Pole sana Marytina. Kwanza nikushukuru kwa kuwa na nia hiyo ya kutaka kumwambia boyfriend wako.
Ushauri wangu uko hivi, naomba ufuatane nami:
Mimi ni Mkatoliki, kanuni za kanisa zinasema ukienda kwa Padri au askofu ukatubu dhambi zako kwa kuzitamka moja baada ya nyingine, halafu padre akakupatia kitubio, ukafanya kitubio kwa sala kadhaa ambazo amekuagiza, ukarudi kwake kumwambia umefanya kitubio sasa Mungu akusamehe dhambi zako, basi kwa moyo mweupe kabisa ukiondoka pale....umesuuza moyo wako maana unajua Mungu amekusamehe kwakuwa umezisema dhambi zote, umeagizwa kusali baadhi ya sala na umetimiza na kisha kuomba msamaha! Kwa kupitia mchakato huo, roho yako, akili yako na generally saikolojia yako inakubali kuwa umesamehewa dhambi zako. Leo hii usingekuja kutueleza maana wewe huna dhambi tena.
Kwa kuwa dhehebu lako ni tofauti, mnaambiwa kuungama dhambi hadharani, na wewe unaona ni vigumu kwa sasa kusimama kanisani ukatamka wazi, na kwakuwa roho inakuuma kwa kuhama kanisa ulilolipenda sana, basi ni vema ukatibu mambo yote haya: kutubu dhambi, kusema ukweli, kurudi kanisani - kule ulikohama na kujenga mahusiano yako na mpenzi wako:
1. Ongea na Mpenzi wako kwamba kuna kitu unataka kuongea naye ukiwa na Mchungaji wa Kanisa Kuu (ulikohama).
2. Mweleze mpnz wako nia yako ya kuolewa naye, kama yupo tayari kufunga ndoa na wewe akueleze ni lini.
3. Kama mpnz wako yupo tayari kwa hizo hatua 1 na 2
4. Ongea na Mchungaji huyo kwamba una neno unahitaji kumwambia ukiwa na mchumba wako.
5. Panga siku ya kwenda wewe na mpnz wako kwa Mchungaji
6. Siku hiyo kuwa jasiri kusimulia kama ulivyosimulia humu ndani.
7. Hdithi yako ihitimishwe na kusema: Mpnz wangu, baada ya kuokoka, nimeona ni vema kuwa muwazi kwako na kwa mchungaji ili niwe huru, nirudi kanisani hapa na toka leo siwezi kusema uongo kwako. Mkumbatie mpnz wako, lia kidogo (najua utalia tu)
8. Ratiba itakayofuata anaifahamu Mchungaji.
N.B: Hakikisha Mchungaji ni mtu wa makamo, siyo kijana na awe ni mtu ambaye anaheshimika. Ushauri atakaoutoa Mchungaji utakuwa wa mwisho. Mpnz wako hawezi kukuacha kamwe! Ndoa itadumu, utafunguliwa kutoka minyororo ya shetani. Unajua unaweza ukawa unasali lakini dhambi ya uzinzi bado inakusumbua, ndiyo maana humo ndani nimeona unapitiwa na kusema,...."nikiharibikiwa utanitafutia mume?'" sijapenda sana hapo, maana wewe unapenda yeyote?? Lakini kwakuwa nafahamu maisha uliyopitia na maisha unayoyataka nimegundua tatizo lako. Ndiyo maana ushauri wangu nataka utue mzigo huo kwa mchungaji.
9. Weka ratiba ya kufanyia kazi ushauri ulipewa na wadau humu ndani!
Hao madada wa Kenya, hawatakudhuru kwa lolote ukifanya haya mambo. Kwanza, utakuwa wewe siyo mdhambi tena. Siyo mwongo tena. Humwogopi Mpnz wako tena. Mpnz wako ameshapewa ushauri wa kutosha na mchungaji na hawezi kukiuka, imani ya dini ni silaha tosha. Utakuwa unawachukulia kama watu wa dunia, usijichanganye nao! Wakikufuata waeleze wewe siyo wa Nairobi, you are a new born again and God fearing Lady!
May the Almighty God Bless You!