Cha tochi, tecno 301 tangu mwaka juz namuona nacho hicho TU. Mwaka Jana kimepasuka mfuniko,nikaahidi ntamnunulia mpya. Sijafanya hivyo. Amefunikia na cover TU isionekane, ila mfuniko uko vile vile kwa ndani umepasuka. Aibu naona Mimi.


Kiukweli wakuu Hapa Kichwa mpk kimestack,
-mpk Kuna MDA nafikiria huyu dada labda ni Jini,
- au Yuko na Mimi tu ila sio kwa ajenda za kimahusiano au mapenzi (honey trap). Yaan namuona yupo yupo TU Kama Hana Moyo vile.

- au hili tabasamu lake kila nnapomtenda Kuna kisasi kavilimbikiza Labda ananiandalia aje anipige pigo takatifu au vipi

Wakuu,
Kiukweli maswali kichwan Ni mengi kuliko majibu.

USHAUR wenu tafadhali
Natanguliza shukrani za dhati


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie nimefurahishwa na kujituma, malengo na jitihada za huyo Dada.

Kama hautojali, unaposema unamwachia posho mkimaliza, inakua ni kiasi Gani Cha pesa?
Mara nyingi ni Elfu 20

Ila Kuna siku natoa Elfu 15
Siku nyingine nikiwa nazo natoa mpk elfu 30

Mambo yakikaa vibaya Nampa hata elfu 10 anashukuru.

Yaan posho Haina kiwango maalum mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chamuhimu nikushauri ni uimarishe intelligence yako ili upate data zake vizuri.
Niliwai muuliza khs bwana alozaa nae,
Nikiwa nna wasiwasi jamaa Labda ndo anamfanyia maendeleo yote Yale.

Akanambia ni jamaa Ni dreva IT,
alimzalisha kipind Yuko kibaha kwa mama ake hivyo hawana mawasiliano kabisa na hachangii chochote khs mwanae.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom