AZUSA STREET
JF-Expert Member
- Oct 31, 2013
- 2,007
- 1,898
dada, Mungu akusaidie. ninaomba usipate shida hivyo, maisha yako yapo mikononi mwa Mungu si mikononi mwa mwanadamu. mwanaume bora ataletwa na Mungu sio wanadamu. wewe mwangalie Mungu, haukuwa hata na umuhimu wa kuhama kanisa, ulitakiwa kubaki tu Mungu atakusaidia, kama kuna mtu atavujisha mwache avujishe, hata katika kuvujisha huko Mungu atakusaidia tu. hayo ni maisha ya zamani. sisi sote tulikuwa malaya sana, nimelala na wanawake wengi sana na nina watoto nje ya ndoa wengi, lakini ilifika kipindi nikaamua kumrudia Mungu, nimebadilika, nikikutana na mtu aliyekuwa malaya zamani, simhukumu kwa mambo yake ya zamani.baada ya matatizo yote ya utotoni kwa sasa nimekuwa mpole sana
nilikuwa kiongozi wa vijana kanisani ila nlilazimika kuhama baada ya MKENYA MDADA flani kuanza kuhudhuria huduma ya hapa kanisani.
BF alinishangaa kwani nahama kanisa ninaloheshimika kwa namna nlivyowaongoza vijana na mchungaji aliingilia akinitaka nisihame....mwishowe nikahama kilazima mkaanza kusali kikanisa kidogo njee ya mji....nayaona maisha yangu yoote yamejaa uongo nateseka sana
ya kale yamepita, tazama yamekuwa mapya. unachotakiwa kufanya, rudi palepale kanisani, wewe fanya mambo mema ili matendo yako yakutetee, hata mtu akisema ulikuwa changu kwa kuona matendo yako atasema ohhh lakini amebadilika kabisa sio kama yule wa zamani. wanawake wengi wanaoolewa walishawahi kufanywa na wanaume wengi sana, tunaoa basi tu. sisi wanaume pia tumelala na machangu wengi tu. mimi binafsi nimelala na machangu rundo, nimelala na wahudumu wa hoteli rundo, nimelala na wahudumu wa migahawa rundo....machangu wa kuwalipa kabisa rundo hadi wengine nikikutana nao siwakumbuki sura, na hata kama kanisani kwangu mtu atasema nililala na mimi, nitasema ohhh really, kumbe nilishawahi kulala na wewe, lakini nitamwambie siku hizi nimeokoka siko vile tena moyo wangu umebadilika, matendo yangu yamebadilika sasaivi nina Yesu na kwakuangalia matendo yangu yeye mwenyewe hata mdomo hatafungua na hata akifungua hatakuwa na madhara yeyote kwangu. watu wote sisi tulikuwa waovu tu zamani bila neema ya Mungu tungeshakufa zamani. wewe hauko tofauti na wanadamu wengine waliokosea sana, cha muhimu tu unatakiwa kujitahidi umwombe Mungu aondoe tamaa ya uzinzi, kama tamaa ikiondoka basi, wewe ni msafi na usiwe na wasiwasi. unasikia?