Nimetumiwa mzigo kutoka Uingereza kuja Afrika Mashariki

Habari za wakati huu wapendwa,

Wana Jukwaa, naomba ufafanuzi. Kuna mtu amekutumia zawadi ya iPhone, laptop, na pesa taslimu $1500. Naomba msaada kwa wale wazoefu, maana mzigo ulitumwa jana usiku na umefika Kenya katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi.

Naomba msaada kutoka kwa wale wenye uzoefu, ni kweli au ni uwongo? Sijui kama ni matapeli au la. Mzigo umewasili asubuhi ya leo na wameniambia niulete Tabora, lakini wameniambia kuna gharama ya kusafirisha ya Tsh 70,000 kuja Tanzania.

View attachment 2934123View attachment 2934124View attachment 2934125View attachment 2934126
Hao ni matapeli
 
Ndugu,Achana kabisa na hao watu.. Ni matapeli, tena hawapo mbali ni matapeli wa hapo Kenya Nairobi. Watakukausha hela zako kwa kigezo cha kwamba ni hela ya kusafirisha au kukomboa hivyo vitu.
 
Last month yalinikuta hayo Ila kwakuwa born town walikimbia wenyewe
 
Wanaitafuta 70,000/= yako ndugu yangu. Yaani acha vyote hivyo mtu akutumie bure $1500 x 2550 =3,825,000/= ashindwe kukulipia hiyo 70K. PIa huko Majuu wana-scan huwezi pitisha hizo Dollar wakakuacha salama
 
Hivi kumbe aina hii ya utapeli bado ipo?!. Watu wamelizwa sana miaka ya nyuma. Halafu mbaya zaidi bidhaa zinazotumwa kama zawadi ni zile zile. Iphone, laptop, camera na pesa.
 
Habari za wakati huu wapendwa,

Wana Jukwaa, naomba ufafanuzi. Kuna mtu amekutumia zawadi ya iPhone, laptop, na pesa taslimu $1500. Naomba msaada kwa wale wazoefu, maana mzigo ulitumwa jana usiku na umefika Kenya katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi.

Naomba msaada kutoka kwa wale wenye uzoefu, ni kweli au ni uwongo? Sijui kama ni matapeli au la. Mzigo umewasili asubuhi ya leo na wameniambia niulete Tabora, lakini wameniambia kuna gharama ya kusafirisha ya Tsh 70,000 kuja Tanzania.

View attachment 2934123View attachment 2934124View attachment 2934125View attachment 2934126

Wakenya hao watumie hela uone!!!!?
 
😂😂😂😂😂😂

Bora umekuja huku
Umenikumbusha kuna mtu tulimpa ushauri asitume hela hiyo tunajua huo utapeli akakaza kichwa

Ati tunataka kuingilia penzi lake😂😂😂

Lilikufa jitu kesho yake job mtu amenuna sisi tunacheka
 
Baba angu anajifanyaga muhuni anajua mbinu zote za wahuni coz kaishi nao sana SA. Ila siku moja nilimvua vyeo alipokua ananiuliza jinsi ya kupokea mzigo wake wa laptop kutoka kwa rafik yake wa Facebook.
Nilicheka sana
😂😂😂
 
Nakushauri utatapeliwa,mdogp wangu alipata mchongo kama huo ila sasa wenyewe ni kutoka US.
Dola 5k
Laptop 6
Computer 2
Saa 2
Cheni
Nguo

Kiufupi kuja kushtuka 500k imeenda. Hao jamaa wajanja sana. Yeye mzigo aliambiwa umefikia morogoro. Nikajiuliza ndege imetoka US imetua dar ila mzigo umeendq kushushwa morogoro!! Nikasema matapel hawa.

Dogo akabisha akawatumia hela ya usafiri ili mzigo utoke kule uje dar, baada ya kutuma hela wakamtumia risit.

Kisha wakamwambia atume hela ya vat akatuma tena aisee. Nisiendelee sana kiufupi usitume pesa yoyte
 
Kuna mwanangu naye alipigwa hivi hivi nilimshauri asitume pesa kilichomkuta sasa alikula za uso.
 
Kuna dogo nimemkuta jana kainamia desk top anachat na hao matapeli, uzuri akaongea kabla hajaulizwa kwamba kuna rafiki yake anachat nae kamtumia mzigo, wamekosa ndege ya moja kwa moja Dsm hivyo wameushushia Jomo Kenyatta Airport😁😁

Nikamuuliza kama anafahamiana nae kwa sura, akadai ni rafiki yake wameshaonana zaidi ya mara 1, nikamwambia dogo unakwenda kupigwa muda si mrefu (Aliambiwa kutumiwa mzigo Tsh. 77,000).
 
hahahahah hivi zama hizi za world rimit,Nala,sendwave kuna mtu anaweza tuma $1500 kwa njia hiyo?
 
Back
Top Bottom