Nimetumiwa ujumbe huu WhatsApp

Nimetumiwa ujumbe huu WhatsApp

Hii niliipata nikaingia naye whatsapp.

Akanitumia maelekezo ambayo yanahitaji nideposit 10,000 kwenye akaunti zao kisha ndiyo nianze kufanya kazi.

Nilichohisi huenda ni roboti.

Maana ukiuliza swali hata la aina nyingine jibu linalokuja ni la kukueleza juu ya mfumo wao unavyofanya kazi.

Mtu wangu wa karibu akawa approached pia.

Huyu mtu wangu wa karibu tuna sifa sawa;
  • Wote ni job seekers.
  • Wote tupo linked in.
  • Wote tumeapply in same company recently.

Nikahisi namba wametoa huko.
Usipokuwa makini unaliwa kichwa
 
Hiyo namba yako umeisajil na email nadhan...wazush hao achana nao
 
Huyo piga block mkuu. Vinginevyo baada ya masaa machache utatumiwa meseji ya TIGOPESA "you have successfully withdrawn all your TIGOPESA balance"
 
Mkuu umetaka ushauri JF na humu kuna hazina kubwa ya watu wenye uzoefu wa kugundua mienendo ya kitapeli ... Jamaa amejipamba tayari na anakutaka na wewe ufunguke, ukitaka kuhakikisha kuwa wanaokushauri humu wako sahihi, basi jifanye unataka urafiki nae uone mwisho utakuwaje. Kwa hakika utajifunza kitu.
Kama ambavyo ungeweza kupita kimya kimya ukaokoa muda wako.
Ninyi watu mlioko serious kiasi hiki sijui huwa mnategemea nini maishani. Maisha ni haya haya mkuu tunabadilishana mawazo sometimes tunakutana kwenye vijiwe, wala server haijalalama wewe tu jiepushe na mambo ya kupoteza muda wako km haya, heri ya pasaka.
 
Puuzia tu Mkuu. Utapeli wa kizamani sana, miaka zaidi ya 20 iliyopita. Kipindi hicho watu wengi hawakuwa na ufahamu wa utapeli wa mitandaoni hasa wabongo, baadhi yao waliingia kwenye mitego kama hii.
 
Yalinipata hayo 2015 maelezo hayo hayo ila yeye alisema yuko umoja wa mataifa anahudumia wakimbizi ataniletea zawadi afrika senegal na picha ya zawadi alibughi usafiri wa treni kati ya sengal na afrika mashariki generally ni matapeli wanakuvuta
 
Mimi wamenitumia Messenger

Hi Dear,Compliments to you and thanks for taking your precious time to reply to my mail. I am more than happy and grateful to you. I know you will be a good and honest friend. What can I say? okay let me tell you a little bit about myself and with time we will know more about each other okay.I am Doctor Jennifer Addison, born and brought up at 24 Burwood road Burwood NSW213,4 Australia into a family of three, I am 32 years old, single with one daughter schooling in Ashburton drive primary school Australia, again have a Palestinian root too, from my grand parents. I was raised in a Christian family, my father is a pastor who works with CHRISTIAN HUMANITARIAN ORGANIZATION. Christian humanitarian organization vision is to bring hope and change for the betterment of sick, poor and needy.
I attended my high school's Basing hall. After that I proceeded to Charles Darwin University of Australia, for my University career and graduated. Presently I work with Queensland hospital as a Doctor in the Medical Department and I have also lived and worked at American Hospital in the Philippines for 4 years.
Serving God is my top priority in life because I believe that nothing ever exists without the permission of God, this makes me believe in the joy of friendship, a thing that has given me the opportunity of knowing you. So how are you coupling with life? How is your country? l have not had any opportunity to be outside of my country to any other country except Singapore, Sweden and Haiti. I hope I know you will make an avenue for me to be there someday by God's grace. This is just a little about myself and I hope you will tell me about you, your nation, occupation and everything that is worth knowing about you okay. Please I am here strictly for friendship and maybe more with time.These are some of my pictures, please I want to see any of your pictures.
Regards
Screenshot_20220417-103941.jpg
Screenshot_20220417-104011.jpg
 
[emoji16][emoji16][emoji16] sawa mkuu, naona wadau wakinambia ntalizwa, sasa sielewi ntalizwa vipi maana hii namba haina connection zozote na akaunti yangu ya benki, pia mpesa hakuna kitu, afu pia mtandaoni nina akaunti Samsung, google na microsoft pekee.
Mkuu, hawa jamaa uwa wanatumia taarifa zako binafsi kukushawishi ili wakurubuni. Suluhisho ni kupuuza tu.
 
Kama ambavyo ungeweza kupita kimya kimya ukaokoa muda wako.
Ninyi watu mlioko serious kiasi hiki sijui huwa mnategemea nini maishani. Maisha ni haya haya mkuu tunabadilishana mawazo sometimes tunakutana kwenye vijiwe, wala server haijalalama wewe tu jiepushe na mambo ya kupoteza muda wako km haya, heri ya pasaka.
Ok. Kula maisha kadiri unavyoweza mkuu,hakuna wa kukuzuia!. Sipotezi chochote kwa kutoa maoni yangu humu hasa kwa kile ninachokijua. Pasaka njema kwako pia.
 
unashindwa kujua kabisa huo ni utapeli mzee
 
mimi sister angu alishawahi kupigiwa hadi video call na mzungu kabisa akijiambulisha ni dr wa UN huko Australia na ana ndoto za kuja kutembelea bongo one day ,baadae akaambiwa kuna zawadi na pesa atamtumia ili amwandalie mazingira akija bongo ,na picha ya mzigo akatumiwa Whatsapp kabisaa ,akaambiwa baada ya siku mbili ndege itakuwa imefika ko aanze process za kuuchukua ,baada ya sku mbili kweli akapokea simu ,anaongea mbongo kuwa kuna mzigo wako hapa kigoma umeletwa na ndege ya UN kutoka Australia umekuja na vitu vya misaada ya wakimbizi ,jamaa akamwambia atume laki 3 kwa ajili ya kufanya clearence airport na mzigo wake utumwe dar. sister hapo ndo akanipigia kunipa stori nzima ,nikamwambia anipe namba ya huyo jamaa ,kuongea naye jamaa nikashtukia ni tapeli lakini usipokuwa makini ni ngumu sana kushtukia mchezo wao . mtandao wa utapeli ni mtandao mkubwa sanaa ukijichanganya tu unapigwa , sister alikua kidogo tu atume 300k kama asingenishirikisha .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom