Nimewahi kuwa changudoa, nimjulishe?

Nimewahi kuwa changudoa, nimjulishe?

mmh ina maana simfai kuwa mkee wa mwanaume yeyote ikiwa ukweli utajulikana????

hata kama ulijiuza usiseme ulijiuza, kama kuna ulazima wa kusema kanisani wewe sema ulipitia magum tu. kumbuka si lazima useme kila kitu, mungu anaelewa kila kitu, kutamka hivyo tu inatosha kuonesha majuto na kutubu, toba inapatikana mbele za mungu wako, si mbele za wanadamu. ulishawahi kuona mchungaji anatoa ushuhuda kuwa alitembea na mke wa mtu? wasikupump wewe ujivue nguo mbele zao ili wapate cha kuongea, sema na mungu wako tu. na hauna haja ya kuwaogopa hao washirika wako wa zamani, wewe ni mtu mpya!
 
Mabinti wengi sasa mnaokoka ili kuolewa, kujifanya kwamba mmebadilika kumbe mnataka tu kuolewa, mkiolewa tu mnarudia fani yenu,ndio maana nikasema kunguru huwa hafugiki, ipo siku atarudi porini.
sijui nitumie maneno gani unielewe ila najutia
najutia kwa nini sikumwambia siku ya kwanza alipoonesha kunipenda....nina matatizo makubwa matatu ikiwa ntaachika

1.To be honest najihisi na najiona kama nimechoka sana kufikiri kwa ajili ya maisha yangu......ubongo kama unashrink
so naitaji mtu wa kufikiri kwa niaba yangu, mtu wa kuplan na kuweka au to monitor mikakati kwa niaba yangu as i am too tired.
Yaan nalitumia kanisa kama sehemu ya kujiburudisha na kujifariji kwa kuwa nakutana na watu wenye shuhuda mbalimbali.Wikiend naweza kwenda kanisani hata mara mbili yaan asubuhi kanisa hili then jioni kanisa lingine.

2.Nimekutana na wanaume wengi sana na kuna wakati nilifikiri siwezi kupenda ila huyu Mmasai ni right person kuwa na mimi na anafikiri, ana panga na kumonitor kwa niaba yangu.Si tajiri na sio kwamba sitongozwi na wanaume matajiri hapa ARUSHA na NAIROBI, nimependa sana na naamin nkiachika ntahangaika maisha yangu yote duniani.

3.Natakiwa niwe na mume anayejali sana kwa maana mimi ni rahisi sana kuanguka.(SI KURUDI KWENYE UCHANGUDOA BALI KUJIINGIZA KWENYE BIASHARA YEYOTE CHAFU)........kumbuka my uncle,dad and the entire circle nlliyokulia bado ipo na ipo tayari kunisaidia na wanataka niache kazi nifanye biashara.Huko kwenye biashara ndiko michezo yote michafu hiubuka.......kurushana, kudhulumiana, kuporana, kutumiana majambazi, kutekeana dili ni uchafu usioongeleka.So naitaji mwanaume wa kuwa nami kiimani na siyo wa kunikwaza nije kujikuta narudi nyuma
 
Hiv hujui wanaume sometimes wanaingia kwenye mahusiano na wanawake wanahisi kabisa huyu demu past yake alikuwa hajatulia lakin hawajisumbui kuhulidhia hayo mambo ya zamani.wadada wengi hata hapa tanzania wanao soma chuo wanajiuza kipindi wakiwa mavyuoni kwa sababu tofauti mengi ikiwa maisha ya kuiga kutaka simu,bumu limechelewa wakati huo wabunge wamejaa mji mzima na kuomba marks kwa waalimu wakisha feli mitihani,semista moja naweza kutembea na wanaume zaid ya kumi lakin kwa sababu ni mwanachuo haitwi changudoa.kwahyo nauyo akipata mwanaume aanze kumwambia namna alivyokuwa akiishi chuoni?
Kuna sehemu PAUL anasema ukifika sokoni usimuulize muuzaji miogo au nyanya anazouza amevipata wapi cause vingine inawezekana ameiba ukijua kwamba aliiba ndio akaja kuuza utajisikia hukumu na kuingia hatiani.ukianza kumwambia mume wako ulikuwaje huko nyuma utamwalibu kisaikolojia na hata siku umechelewa bahati mbaya simu ikazma utaanza kumpa wasiwasi nakuanza kufikiri kwamba machanguadoa hawaachagi kabisa kazi yao.Cha muhimu ni kuwa serious na MUNGU wako ile neema ya kristu itakufunika na utapata kibali zaidi kwahyo bwana.(biblia inasema njia za mtu zikimpendeza MUNGU yeye humpatanisha na hata adui zake).to be born again it means your new species your past has nothing to claim in you.Inawezekana mchunguji wako anakubaliki sana anavyohubiri lakin akikupa historia yake ya nyuma unaweza ukakiimbia inawezkana alikuwa mteja mzuri wa machangudoa.GOD qualify unqualified people for HIS own glory.
 
hapo ndo tunapotofautiana waislam na wakristu.... kutubu......uchangu wako ulioufanya hujamkosea mtu....umemkosea MUNGU ask forgiveness to ur almighty GOD na si kwa mchungaji wala nani....once mungu akikusamehe haina haja ya kujitangaza kwa binadam kwan nas tu wakosefu mbele yake

kama ungeniibia Jose wangu basi ningekushauri uje uniombe radhi kwa wizi wako and then kwa MUNGU WAKO
 
Last edited by a moderator:
Ingekuwa ni mimi, ningeprefer uniambie ASAP. Ila watu tunatofautiana sasa....

Kama ni mtu anayeongozwa ama kuyumbishwa na hisia na maneno ya watu....huyo itakuwa ni rahisi kumuelezea na kumbembeleza pale atakapoujua ukweli yeye mwenyewe....

Ila a rational person hatoelewa...better get it over with mapema.
 
We mwanamke mbona hutaki kujibu kama ulipima?!!
ndio ndio nshapima ndio maana nawaza familia na tulishasex mara kadhaa ukumbuke nlipoanza naye uhusiano hatukuwa watu wa kanisa
 
nashukuru kwa ufafanuzi mkuu, si unajua maneno ya kuskia!...sasa unapopata firsthand info kama hivi unaelimika. vipi kuhusu k kuwa used sana, yaani inalegea sababu inatumika sana...kuna ukweli wowote?

hamna jambo kama hilo na huwezi mjua muuzaji kwa maumbile ya uke
 
My advise, think it through before you make any stupid decisions that may take u back to that devilish way o hustle Ila this tyme itakua unafanya kuondoa stress!
Maana kosa si kosa if it was for the right reason! But this kujianika might cost u big time!
Nahc nimeshawahi kukuona kiambuu!

sio rahisi cz tulikuwa tukiprefer hotels na sio madanguro au barabarani
 
hapana dada, lengo siyo kukuumiza, nilikuwa namjibu huyo jamaa niliemquote, kiutani tu, tunajua wewe ni mchumba wa mtu kwa sasa.

so unaweza kuoa msichana kama mimi au kumpigia jamaa yako chepuo amuoe x-changudoa? i am asking kindly!!!!!!!!!
 
Ningekushauri uweke wazi kila kitu tu dada yangu.
 
Pia stop blaming yourself it was the prevailing situation which forced and it exists no longer so be open please.
 
Ingekuwa ni mimi, ningeprefer uniambie ASAP. Ila watu tunatofautiana sasa....

Kama ni mtu anayeongozwa ama kuyumbishwa na hisia na maneno ya watu....huyo itakuwa ni rahisi kumuelezea na kumbembeleza pale atakapoujua ukweli yeye mwenyewe....

