Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
Dereva, konda waua abiria
Na Mwandishi Wetu (Mwananchi)
POLISI mkoani hapa wanamshikilia dereva na kondakta wake wa basi dogo la abiria aina ya Toyota Coaster kwa tuhuma za kumuua abiria, Herry Losujak Saningo (34) aliyekuwa anadai arejeshewe chenji yake ya Sh600 baada ya kulipa nauli.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Matei Basilio, alisema baada ya kumpiga na kumuua abiria huyo, watuhumiwa hao walikamatwa wakimtupa katika eneo la makaburi ya Kaloleni jijini hapa.
Kamanda Basilio alisema, tukio hilo lilitokea juzi saa 1.30 jioni baada ya gari hilo kurejea jijini hapa likitokea Moshi mkoani Kilimanjaro, ambako hufanya safari zake za kila siku.
Wakielezea tukio hilo, ndugu wa marehemu ambao walikuwa wamesafiri naye kutoka eneo la Kingori wilayani Arumeru kuja mjini hapa, walisema ugomvi baina ya marehemu na kondakta wa basi hilo, ulianzia katika eneo la Mianzini wakati alipoanza kudai chenji yake.
William Mandaine ambaye ni shemeji wa marehemu, alisema wakiwa kwenye gari hilo, Saningo ambaye alikuwa ameandamana na mkewe, Glory Herry, alitoa Sh2,000 kama nauli.
Mandaine alisema nauli ya kutoka Kingori hadi Arusha mjini ni Sh700 na hivyo aliomba kurejeshewa Sh600, kitu ambacho kondakta alikataa.
Baada ya kumuomba kwa muda mrefu tulipofika Mianzini ambapo ndio mwisho wa safari yetu, tulianza kushuka na ndipo Saningo alikumbushia kupewa Sh600 yake, na ndipo kulitokea kutoelewana baina yao. Dereva kuona hivyo, alishuka kwenye gari hilo kuingilia, alisema Mandaine.
Alisema badala ya dereva huyo kusuluhisha ugomvi huo, naye alimuunga mkono kondakta wake kuwa kamwe hawarejeshi fedha, kwani wao ndio wanadai na hapo hapo walimbeba Saningo na kumrejesha kwenye gari na kuondoka naye kwa kasi.
Mandaine alisema, baada ya kuondoka na Saningo, wao walikodi teksi na kuanza kuwafuata kwa nyuma lakini kutokana na mwendo kasi ya gari hilo, walipotezana katikati ya jiji, hivyo wakaamua kwenda polisi.
Alisema wakiwa polisi, waliliona gari hilo likiwa katika makaburi ambayo yapo jirani na Kituo Kikuu cha Polisi mjini hapa na ndipo nao walipokwenda na kukuta tayari polisi wamefika.
Mara baada ya kuwakuta polisi, ndipo tulipewa taarifa kuwa kondakta na dereva huyo wameonekana wakimtupa mtu nje ya gari na baada ya kufuatilia ndipo tulimkuta Saningo akiwa katika hali mbaya na baadaye alifariki, alisema.
Kwa mujibu wa taarifa ya awali ya uchunguzi wa kifo hicho, Saningo alifariki kutokana na jeraha kubwa kichwani baada ya kupigwa na kitu kizito kilichotoboa sehemu ya kichwa.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Basilio, alisema polisi bado inafanya uchunguzi ili kujua chanzo cha kifo hicho lakini taarifa ya awali inaonyesha marehemu alipigwa na kitu kizito kichwani.
Tunaandika maelezo na yakikamilika tutawafikisha mahakamani watuhumiwa hao hiki ni kitendo cha kinyama kamwe hatuwezi kukaa kimya, alisema Kamanda Basilio
Marehemu huyo, ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kiranyi, Wilaya ya Arumeru ameacha mjane na watoto wawili ambao ni Jesca anayesoma darasa la pili na Linda anayesoma shule ya awali.
Kutokana na tukio hilo, chama cha wamiliki wa magari ya abiria Arusha na Kilimanjaro (Akiboa) na chama cha madereva mkoa wa Arusha (Umma) wamelaani kwa nguvu kitendo kilichofanywa na dereva huyo na kondakta wake.
Katibu Mkuu wa Akiboa, Locken Adolf, alisema jana kuwa wamepokea kwa mshituko tukio hilo na wanatoa pole kwa familia ya marehemu.
Tukio hilo limekuja siku chache baada ya dereva mwingine wa gari dogo la daladala maarufu, kama kifodi jijini hapa, kumjeruhi kwa sime askari ya kikosi cha usalama barabarani, PC Hamad.