Nimewahi kuwa changudoa, nimjulishe?

Nimewahi kuwa changudoa, nimjulishe?

Sijui kwanini nimekupenda ghafla..!!!

Napenda sana mtu mkweli, especially Mwanamke mkweli..!! Umenivutia sana dada yangu una 60% za pendo langu..!! Huwa sipendi mwanamke Muhuni, kiruka njia ila sijui kwanini sitaki kuyafikiria haya juu yako..!!!

Hongera sana dada kama haya uyasemayo ni kweli, wewe ni mtu jasiri sana, hata kama unatumia Id ya kifocho hapa, ila kunaukweli kwenye story yako hii hatakama si 100% hizo asilimia 30 ni nyingi sana..!! Kuziweka wazi hizo tu kunaonyesha ni kiasi gani ulivyo Jasiri. Pongezi nyingi kwa hilo.

Pia dada Marytina, yakumbuke maisha uliyoishi bila huyo Mmasai, Yakumbuke maisha uliyoishi ukiwa bila mwanaume huku ukiwa umeacha Uchangudoa, Angalia ulipungukiwa kitu gani? Maisha ni zaidi ya Mwanaume, Amani Moyoni ni zaidi ya Mwanaume. Fikiria maumivu utakayoyapata baada ya kuachwa na huyo Mmasai pindi atakapogundua kwamba ulikuwa Changudoa bila wewe kumuweka wazi. Hitimisha na "Ninge" utakazokuwanazo baada ya kuachwa na huyo Man.

UKWELI NI KITU KIZURI SANA KTK MAISHA

Mwambie ukweli huyo Mwanaume akikuacha wewe utabaki na amani moyoni mwako huku ukijisifu kwa Ujasiri wako. Hilo litampa amani huyo Mwanaume kwamba kama umeweza kumwambia Black side yako hakuna haja ya kukuacha kwasababu hakuna jambo linaloumiza kama Mapenzi, sasa kama wewe umeshatumia muda mwingi ktk Mapenzi utawezaje kuendelea na jambo hilo ilhali uko kwenye Ndoa..!!!?

NAKUHAKIKISHI KAMA ANAKUPENDA KWA DHATI HATOKUACHA KAMWE.

Kutongoza sijui ila Nimekupenda sana wewe dada (Sikutongozi) kudos endelea na moyo huo huo.

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Dada piga kimya, yake kakueleza, hao wakijifanya wanakujua waambie labda wanakufananisha, tena ikibidi jifanyie mabadiliko, badilisha muonekano wako hata kwa vipodozi, style mpya ya nywele mavazi, na usiwe na mazoea nao ya karibu na wala wasimzoee boyfriend wako wala kutaka kujua unapoishi, wakukome, ishi maisha mapya, na usiishi karibu nao kabisa, kila mtu kivyake, badili maisha yako
 
Yaani umeona enh nilishtuka mapemaaaaaaaa kabisa Kama hayuko serious huyu MTU

huyo ndo Marytina a.k.a baba mngoni mama mchaga!
poleni kwa msiomjua!
kwa msaada tu pitia threada zake zote!
but still kipo kitu anataka kusema kuhusu mahusiano
vip kuhusu past zetu zinaeeza kutuhunt na kutuumiza kwenye mahusiano mapya!
vip kuhusu trust zetu,do we trust watu sahihi?
vip kuhusu tafsiri zetu za upendo?
vipi kuhusu nguvu ya matafiki na watu wa karibu kwetu?
well soma tu kimakala makala dont take it serious kuwa kuna ntu huko arusha sa hiz anazunguka sanawari na ka ist!
 
Siku jamaa akijua kupitia hao wakenya utakuwaje?
1. Kumbuka mleta mada mwenyewe kashajichanganya, kahama kanisa baada ya hao wenzake wakenya kuja kusali kanisani kwao hadi mchungaji na huyo mchumba wake wakabaki njia panda..
Hamuoni kuwa siku siri zikianza kuvuja huyo mchumba wake atakuwa na ushahidi 100% na anaweza kumuuliza sbb ya kutokuwa muwazi kabla?
2. Mleta mada hakufanya ukahaba kwa kupenda... Ni mazingira yalimlazimisha.. Hamuoni kama akajieleza maelezo ya kutosha kwa bf wake jamaa Anaweza kumuelewa kama kweli ana mapenzi ya dhati na yy?

