Kumbe Preta wa Arusha ni kidume
na mwandishi Maalum.
[/CENTER]
Mtu maarufu humu jamvini anayetambulika kwa Jina la Dada Preta amegundulika kuwa ni Kidume cha mbegu ambaye ana wake watatu pamoja na watoto 11. mtu huyo amegundulika kwa jina la Athumani kambambili mkaazi wa Yaeda chini Jijini Arusha. Kutokana na tatizo la ukata pamoja na majukumu ya kutunza familia, Bwana Athumani (au Da' Preta kama alivyozoeleka humu Jamvini) kwa kushirikiana na Swaiba wake wa Karibu jina tunalihifadhi (ambaye jamvini amezoeleka kwa jina la Pi Jei) walibuni mbinu ya kujipatia kipato kutoka kwa memba wakware ambao masaa yote wanawaza kuduu.
Habari kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika zinapasha kuwa Bwana Athumani amekubaliana na Rafikiye (Pii jei) kuwa awe anampigia chapuo kwa wale wote watakaoonekana kutaka kumpata "Da' Preta" na kwamba Pii Jei ndiye amepewa jukumu la kupokea huo mshiko kutoka kwa wakware pamoja na kuwaambia venyu ya kukutana na "Da' Preta". imebainika kuwa wana mtandao mkubwa kwani kuna dada ambaye ni Mhudumu wa Pub moja maarufu Jijini Arusha ambaye amepewa jukumu la kuongea na Mkware yeyote anayetaka kulonga na "Da' Preta".
Vyanzo vyetu vimezidi kupasha kuwa Bwana TANMO alipojaribu kurusha kete yake kwa gia ya kwamba yeye ni fukara lakini yuko tayari kumpenda "Da' Preta" mpaka kifo kiwatenganishe, alipingwa vikali na Bana Pi Jei ambaye alimtaka akauze shamba lake la urithi ndipo ataweza kusikilizwa ombi lake. bwana mtu Chake ambaye alijitanabaisha moja kwa moja kwamba ana pesa anasemekana kukubalika zaidi na Ndugu Pii Jei ambaye anajifanya kumpa maujanja zaidi namna ya kumnasa "Da' Preta" ili Mtu Chake aingie kingi na kutoa Mshiko wake. tutaendelea kufuatilia kwa ukaribu na tutawajilisha iwapo Mtu Chake ataingizwa mjini ama la.