Nina hamu sana ya kusikia kuna mabadiliko madogo/makubwa ya Baraza la Mawaziri, Ma RC's na DC's kuanzia sasa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,689
109,104
Nitafurahi mno nikisikia kuna mabadiliko haya kwani kwangu mimi GENTAMYCINE naona Overall Performance ya Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa sasa ni below standard (very poor)

Natumai kwakuwa Mteuwaji Mkuu huwa Ananisoma sana GENTAMYCINE na tuko nae hapa JamiiForums tena hii mida ya Saa 10 Kamili alfajiri hadi Saa 12 Kamili asubuhi huwa anashinda mno katika huu Mtandao basi atanielewa na itampendeza kupelekea kuchukua maamuzi haya ambayo nayatamani yatokee.
 
Kitu ambacho raisi wetu alikosea ni kusikiliza ushauri mbovu ambao umeirudisha nyuma nchi yetu katika baadhi ya maeneo muhimu kama umeme, mfumuko wa bei na ubadhilifu na udhibiti wa mali na fedha za umma.

Raisi alipaswa kuendelea na serikali ilokuwepo hadi uchaguzi upite wa 2025 ndipo afanye yale ambayo ndo ayapigania sasa.

Kufanya hivyo kungeondoa matumizi mengine makubwa ya kodi za wananchi kumtumia Paul Makonda kufanya kitu twaita kwa kiingereza "Whitewash".

Hichi ni kitendo cha kutumia maneno ya ulaghai, au vitendo ili kuficha (Cover-up) matendo au mienendo mibovu, makosa, au utendaji mbovu au kuwa tayari kubeba lawama kwa makosa yalofanywa na watu wengine.

Nchi yetu imefikia mtu mwenye nafasi na madaraka makubwa aweza kukiri wazi kwamba amemteua fulani baada ya usaili kufanyika kwenye baa!

Baraza la mawaziri ni watu muhimu sana katika mstakabali wa nchi kimaendeleo.

MaRC na MaDC ni watu ambao nafasi zao zatakiwa kuwa ni za kuchaguliwa.

Nchi yetu ni kubwa na ina watu zaidi ya milioni 65, hivyo umefika wakati wa kugawa madaraka ili mikoa na wilaya ziwe na uwezo wa kujiamulia aina ya miradi, mikakati na uchumi (local economy) ambao waweza kunyanyua mikoa na wilaya hizo bila kuegemea sana bajeti kuu ya serikali ambayo yaweza kuelekezwa katika miradi mikubwa ya kimkakati.

Hizi 4Rs za sasa ziondolewe na badala yake tuwe na serikali yenye 4 Rs zingine za uongozi ambao ni "reliable", "resilient", "responsible" na "robust" katika utekelezaji wa maamuzi na shughuli zake.
 
Ungetamani kuona sura gani mpya baraza la mawaziri?
Luhaga Mpina

Fred Lowasa

Mrisho Gambo

John Kanyasu

Cosato Chumi

Jasson Rweikiza

Zainabu Katimba

Rose Tweve

Ritta Kabati

Sophia Mwakagenda

Hawa ni baadhi tu lakini raisi pia ajaribu kuteua mawaziri kuongoza wizara kulingana na sifa walo nazo.
 
Nitafurahi mno nikisikia kuna mabadiliko haya kwani Kwangu Mimi GENTAMYCINE naona Overall Performance ya Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa sasa ni below standard ( very poor )

Natumai kwakuwa Mteuwaji Mkuu huwa Ananisoma sana GENTAMYCINE na tuko nae hapa JamiiForums tena hii mida ya Saa 10 Kamili alfajiri hadi Saa 12 Kamili asubuhi huwa anashinda mno katika huu Mtandao basi atanielewa na itampendeza kupelekea kuchukua maamuzi haya ambayo nayatamani yatokee.
N ipigie debe kusudi niteuliwe kuwa "Waziri wa Fedha."
 
Luhaga Mpina

Fred Lowasa

Mrisho Gambo

John Kanyasu

Cosato Chumi

Jasson Rweikiza

Zainabu Katimba

Rose Tweve

Ritta Kabati

Sophia Mwakagenda

Hawa ni baadhi tu lakini raisi pia ajaribu kuteua mawaziri kuongoza wizara kulingana na sifa walo nazo.
Mpina na fred kwa maoni yako wanafaa wizafa zipi?
 
Kitu ambacho raisi wetu alikosea ni kusikiliza ushauri mbovu ambao umeirudisha nyuma nchi yetu katika baadhi ya maeneo muhimu kama umeme, mfumuko wa bei na ubadhilifu na udhibiti wa mali na fedha za umma.

Raisi alipaswa kuendelea na serikali ilokuwepo hadi uchaguzi upite wa 2025 ndipo afanye yale ambayo ndo ayapigania sasa.

Kufanya hivyo kungeondoa matumizi mengine makubwa ya kodi za wananchi kumtumia Paul Makonda kufanya kitu twaita kwa kiingereza "Whitewash".

Hichi ni kitendo cha kutumia maneno ya ulaghai, au vitendo ili kuficha (Cover-up) matendo au mienendo mibovu, makosa, au utendaji mbovu au kuwa tayari kubeba lawama kwa makosa yalofanywa na watu wengine.

Nchi yetu imefikia mtu mwenye nafasi na madaraka makubwa aweza kukiri wazi kwamba amemteua fulani baada ya usaili kufanyika kwenye baa!

Baraza la mawaziri ni watu muhimu sana katika mstakabali wa nchi kimaendeleo.

MaRC na MaDC ni watu ambao nafasi zao zatakiwa kuwa ni za kuchaguliwa.

Nchi yetu ni kubwa na ina watu zaidi ya milioni 65, hivyo umefika wakati wa kugawa madaraka ili mikoa na wilaya ziwe na uwezo wa kujiamulia aina ya miradi, mikakati na uchumi (local economy) ambao waweza kunyanyua mikoa na wilaya hizo bila kuegemea sana bajeti kuu ya serikali ambayo yaweza kuelekezwa katika miradi mikubwa ya kimkakati.

Hizi 4Rs za sasa ziondolewe na badala yake tuwe na serikali yenye 4 Rs zingine za uongozi ambao ni "reliable", "resilient", "responsible" na "robust" katika utekelezaji wa maamuzi na shughuli zake.
Tatizo ni ccm tu na watu wake hakuna kingine.
 
Ila humohumo CCM wapo watu ambao wamesoma uzuri tu.

Luhaga Mpina amesoma uchumi uzuri tu tena amesoma pale Strathclyde Scotland si chuo cha kubahatisha.

Hawa watu wapo humohumo CCM wapewe nafasi ya kuonyesha uwezo wao, wakishindwa ndipo wazodolewe.

Hayati Mwalimu Nyerere aliwahi kusema upinzani utatoka ndani ya CCM na si nje.
 
Nitafurahi mno nikisikia kuna mabadiliko haya kwani kwangu mimi GENTAMYCINE naona Overall Performance ya Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa sasa ni below standard (very poor)

Natumai kwakuwa Mteuwaji Mkuu huwa Ananisoma sana GENTAMYCINE na tuko nae hapa JamiiForums tena hii mida ya Saa 10 Kamili alfajiri hadi Saa 12 Kamili asubuhi huwa anashinda mno katika huu Mtandao basi atanielewa na itampendeza kupelekea kuchukua maamuzi haya ambayo nayatamani yatokee.
Ili ipige hatua za maana za maendeleo nchi inahitaji 'overhaul'. Hi toa huyu weka huyu haitusaidii.
 
Back
Top Bottom