Nwy.. Kila mtu ana kitu anachokilenga... Bt for me Marytina angefunguka tu... Kama huyo bwana Mungu kampangia atamuoa tu na kama hakumpangia bila hata kujua hiyo siri huo uchumba unaweza kuvunjia kwa sabb nyingine tu ya tofauti...
Marytina my love... Binafsi niliwahi kuwa na mchumba ambae alikuwa na mtoto.. (wakati namuapproach tyr alikuw na mtt wa miaka 2) niliwahi kumuhoji akabiambia kuwa alipewa Mimba na bf wake Wa kwanza akamtelekeza...
NIKAAMINI JUST KIRAHISI...
Bt kuna siku yule dada alinitafutia muda wa kunieleza siri nzito iliyopo moyoni mwake.. Alianza kwa kuniomba msamaha kwa kunidanganya ( wakat naanza nae mahusiano hakudhani kama tungefika mbali, so hakupenda sana kuianika siri yake kwa kila mtu) bt baada ya kuona kuwa nilikuwa serious Na yy akaona bora awe muwazi..
Story ikaanza.......
Mama yake na baba yake waliwahi kutengana na baadae mama akaolewa na mwanaume mwingine ( Alikuwa kijana tofauti na umri wa baba yake) so wakawa wanaishi na huyo baba yake mdogo au baba wa kambo ambae alikuja kuishi kwa mama yake... Siku moja mama akiwa safarini yule jamaa akambaka yule binti (alikuwa na age ya Miaka 15na alikuwa form one secondary) kwa bahati mbaya akabeba mimba na shuleni akafukuzwa.. Alipomwambia mama yake muhusika wa mimba mama akabisha na akaona iwe siri (asije akajaribu Kusema Mtu yyt akamdhalilisha mume wake) kutokana na umri mdogo yule dada hakuwa Na msaada.. Akalea mimba yake akazaa...
Aliponieleza ile siri nilimwonea sana Huruma na nikampenda zaidi tofauti na matarijio yake kuwa huenda ndo ingekuwa mwisho wa mapenzi...
Nilidumu na yule dada kwenye mahusiano kwa muda wa miaka minne ila kwa bahati mbaya tukaja kuachana kwa sbb tofauti kabisa... (niliamini Mungu hakunipangia)..

SO MPENZI Marytina KUENDELEA KUFICHA HIYO SIRI

1. Kutaendelea kukutesa nafsi na kujishuku hata kama hao wenzio wa kenya hawavujisha lakini hutakuwa na ujasiri wa kuishi kimaisha.
2. Kutokuwa na uhuru wa kufanya ibada hasa kwa sbb hao wanasali kanisa ulilokuwa unaabudu
3. Hutakuwa na uwezo Wa kuongoza kanisani kwa kudhani wenzio wanakuelewaje ilhali wanakujua mwanzo mwisho....
Imagine hao wakenya wakaja kuhamia kwenye hilo kanisa ulilokimbilia, UTAHAMA TENA?

FICHUA MAMBO UWE HURU.. Tena wahi kabla jamaa hajastuka.. Akijua kabla hujamwambia wewe KWANZA UMEKWISHA... Hatakuwa na IMANI TENA NA WEWE.. ATAKUACHA VIBAYA SANA.
First Born.....
Thanks ...so much
ntakuwa naku update kila hatua
ila nkiwa naye barabarani usiku akiona machangudoa huanza kusikitika na kufokea hata usukani wa gari...hulalamikia hata mambo yasiyokuwepo
 
Wewe ndio uamuzi wa mwisho Marytina kwahio akili kumkichwa!

next wiki ntaisoma kwa makini kila ushauri nliopewa na kuhitimisha hili jambo...
nimegundua nasumbuliwa na mambo matatu
1.imani ya dini
2.hofu ya kuachwa
3.kuolewa na kunyanyaswa kama jamaa akinikubali ikiwa siri itavuja au ntamueleza
 
Don't try please Marytina because I were him I would choose to die after knowing. Ulitakiwa useme hayo kabla hamjaoana now is too late
 
Last edited by a moderator:
Kwa sababu wakaka wanajiweka katika position ya huyu jamaa. Una mrembo wako mnapendana wote mnaona hakuna pingamizi la kufunga pingu za maisha kwa jinsi mlivyopendana. Ghafla tu mrembo wako AKA mke mtarajiwa anakuja kukwambia nina siri ambayo imekuwa ikinitafuna kwa siku nyingi sasa. Unafunguka vile utakavyofunguka ili kumwambia kwamba kuna wakati uliwahi kujiuza. Kwa wanaume hii ni ngumu kumeza 99.9% wataingia mitini bila kujali sababu zilizikufanya uamue kujiuza. Huo ndiyo ukweli halisi wakaka hawakutaka kumung'unya wamekwambia ukweli huku wakijiweka wao katika nafasi ya huyo mume mtarajiwa. Kila la heri katika maamuzi yako.

thanks so much
nlichogundua wadada JF wameridhia niseme ukweli ila wakaka hawataki kabisa niseme sasa hapa ipo kazi....
 
