Rais Magufuli afanya mabadiliko madogo katika baraza la Mawaziri, pia ateua Balozi na Makatibu wakuu

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,320
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 08 Januari, 2019 amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Uteuzi huo utatangazwa moja kwa moja kupitia Redio, Televisheni na Mitandao kuanzia saa 6:45 mchana huu kutoka Ikulu, Dar es Salaam


UPDATES


Katibu Mkuu Kiongozi anasema;

Kituo cha uwekezaji Tanzania TIC, rais ameagiza kihamishwe kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kihamishiwe kwenda ofisi ya Waziri mkuu ili kuongeza msukumo katika Maswala ya uwekezaji hapa mchini.

Vilevile rais amemteua Angela Kairuki kuwa Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu wa kusimamia uwekezaji. Hii ni Wizara mpya

Rais pia amemteua Dr. Dotto Biteko kuwa Waziri Kamili wa Wizara ya Madini.

Stanslaus Nyongo ataendelea kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Madini pekee, kabla ya hapo Manaibu Waziri walikuwa wawili.

Kwa upande wa Makatibu Wakuu, Rais Kateua Makatibu wakuu wanne

Katibu mkuu Tamisemi ni Joseph Nyamhanga ambaye amechukua nafasi ya Yombe

Katibu mkuu Wizara ya Afya ameteuliwa Zainab Chaula, kabla ya uteuzi alikuwa TAMISEMI.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi ameteuliwa Elius Mwakalinga

Sera na uwekezaji kateuliwa Doroth Mwaluko

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI ameteuliwa Doroth Gwajima atakayeshughulikia Afya

Naibu Katibu Mkuu Utumishi ameteuliwa Francis Michael wa chuo kikuu UDSM

Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Ulinzi imefutwa.

Rais amemteua Dr. Mpoki kuwa Balozi, kituo chake kitatangazwa baadae. Kabla ya uteuzi alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya

Rais amefungua ubalozi wa Tanzania nchini Quba

Rais amemteua Prof. Faustine Kamuzora kuwa Katibu Tawala mkoa wa Kagera, amechukua nafasi Kamishna Diwani Athumani aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU.

HABARI ZAIDI, SOMA...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 08 Januari, 2019 amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na kufanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wa wizara na taasisi za Serikali.

Uteuzi wa viongozi hao uliotangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam ni kama ifuatavyo;

Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Anjellah Kairuki kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji.

Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Waziri anayeshughulikia masuala ya uwekezaji kwa lengo la kuongeza msukumo na kuimarisha usimamizi wa masuala ya uwekezaji hasa baada ya kuamua Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kihamishiwe Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kabla ya uteuzi huo Mhe. Kairuki alikuwa Waziri wa Madini.

Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Doto Biteko kuwa Waziri wa Madini. Kabla ya uteuzi huo Mhe. Biteko alikuwa Naibu Waziri wa Madini.

Kufuatia uteuzi huo Wizara ya Madini sasa itakuwa na Naibu Waziri mmoja ambapo Mhe. Stanslaus Nyongo anaendelea na wadhifa wake.

Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Joseph Nyamuhanga kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Nyamuhanga alikuwa Katibu Mkuu Ujenzi, na anachukua nafasi ya Mhandisi Mussa Iyombe ambaye amestaafu.

Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Zainabu Chaula kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (anayeshughulikia afya). Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Chaula alikuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (afya).

Mhe. Rais Magufuli amemteua Arch. Elius Mwakalinga kuwa Katibu Mkuu Ujenzi. Kabla ya uteuzi huo Arch. Mwakalinga alikuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na anachukua nafasi ya Mhandisi Nyamuhanga ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu TAMISEMI.

Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Dorothy Mwaluko kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji). Kabla ya Uteuzi huo Bi. Mwaluko alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Dorothy Gwajima kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (Afya). Kabla ya uteuzi huo Dkt. Gwajima alikuwa Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Francis K. Michael kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Francis K. Michael alikuwa Mhandiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Mpoki Ulisubisya kuwa Balozi.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Ulisubisya alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (akishughulikia afya). Kituo cha kazi cha Dkt. Ulisubisya kitatangazwa baadaye.

Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Faustin Kamuzora kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.

Kabla ya Uteuzi huo Prof. Kamuzora alikuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Athumani Diwani Msuya ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Uapisho wa viongozi hao utafanyika kesho tarehe 09 Januari, 2019 saa 3:30 asubuhi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameifuta nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi. Nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa Bi. Immaculate Ngwalle ambaye amestaafu.

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amefanya uamuzi wa kufungua Ubalozi Mpya wa Tanzania nchini Cuba. Balozi wa Tanzania nchini Cuba atateuliwa baadaye.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

08 Januari, 2019
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 08 Januari, 2019 amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.
Uteuzi huo utatangazwa moja kwa moja kupitia Redio, Televisheni na Mitandao kuanzia saa 6:45 mchana huu kutoka Ikulu, Dar es Salaam

UPDATES


Katibu Mkuu Kiongozi anasema;

Waziri wa nchi Ofisi ya waziri mkuu wa kusimamia uwekezaji ameteuliwa Anjela Kailuki Rais John Magufuli amemteua aliyekuwa waziri wa Madini, Angellah Kairuki kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji)

Rais pia amemteua Biteko kawa Waziri Kamili wa madini

Naye Nyongo kateuliwa kuwa naibu waziri madini.

Kwa upande wa makatibu wa kuu, rais Kateua Makativu wakuu wanne

Katibu mkuu Tamisemi ni joseph Nyamhanga amechukua nafasi ya Yombe

Katibu mkuu afya Zainab chaula alikuwa tanisemi

Katibu mkuu ujenziElius Mwakalinga

Sera na uwekezaji kateuliwa Doroth Mwaluko

Naibu katibu mkuu Tamisemi ni Doroth Gwajima

Naibu katibu mkuu utumishi ni Francis Michael wa chuo kikuu UDSM

Nafasi ya Naibu katibu mkuu ulinzi imefutwa.

Rais amemteua Balozi Mpoki kituo chake kitatangazwa baadae. Alikuwa akatibi mkuu afya

Rais amefungua ubalozi wa Tanzania nchini Quba

Rais kateua katibu tawala Faustine Kamzola kaenda Kagera baada ya Athumani kuteuliwa takukuru.
 
Back
Top Bottom