Ila a rational person hatoelewa...better get it over with mapema.

mapema ni kumwambia na hapo lazma niachike na staki hilo litokee
 
so unaweza kuoa msichana kama mimi au kumpigia jamaa yako chepuo amuoe x-changudoa? i am asking kindly!!!!!!!!!

siku hizi mapenzi yanavyoanza ni tofauti na zamani. sasa hivi unakutana na mtu sehem, say JF, mnazoweana, mnabadlishana namba, mnaanza kuongea nje ya JF, mnavutiana baada ya kuona interest zinaendana, mnakutana, mnagegedana, baada ya hapo kuna uwezekano mkapendana bila kukua mwenzako katokea wapi. ikitokea mahusiano yakaota mizizi mnataka muowane kila mtu anaanza kumpeleleza mwenzake kimyakimya, nikiridhika na tabia zake kwa sasa, wala siangalii ya miaka hiyo naoa.
 
kwani huyo mchumba wako unazikwa nae? nilichogundua hapo we unaogopa kuachwa,lakin hakuna kitu kizuri dunian kama kuishi na amani moyoni, jitahidi kumuandalia mazingiria ya kumueleza ukweli. Bora umuweke huru sasa hivi kuliko kusubiri hadi ndoa halafu akajua kupitia watu wengine
 
Ningekushauri uweke wazi kila kitu tu dada yangu.

nkiweka wazi ntaachika tu hamna mwanaume anayekubali kuona x-changudoa
staki kuachuka kwa kuwa:

1.To be honest najihisi na najiona kama nimechoka sana kufikiri kwa ajili ya maisha yangu......ubongo kama unashrink
so naitaji mtu wa kufikiri kwa niaba yangu, mtu wa kuplan na kuweka au to monitor mikakati kwa niaba yangu as i am too tired.
Yaan nalitumia kanisa kama sehemu ya kujiburudisha na kujifariji kwa kuwa nakutana na watu wenye shuhuda mbalimbali.Wikiend naweza kwenda kanisani hata mara mbili yaan asubuhi kanisa hili then jioni kanisa lingine.

2.Nimekutana na wanaume wengi sana na kuna wakati nilifikiri siwezi kupenda ila huyu Mmasai ni right person kuwa na mimi na anafikiri, ana panga na kumonitor kwa niaba yangu.Si tajiri na sio kwamba sitongozwi na wanaume matajiri hapa ARUSHA na NAIROBI, nimependa sana na naamin nkiachika ntahangaika maisha yangu yote duniani.

3.Natakiwa niwe na mume anayejali sana kwa maana mimi ni rahisi sana kuanguka.(SI KURUDI KWENYE UCHANGUDOA BALI KUJIINGIZA KWENYE BIASHARA YEYOTE CHAFU)........kumbuka my uncle,dad and the entire circle nlliyokulia bado ipo na ipo tayari kunisaidia na wanataka niache kazi nifanye biashara.Huko kwenye biashara ndiko michezo yote michafu hiubuka.......kurushana, kudhulumiana, kuporana, kutumiana majambazi, kutekeana dili ni uchafu usioongeleka.So naitaji mwanaume wa kuwa nami kiimani na siyo wa kunikwaza nije kujikuta narudi nyuma
 
mapema ni kumwambia na hapo lazma niachike na staki hilo litokee

Unakosea na utakosea sana kung'ang'ania jambo (yaani huyo mchumba) kwa nguvu na akili zako. Kwa kuwa umeokoka naomba umtangulize Mungu, yeye ni mkubwa kuliko wanadamu wote anajua unahitaji mume wa namna gani na anao uwezo wa kukupa huyo mume. Kwa hiyo, funguka kila kitu ili mmasai akufahamu kwa undani.
 
mapema ni kumwambia na hapo lazma niachike na staki hilo litokee

Unaongea kama mtu ambaye amekuja akiwa tayari anajua every possible course of action and its consequences....

Unahitaji ushauri gani? Tukupeti peti tukwambie "Its gonna be okay?"
 
Huna haja ya kusema chochote we tulia tu. Hivi ungekua umetoa mimba kumi ungesema? Kwa kuwa umeamua kubadilika hata Mungu atakulinda.
 
Back
Top Bottom