mamito..............
wewe ndo unaoujua ukweli wa maisha yako yote, na pia ndo pekee unayeweza kufeel aina ya mahusiano uliyonayo.
ushauri wangu kwako huu............

kwasabb umeokoka basi mshirikishe sana Mungu kwanza ili Mungu akupe njia ya kutokea. kisha ukipata amani basi mweleze kwa ukimya tena iwe kama vile unampa historia ya maisha yako yote na pia umwambie msimamo awako kwasasa. Kisha chukua hatua kumfanya akuamin meaning michepuko, acha, kampani mbaya acha, tulia uwe mke, na mama wa watoto wa mumeo.

kuna machangudoa kibao wameolewa na wametulia na ndoa zinazidi kukua kukua. Uzuri ni kwamba ukisha jua tatizo lako na sasa umeamua kubadilika basi take it badilika wala usimwogope mtu eti atamwambia.

cha kufanya just be open na hata juu ya uwepo wa hao ulokuwa nao huko nairob ambao unawahofia mweleze ukweli

asante na nikupe hi....ni siku nyingi hatujapostiana mimi na wewe

niko mdhaifu sana juu yake ...........yaan najutaaa hata kwa nini skumwambia day one.
 
Mwenyewe nilimshtukia ana taka ushauri lakini ana mawazo yake tayari. Kila ushauri anabisha kwa kuweka visabu Mara ooh sijui nini.
mmmh! tatizo ni kwamba bila utani hutapata mtazamo halisi wa watu
utani gives connectivity....mtu anakushauri ukimpa visabu anabadili ushauri wa awali hapo najua hakujipanga
by the way nawapenda wooote jaman
 
Yaani umeona enh nilishtuka mapemaaaaaaaa kabisa Kama hayuko serious huyu MTU
niko serious ila pana kaukweli ndani ya majibu yangu
ni kama vile hamuungani na majibu nliyokuwa nimeyapanga...........unajua wakati mwingine mshauriwa anataka kusikia kile alichokwisha kupanga yeye na hili ndio tatizo.
 
what if i keep it down as posibo ila akajajua baadae kupitia kwa wadada wakenya ambao wako hapa AR?
si unabisha tu! kwani wana video waliyokurekodi ukijiuza? nakushauri baki kimya
 
mweleze historia yako na sababu ya kujiuza. Yawezekana hata yeye alishawahi kufanya mabaya kuliko hayo. Ila maisha yako yaonekane yemebadilika kabisa.

Hata kwenye bibilia kuna nabii aliambiwa akamuoe mke wake aliyemuacha aliyekuwa anajiuza barabarani.
Badilika na Mtegemee Mungu. aatakupa mahitaji ya Moyo wako.
 
sikuwahi kufanya kinyume na maumbile
pia kuna wadada wakenya wako hapa AR wanaweza kuvujisha hii siri ikawa msala zaidi sjui hata nianzie wapi..

Nakushauri anza na mchungaji wako mweleze ukweli then umwambie boy wako historia yako maana hao wanaweza kuja kutoa siri utaabika ingawa ni ngumu lkn utakuwa huru kwa mungu wako
 
hallow wapendwa
tuelekee makanisani saa saba............tuombeane
 
Kama lengo ni kumshirikisha maisha yako ya zamani mshirikishe ila habari ya ndoa sahau maana atakuacha tu.

Ni wanaume wachache sana wanaweza kuendelea na mahusiano na mtu mwenye historia kama yako(mimi siwezi) nadhan hata bwana yako hawezi.
 
Duh nafikiri ushauri umekutosha. Leo anza mchakato wa kumwambia mchungaji. Tukirudi nyuma, ni msichana gani hapa hajafanywa na zaidi ya wanaume 10 toka azaliwe?? Huo siyo uchangu?? Ni mwanaume gani hajafanya wanawake zaidi ya 20? Huo siyo umalaya?? Sote hapa tu wazinzi tu. Atakusamehe!
 
Kwani kwa jinsi wewe mwenyewe unavyojiona bado una elements za uchangu? Au tangu uanze uhusiano na huyo mmasai mmewahi kugombana chanzo kikiwa ni wewe kum-cheat?
 
Duh nafikiri ushauri umekutosha. Leo anza mchakato wa kumwambia mchungaji. Tukirudi nyuma, ni msichana gani hapa hajafanywa na zaidi ya wanaume 10 toka azaliwe?? Huo siyo uchangu?? Ni mwanaume gani hajafanya wanawake zaidi ya 20? Huo siyo umalaya?? Sote hapa tu wazinzi tu. Atakusamehe!

Mkuu kufanya na wangapi sio shida, je hiyo list ya uliofanya nao ulimu hadithia mwenzako.? Chamsingi ni yaliyopita si ndwele mgange yajayo kwanini kudeal na yaliyo pita.?
 
Back
Top Bottom